Maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanzania yafana sana leo uwanja wa uhuru jijini dar

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,886
2,000

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akiwasalimia wananchi alipokua akiwasili uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akipokea salam ya Rais na kupigiwa mizinga 21 kutoka kwa gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi ya Tanzania leo uwanja wa Uhuru mara baada ya kuwasili.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akikagua gwaride la vikosi vya majeshi ya Ulinzi na usalama leo uwanja wa Uhuru wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.

Sehemu ya askari wa vikosi vya ulinzi na usalama wakiwa wamesimama kwa ukakamavu wakati kabla ya kamanda wa gwaride kumkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kukagua gwaride hilo leo jijini Dar es salaam.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete akiwasili jukwaa kuu la Uwanja wa Uhuru wakati wa sherehe za maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo.

Gwaride likipita mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu kwa mwendo wa haraka.

Rais Jakaya Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakati gwaride la vikosi vya Ulinzi na Usalama likipita mbele ya jukwaa kuu la uwanja wa Uhuru kwa mwendo wa haraka.

Baadhi ya Maofisa wa jeshi wakipiga saluti wakati wimbo wa Taifa ukiimbwa wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru leo jijini Dar es salaam. Picha na 9.Wananchi wa mkoa wa Dar es salaam waliojitokeza kuhudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru uwanja wa Uhuru leo jijini Dar es salaam.

Wananchi wakifatilia

Vijana wa halaiki kutoka Tanzania Bara na Visiwani wakitamka kauli mbiu ya maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara leo jijini Dar es salaam ambayo ni “ Vijana ni Nguzo ya Rasilimali Watu,Tuwaamini, Tuwawezeshe na Tuwatumie kwa Manufaa ta Taifa Letu”.

Vijana wa halaiki wakiendelea kuwasilisha jumbe mbalimbali kama inavyoonekana mfano wa mnyama aina ya samba kuashiria utalii katika hifadhi za wanyama za Tanzania.

Vijana wa halaiki wakionyesha ukakamavu.

Baadhi ya Maafisha wa Jeshi wakitoa salamu.

Ujumbe ukiwasilishwa kwa njia ya picha kuhusu viongozi wapigania Uhuru wa Tanzania Bara, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akitoa hatuba fupi kwa watanzania wakati wa maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara, Hatuba yake licha ya kujaa maneno ya kumkumbuka rais wa kwanza wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Rolihlahla Mandela Madiba aliyeaga dunia juzi nchini Afrika ya Kusini imesisitiza Upendo, Amani, Mshikamano miongoni mwa watanzania na kukemea tabia ya baadhi ya viongozi kulipiza kisasi pindi waingiapo madarakani.

Rais wa Zanzibar Dkt Ali Mohamed Shein (kushoto), Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete (katikati) na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo katika uwanja wa Uhuru wakati wa Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.

Raia wa kigeni waliohudhuria sherehe za miaka 52 ya Uhuru wa Tanzania Bara wakisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.

Rais Jakaya Kikwete akifurahia jambo na Mkuu wa Majeshi Generali Davis Mwamunyange alipokua akisoma Jarida la Nchi Yetu linalochapishwa na Idara ya Habari (MAELEZO) leo.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru. Picha na Aron Msigwa - MAELEZO


Chanzo Michuzi
 

Kakke

JF-Expert Member
Dec 4, 2010
1,886
2,000
Tanzania imepata uhuru kutoka kwa mtawala gani? Musijihashue na kujifanya comfuse kwa kuikana Tanganyika yenu ,kwani kuna aibu gani kusema hizi ni Sherehe za Uhuru wa Tanganyika.Mbona munajizalilisha na kujitowa samani ya kuikana Tanganyika.

Mbona Wazanzibar hawaoni aibu kusherehekea Uhuru wao wa Zanzibar Jan 12/1964.
 

Ciril

JF-Expert Member
Jan 10, 2011
8,562
2,000
Me nnataka tu kujua imetumika bilioni ngapi na ngapi zimeingia mifukoni mwa wezi ndani ya Serikali ,alipokuja Obama hapa tulishuhudia kuripotiwa habari kuwa wezi wanaoitwa wajanja waliweka mifukoni mwao kiasi kadhaa.
 

