MAADA: Miaka miwili ya serikali ya awamu ya tano, nini mafanikio na changamoto?

GANG MO

JF-Expert Member
Dec 6, 2016
2,087
2,193
Habari ndugu zangu wa jf. Hii ilikua ni maada iliyorushwa jana na ITV kupitia kipindi cha malumbano ya hoja. Kwa aina ya watu waliokuwa wanachangia na namna wanavojenga hoja napata shida kuwaelewa watz. Okey niachane na hao. Najua hapa jf kuna wasomi na watu mahili wa kujenga hoja na kudadavua mambo. Hebu nasi tulumbane kwa hoja katika hiyo maada inayosema:
'MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO, NINI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO?'. Nawasilisha
 
Mafanikio kiukweli ninazidi kufurahia makampuni ya bet yanaongezeka na punde kila Mtanzania ataweza kubet, tunaomba elimu stahiki itolewe mashuleni kwenye hii michezo ya betting ili iwe sehemu ya ajira ya nchini.

Changamoto: ni Umeme kwa sisi tunaobet uwepo umeme wa uhakika tusitoke online maana wengine tunacheza sana Inplay.
 
Tanzania ingekuwa na bunge imara tungesha ondoa MTU aliye fail kuongoza bali anatawala kama sultani.
Kwa hiyo changamoto ni moja tuu, kutokuwa na bunge imara
 
Mafanikio ;kila kukicha makampuni ya michezo ya bahati nasibu yanaongezeka sijui ndo viwanda tulivyoambiwaa?
 
Mafanikio kiukweli ninazidi kufurahia makampuni ya bet yanaongezeka na punde kila Mtanzania ataweza kubet, tunaomba elimu stahiki itolewe mashuleni kwenye hii michezo ya betting ili iwe sehemu ya ajira ya nchini.

Changamoto: ni Umeme kwa sisi tunaobet uwepo umeme wa uhakika tusitoke online maana wengine tunacheza sana Inplay.
Naunga mkonyo
 
Mafanikio ni mengi haswa upande wa viwanda,tumejenga viwanda vipya vya majungu,visasi,maiti kwenye viroba,uwongo uwongo mwingi kuzindua viwanda mwanza ambayo vilishafanya kazi toka enzi ya jk.
Tumepiga hatua 100 mbele
 
  • Thanks
Reactions: Lee
Mafanikio: amenunua mapanga shaa kwa fedha taslimu na ile panga shaa ya julai imeshaingia nchini, na inapiga kazi ya kubeba watalii kutoka Dar mpk Marekani. Pia Mahakama ya mafisadi inafanya kazi yake kwa kasi ya ajabu. Changamoto kubwa ni kwamba ukivaa nguo ya rangi ya kijani ufisadi hauonekani kabisa, ila ukifanya maamuzi ya kuvaa gwanda la makamanda unakuwa fisadi .
 
Changamoto ni kununua bombadia kwa keshi huku tunadaiwa. Naamini waliotuuzia wangelikuwa hawajalipwa pesa yote wasingelikubali mtu kuizuia kabla hajakabidhiwa mnunuzi!
 
mafanikio:
Mkuu wetu amefanikiwa kuziba mirija ya pesa haramu na biashara haramu kwa kiwango kikubwa.
Amefanikiwa kuwafikia wakwepa kodi wengi na sasa kuna idadi kubwa ya walipa kodi, ingawa changamoto wale walioshtushwa bila kuwa wamejiandaa mshtuko huu unawatoa kwenye game.
Amefanikiwa kutengeneza nidhamu ya matumizi ya fedha kwa wananchi, money psychology ya watanzania wengi imebadilika.

changamoto.
Baada ya kuondolewa pesa,biashara na vipato haramu hilo gap halijaonekana kujazwa na ongezeko la pesa, biashara na shughuli halali. Swali linalobaki hiyo hali itafikiwa lini? wataalam wa forecast za kiuchumi sijajua wanasemaje maana yule wq mwisho kumsikia alisema hali hiyo itaisha ndani ya miaka miwili.

nampongeza kwa mengi mazuri, lkn anachangamoto ya kutatua chabgamoto zilizoibuka ktkt ya utawala huu.
 
Habari ndugu zangu wa jf. Hii ilikua ni maada iliyorushwa jana na ITV kupitia kipindi cha malumbano ya hoja. Kwa aina ya watu waliokuwa wanachangia na namna wanavojenga hoja napata shida kuwaelewa watz. Okey niachane na hao. Najua hapa jf kuna wasomi na watu mahili wa kujenga hoja na kudadavua mambo. Hebu nasi tulumbane kwa hoja katika hiyo maada inayosema:
'MIAKA MIWILI YA SERIKALI YA AWAMU YA TANO, NINI MAFANIKIO NA CHANGAMOTO?'. Nawasilisha
Yap, ni kweli Watanzania tuna matatizo makubwa sana ukiacha ya mitizamo, itikadi na kasumba ni shida tupu.......
 
Big up kwa serikali ya awamu ya tano kwa mambo yafuatayo: Kuanza kwa ujenzi wa treni ya mwendo kasi, Ujenzi wa miundombinu muhimu kama daraja la mto Kilombero, vivuko katika ziwa victoria na overpass pale TAZARA na Ubungo, udhibiti wa matumizi ya fedha za umma, na kurejesha nidhamu ya kazi kwa watumishi wa umma.
Tunaweza kufanya vizuri zaidi katika huduma za afya, maji na elimu sekta ambazo kwa maoni yangu bado zinasuasua.
Tumerudi nyuma zaidi katika masuala ya demokrasia na utawala bora. Moja ya sababu zilizopelekea hali hii ni sarcastic thinking kwamba ili tupate maendeleo ya haraka hatuhitaji kuwa na demokrasia au utawala bora. Eneo hili tusipokuwa makini litavuruga hata mafanikio yaliyopatikana katika baadhi ya maeneo niliyoyataja hapo juu. Ushauri wangu: 1) Serikali iweke vipaumbele katika maeneo yanayogusa maisha ya watanzania wengi: Umeme, maji, miundombinu, elimu, afya, kilimo n.k. Tukipata mafanikio ya 70% katika maeneo haya, Tanzania itakuwa imepiga hatua kubwa kimaendeleo, hata kama haitakuwa nchi ya viwanda. 2) Serikali yetu iendelee kujikita kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na iachane na notion ya "Serikali ya Chama Cha Mapinduzi". Serikali ikishashinda uchaguzi na kuongoza dola, inakuwa serikali ya wote na si ya chama fulani. Kila mtu akielewa msingi wa jambo hili, nchi yetu itatulia sana, na serikali itaungwa mkono na watanzania wote.
 
Nimefahamu kwamba kutawala nchi huna haja ya miongozo ya katiba, wewe ni top, pia vyama pinzani ni vya kufutiliwa mbali, na ukabila ukanda ni muhimu kupewa kipaumbele.... nk
 
changamoto. pesa imekuwa ngumu kiasi fulani hivi.
mafanikio.kutokana na pesa kuwa ngumu imefanya dada zetu kuwa warahisi tofauti na awali.. nafikiri hii inaendana na ile logic ya sunset na sunrise:D
 
Mafanikio makubwa ni kukamata wapinzani na changamoto ni kushindwa kuelewa wapi tunatikiwa kwenda(direction) mpaka sasa.
 
Back
Top Bottom