Maadhimisho ya kimataifa ya siku ya haki za binaadamu: Waandishi wa habari 42 wameuawa wakati wakitekeleza majukumu yao

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
3,376
2,000
Ripoti mpya ya kila ya mwaka ya Shirikisho la Kimataifa la Waandishi wa Habari IFJ, lenye makao yake nchini Uholanzi, inasema waandishi wa habari 42 na wafanyakazi wa vyombo vya habari wameuwawa wakati wakitekeleza majukumu yao kwa mwaka huu pekee.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo iliyotolewa jana Jumatano, inayolegea siku ya leo ya maadhimisho ya kimataifa ya siku ya haki za binaadamu inasema watu wengine wapatao 234 kwa sasa wapo magerezani kwa kesi zenye kuhusisha kazi zao.

Kiwango cha vifo kinakaribia kufanana, kile kilichokuwa kikifanyiwa majumuisho ya mwaka na shirika hilo takribani miaka 30 iliyopita.

Shirika hilo lenye wanachama 600,000 kutoka mataifa 150 duniani kote limesema Mexico inaongoza kwa idadi kubwa ya waandishi wanaouwawa kwa mara nne katika kipindi cha miaka mitano, kukiwa na mauwaji 13, ikifuatiwa na Pakistan watano. Mataifa mengine Afghanistan, India, Iraq na Nigeria ambapo kwa kila moja kumetokea vifo vitatu, vitatu.

CHANZO: DW Swahili
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom