Maadhimisho ya miaka 52 ya Uhuru wa Tanganyika/Tanzania bara

utaifakwanza

JF-Expert Member
Feb 1, 2013
14,193
2,812
Leo tarehe 9.12.1961 Tanganyika inakabidhiwa uhuru wake kutoka katika makucha ya wakoloni waliomnyonya mtanganyika miaka na miaka. Leo desemba 9 hapa uwanja wa uhuru, mwalim julius ka,barage Nyerere anakabidhiwa nchi hii na hivyo kuwa rais wa kwanza wa tanganyika na kukomesha utawala dhalimu wa mkoloni.

kwa kumbukumbu hiyo, leo tarehe 9 desemba 2013 tunakuletea live updates za yanayojiri uwanja wa uhuru ambapo rais wa nne wa jamhuri ya muungano wa tanzania anakuwa mgeni rasmi kusherehekea makabidhiano ya tanganyika huru.


Televisheni ya taifa, tbc1 na radio tanzania/ tbc fm wanarusha moja kwa moja maadhimisho haya ya 52 ya uhuru wa tanganyika.

tufuatilie.
 
Hivi sasa ni shamrashamra za hapa na pale, watu kibao, furaha, vifijo na nderemo kila kona ya uwanja wa uhuru na mitaa mbalimbali ya jiji. Wageni na wananchi mbalimbali wanazidi kumiminika haa uwanjani
 
Wabunge wa bunge la jamhuri ya muunano wa tz pamoja na wale wa baraza la mapinduzi znz wameingia hivi punde
 
Vikosi vya ulinzi na usalama vimeingia uwanjani tayari kwa gwaride
 
Mawaziri wakuu wastaafu wameingia hapa, john malecela, warioba, salim ahmed salim
 
Viongozi wa vyama vya siasa, prof. Lipumba, mbowe na mangula wameingia
 
Na sasa tanganyika inatawaliwa na mkoloni mweusi ccm nae anamwaka tu aondoke na utawala wake wa kidhalumu
 
Tangu waamie digital, tbc mikoa mingi haipo. Matangazo hayo ni yenu huko dar siyo mikoa ya pembe zoni.
 
Rais mstaafu wa znz amani abeid karume ameingia na pia katibu mkuu kiongozi ombeni sefue
 
Mimi nasubiria maadhimisho ya UHURU toka kwa mkoloni mweusi ccM hapo 2015!!
 
Safi mbowe leo kahudhuria... waraka kausoma vizuri ni vyema wakiyafanyia kazi yaliyomo kwenye waraka hata kama watawaadhibu waliouandika.
 
Back
Top Bottom