Maadhimisho wiki ya sheria: ''Aibu yetu''

kunguni wa ulaya

JF-Expert Member
Mar 16, 2014
4,131
6,109
WIKI YA SHERIA ..
"AIBU YETU" ANAANDIKA WAKILI MSOMI JUMA NASSOR

Wakili Juma Nassoro

AIBU YETU

sheria ya kuzuia ugaidi ilipitishwa na bunge mwaka 2002 na kusainiwa na Mhe. Rais Mkapa 2004.

Sheria hii baada ya kupitishwa na bunge na kusainiwa na rais wa wakati huo haikuwahi kutumika mpaka awamu ya mwisho ya Mhe. Rais Kikwete.

Sheria hii ilipokuwa inapitishwa na bunge mwaka 2002 wanasheria nguli Tanzania maprofesa Issa Shivji na Abdallah Safari pamoja na wananchi wengi walikosoa utungwaji wa hii sheria kwasababu mbili kubwa kwanza imetoa mamlaka makubwa sana kwa askari polisi kutumia nguvu zisizohojiwa dhidi ya yeyote anayemhisi kuwa gaidi kabla hajatiwa hatiani lakini pia sheria hii imekuja na makosa yanayoitwa ya kigaidi ilihali makosa hayo tayari yalikuwa na sheria zake na adhabu zake.

Lakini kwa kuwa kulikuwa na nguvu kubwa ya kidunia sheria ilianza kutumika.

Katika awamu ya mwisho ya rais Kikwete ndipo watanzania tulianza kushuhudia watu wanaoshitakiwa kwa ugaidi.

Hata hivyo hakuna hata kesi moja mpaka sasa iliyowahi kusikilizwa ushahidi ulitolewa na kisha mtuhumiwa anatiwa hatiani au kuachiwa. Kesi zote zimekuwa ama DPP aliiondoa kwa kuwa hakuwa na nia ya kuendelea nazo au bado ziko mahakamani zikipigwa danadana upelelezi haujakamilika.

Hii ni aibu kubwa sana kwetu wanasheria na hasa ofisi ya DPP na polisi Upelelezi.

Sio sifa ya DPP na polisi kujaza watuhumiwa wa ugaidi mahakamani bila kesi zao kusikilizwa. Sifa kwa DPP ni kumfikisha mtuhumiwa mahakamani ushahidi utolewe adhabu aipate afungwe au la aachiwe ikiwa ushahidi hautoshi.

Sheria hii imekuwa mwiba kwa masheikh waalimu wa madarasa na maimam wapo wametapakaa magerezani hakuna kesi hata moja zinazo wakabili imeshawahi kusikilizwa zaidi ya miaka mitatu sasa au miwili

Imekuwa malalamiko, masikitiko na huzuni kwenye nyumba za ibada na familia mbalimbali zinazowahusu masheikh waalimu wa madarasa na maimamu. Tumeshuhudia madrasa zilitungwa au kuvamiwa kusaka magaidi.

Hili ni tatizo na linaleta hisia mbaya kwa jamii kubwa.

Leo tunaanza mwaka mpya wa mahakama 2017 kauli mbiu UTOAJI HAKI KWA HARAKA KUWEZESHA KUINUA UCHUMI. mhe. Kaimu Jaji Mkuu na Mhe. Mwanasheria Mkuu wa serikali wametoa hotuba nzito na nzuri juu ya umuhimu wa utoaji haki kwa haraka na kwa wakati. Watuhumiwa wa ugaidi ni watu hawajatiwa hatiani wanayo haki kesi zao kusikilizwa kujua hata yao. Tunatoa aibu

Zipo kesi kubwa za mauaji, madawa ya kulevya, uhujumu uchumi na nk nk zilifunguliwa baada ya kesi hizo za ugaidi zimesikilizws na hukumu kutolewa. Kuna nini kwa hawa watuhumiwa wa ugaidi?

Historia imemnukuu waziri wa mambo ya ndani amewahi kusema kuwa Tanzania hakuna ugaidi, huyu ndiye waziri ambaye polisi wanaopeleleza na kukusanya ushahidi wa tuhuma za ugaidi wako chini yake. Na Waziri huyu si miongoni mwa wakurupukaji naamini ana yakini na alichokisema.

Watuhumiwa wa ugaidi ni aibu yetu katika tasnia ya sheria aibu aibu aibu
 
Back
Top Bottom