Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika/Tanzania bara

Katika hotuba yake ya kuadhimisha miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika,kikwete amesema watu tuwe na moyo wa kusameheana.Alisema, na nukuu"wengine hapa wanatamani wakichaguliwa watanikoma".Je,kikwete anamaanisha serikali ya ccm ni ya kikoloni,kibaguzi au ya kikaburu? Anamaanisha kuwa kwa mateso kwa raia,mauaji ya raia,ufisadi uliopo unaofanywa na ccm kwa kuwa ccm ni serikali ya kikoloni? Je,yeye ni rais wa kikoloni? Kwa kauli ya kikwete,ccm wamepoteza uhalali wa kutawala nchi,kumbe tunatwaliwa na makaburu(yaani CCM).Je,anafanya maovu makusudi ili aje kusamehewa kama makaburu wa S.A?
Kwani wewe una mtazamo gani.
 
CCM siyo serikali, bali kakikundi cha wahuni wanaotawala serikali utadhani wale wadudu wanaokula mahindi sijui wanaitwa scania!

CCM ni majangili fulu!

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Leo tarehe 9.12.1961 Tanganyika inakabidhiwa uhuru wake kutoka katika makucha ya wakoloni waliomnyonya mtanganyika miaka na miaka. Leo desemba 9 hapa uwanja wa uhuru, mwalim julius ka,barage Nyerere anakabidhiwa nchi hii na hivyo kuwa rais wa kwanza wa tanganyika na kukomesha utawala dhalimu wa mkoloni.

kwa kumbukumbu hiyo, leo tarehe 9 desemba 2013 tunakuletea live updates za yanayojiri uwanja wa uhuru ambapo rais wa nne wa jamhuri ya muungano wa tanzania anakuwa mgeni rasmi kusherehekea makabidhiano ya tanganyika huru.


Televisheni ya taifa, tbc1 na radio tanzania/ tbc fm wanarusha moja kwa moja maadhimisho haya ya 52 ya uhuru wa tanganyika.

tufuatilie.


TANGANYIKA INDEPENDENT - British Pathé

Tuwaeleimishe watoto kuhusiana na Uhuru huu
 
Tumezoea kusema yale ambayo Nyerere alimwambia JK wakati akigombea urais 1995, moja wapo ni kuwa bado mdogo asubiri, katika hali ya ajabu watu tukiwa tunakuna vichwa kuwa alikuwa mdogo vipi wakati umri kikatiba ulitimia, leo JK katoa siri nyingine nzito kuhusu Mzee Madiba.

Mzee madiba akiwa mcheshi kwa maneno ya JK, wakati JK alifuatilia kurejeshea viatu vyake alivyovicha kwa mhazina wa CCM Enzi hizo na baadaye waziri wa mipango, somebody Swai au laswai. Madiba alikutana na JK mara kadhaa ndipo akaamua kufunguka. Madiba alimwambia JK mbona unaendelea kukua kwa maana ya kimo??? JK akajibu kama sayansi inaruhusu mtu wa miaka 45 akuendelee kukua kwa kimo basi itakuwa hivyo.

Hapa naona JK aliingia kichwa kichwa mtego wa Madiba, wa kutumia fahisi kufisha ujumbe, JK kweli hadi anasimulia leo anaamini mZee Madiba alinotice JK kuendelea kurefuka kimo kitu ambacho kama n kweli basi madiba atakuwaa mjingaaa mno. Siamini madiba alisema juu ya kimo, nafahamu alijua JK alikuwa anafanya utoto mwingi ktk mambo ya msingi, ama alimuona anapelea sana kiasi kwamba anahtaji kukua kimaarifa , akili na uwezo na wala sio kimo chake.

Cha msingi hapa ni ukweli kuwa Madiba aliona na kusema kile kile Nyerere alisema kwa staili yake. JK bado anakua?????

Nawasilisha
 
Back
Top Bottom