issenye
JF-Expert Member
- Feb 2, 2011
- 3,781
- 5,205
Ndugu Watanzania wenzangu, leo tunakumbuka miaka 12 toka Muasisi wa Taifa hili la Tanganyika Mwalimu J. K. Nyerere kufariki dunia, pamoja na kuwashwa kwa mwenge wa uhuru ikiwa na maandaliozi ya sherehe za miaka 50 ya kujitawala (Sio Uhuru kama wanavyotaka tuamini). Lakini cha kushangaza Rais wa nchi hatahudhuria sherehe hizo bila sababu zozote za maana. Je hii inamaanisha bado ana hasira na maneno ya Mwalimu aliyosema kuwa bado muda wake wa kuwa Rais haujafika?