Threesixteen Himself

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
8,207
2,000
!
!
Tanzania haijawahi kutawaliwa kwa hiyo kuwa na sikukuu ya uhuru wa Tanzania ni ubatili mtupu. Leo ni siku ya uhuru wa Tanganyika.
 

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
0
Watanzania wote ni mashahidi kuwa Viongozi wa CHADEMA miaka yote wamekuwa mstari wa mbele kususia shughuli za Kitaifa,sijajua sababu nini?Lakini leo hii Mbowe kashukiwa na malaika wa Mungu na kuamua kushiriki siku ya Uhuru,Ni imani yangu kuwa nafsi yake imemsuta kuwa kiongozi bora hasusii mambo,hasusii kazi za Kitaifa,Ni yule anayeongoza Wananchi wake kwenye upande sahahi,upande postive kwa manufaa ya Nchi.Hongera Mbowe kwa kujikanya,kwa kusemezana na moyo wako.Bado Dr.slaa hajajitambua yeye ni nani kwa taifa hili,ipo siku atafunguka akili yake na kushiriki mambo muhimu kama haya.Mandela hakuwa Hivi kama slaa.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye naye pia leo anasherehekea maana halisi ya jina lake kutokana na kuzaliwa mwaka uliopatikana Uhuru wa Tanzania, mwaka 1961. na ndiyo maana akaitwa Freeman.
 

Chikaka Sumuni

JF-Expert Member
May 16, 2013
1,337
0
Watanzania wote ni mashahidi kuwa Viongozi wa CHADEMA miaka yote wamekuwa mstari wa mbele kususia shughuli za Kitaifa,sijajua sababu nini?Lakini leo hii Mbowe kashukiwa na malaika wa Mungu na kuamua kushiriki siku ya Uhuru,Ni imani yangu kuwa nafsi yake imemsuta kuwa kiongozi bora hasusii mambo,hasusii kazi za Kitaifa,Ni yule anayeongoza Wananchi wake kwenye upande sahahi,upande postive kwa manufaa ya Nchi.Hongera Mbowe kwa kujikanya,kwa kusemezana na moyo wako.Bado Dr.slaa hajajitambua yeye ni nani kwa taifa hili,ipo siku atafunguka akili yake na kushiriki mambo muhimu kama haya.Mandela hakuwa Hivi kama slaa.

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendelo Freeman Mbowe akiwa miongoni mwa viongozi wa vyama vya siasa waliohudhuria maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru.


Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ambaye naye pia leo anasherehekea maana halisi ya jina lake kutokana na kuzaliwa mwaka uliopatikana Uhuru wa Tanzania, mwaka 1961. na ndiyo maana akaitwa Freeman.

As young as you seem to be, Hon Mbowe is leading a party that is a government in waiting. Hope you did listen from Kikwete's speech recently when he told his party fans that CCM won't won the upcoming elections due to chronic Corruptionphobia.
 

Vikao vya Harusi

JF-Expert Member
Sep 19, 2012
498
250
As young as you seem to be, Hon Mbowe is leading a party that is a government in waiting. Hope you did listen from Kikwete's speech recently when he told his party fans that CCM won't won the upcoming elections due to chronic Corruptionphobia.

Weka picha na video,ili uthibitishe kuwa kikwete alisema hayo


Halafu kuhusu suala la umri,kama ww unajiona mtu mzima sana,wazima wenzako wanapewa salute kule jeshini
 

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
1,507
2,000
Nimeamini ule waraka ni wa kweli Kabisa. "Too local Mbowe."
Anastahili amuhachie Zzk alete mabadiliko kwenye CHAMA.
Na members wa CHADEMA tukubali mabadiliko sasa. Tusiwe na MAWAZO Mgando saaaaaaaaaana!!
 

kamtu33

JF-Expert Member
Mar 15, 2012
999
1,500
Anajifunza kitu tukitimiza miaka 54 ya uhuru chini ya serikali ya CHADEMA arekebisheje mambo.
Hongere comred Mbowe!
 

mtz one

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
4,211
2,000
Teh magamba mkikosaga cha kuandika mnaandikaga chochote
ninawasi wasi akili yako ni kama ya hiyo avatar ni wadhaifu mno ktk kutetea hoja hivi mbowe na chadema si mnapingaga maadhimisho sasa mbona leo kaenda kujipendekeza??
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom