Maabara ya Jinai yapunguziwa ruzuku ya Tsh. Billion 1.3 hadi Million 100,500,000/= hii ndio BRN?

kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,727
2,000
Ndugu wanaJF
Kupitia Taarifa ya Habari ITV nimeweza kuona na kusikia Mkemia Mkuu wa Serikali akilalamika juu ya Taasisi hii kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi na kushindwa kupima baadhi ya vipimo na kufanya baadhi ya kesi kutosikilizwa kwa wakati na imefahamika kuwa maabara inapokea vipomo zaidi ya 30,000 pia kwa zaidi maabara hii inajihusisha na uchunguzi wa madawa ya Kulevya, vipimo vya DNA pia uchunguzi wa jinsia pale mtoto anapozaliwa akiwa na jinsi mbili pia na vipimo vingine mbalimbali vinavyohusika na jinai.

- Kilichonishangaza ni kuwa hapo awali walikuwa wanapatiwa ruzuku ya Tsh. Billion 1.3 lakini wamepunguziwa hadi Tsh. Million 100,500,000/= na inatakiwa tujue serikali imetangaza utekelezaji wa BRN (Big Result Now) sasa kwa kufanya hivi tutafika tunakotaka kufika yaani unaipunguzia taasisi kutoka Million 1000 na 300 hadi Million 100.
 

mwinukai

JF-Expert Member
May 3, 2011
1,448
1,225
Madhara yake ni makubwa sana kuliko tunavyofikiri 1) ufanisi utapungua sana na utaleta msongamano wa mahabusu kwa vile kesi nyingi upelelezi wake itabidi uchukue mda mrefu sana, zikisubiri vipimo toka kwa mkemia miongoni mwa kesi hizo ni za madawa ya kulevya, mauaji na nk, 2) inarudisha nyuma mapambano ya madawa ya kulevya kwani huwezi ukapambana na dawa haramu za kulevya kama hutaiwezesha kwa mali na raslimali ofisi ya mkemia mkuu wa serikali, kwani madawa ya kulevya ni lazima yafanyiwe kazi na mkemii mkuu na atoe ripoti zake 3) Baadhi ya kesi nii ya kesi za mauaji kwa kutumia sumu na n.k sasa msongamano wa mahabusu unaosubiri taarifa taarifa za mkemia kwa kifupi umekuwa ukiicost serikali katika kuwalisha na kuwahudumia mahabusu wakati hilo lingeweza kuepukwa kwa kuboresha ofisi ya mkemia mkuu wa serikali
 

commited

JF-Expert Member
Feb 27, 2012
1,615
1,195
Mkemia mkuu wa serikal anahitaji 1.3 bilioni tu kwa mwaka kama ruzuku ya kufanyia shughuli zake , wakati ruge kamuwekea nshomile mwenzake 1.6 bilioni, hapo ndipo utaona madhara ya ufisadi, sasa hivi magereza zimesheheni mahabusu lukuki, ambao wanasubiri majibu ya mkemia mkuu, so unaweza kuta mtu akakaa hata miaka 10 gerezani, bila kuhukumiwa maana ushahidi haujapatikana.. Watu tuelewe huu ufisadi ni hatari kwa usalama wa nchi, tuache itikadi za kivyama kwani kuna ndugu zetu wako rumande ambao si wanachama/wala washabiki wa chama cha siasa, ila wanapata mateso kwa kukosekana kwa usawa katika usimamizi wa rasilimali zetu;
 

FaizaFoxy

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
71,300
2,000
Ndugu wanaJF
Kupitia Taarifa ya Habari ITV nimeweza kuona na kusikia Mkemia Mkuu wa Serikali akilalamika juu ya Taasisi hii kushindwa kufanya kazi yake kwa ufanisi na kushindwa kupima baadhi ya vipimo na kufanya baadhi ya kesi kutosikilizwa kwa wakati na imefahamika kuwa maabara inapokea vipomo zaidi ya 30,000 pia kwa zaidi maabara hii inajihusisha na uchunguzi wa madawa ya Kulevya, vipimo vya DNA pia uchunguzi wa jinsia pale mtoto anapozaliwa akiwa na jinsi mbili pia na vipimo vingine mbalimbali vinavyohusika na jinai.
U
- Kilichonishangaza ni kuwa hapo awali walikuwa wanapatiwa luzuku ya Tsh. Billion 1.3 lakini wamepunguziwa hadi Tsh. Million 100,500,000/= na inatakiwa tujue serikali imetangaza utekelezaji wa BRN (Big Result Now) sasa kwa kufanya hivi tutafika tunakotaka kufika yaani unaipunguzia taasisi kutoka Million 1000 na 300 hadi Million 100.
= ruzuku
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom