Ma-RC&DC; kamateni Madiwani na maafisa manispaa wanaochonga barabara za mitaa kihuni huni

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,279
21,396
habari za weeked:
Pasipo kupoteza mda, Nasikitishwa na utaratibu wa kihuni unaofanywa na baadhi ya madiwani kwa kushilikiana na manispaa kuchonga barabara za mitaa nchi kwetu,
SABABU ZA KUWAKAMATA
  1. UTARATIBU WA KUCHONGA NI MBOVU
Barabara za mitaa hazichongwi kwa utaratibu unaotakiwa, Barabara ambazo zinakuwa katika hali ya kutumika vizuri zinatifulia na kuharibiwa na hayo magreda ya manispaa ambapo ni kinyume na utaratibu wa ujenzi;
hawazingatii utaratibu wa ujenzi unaowataka kumwaga maji punde tu baada ya kuchonga barabara hizi, hii ni kutokana na kupunguza vumbi pamoja na kushindiria ili barabara iweze kutumika na wote ipasavyo,
Kinyume na utaratibu huo, Madiwani wamegeuza barabara hizi kuwa ni miradi ya kujinufaisha na hakuna anaefuatilia,Hakuna mtaalam anaesimamia kazi zaidi ya Dreva wa GREDA anaechonga kwa kufuata maelekezo ya diwani pekee,GREDA linatifua hovyo na kufanya barabara inakuwa kero kutumika hata kwa watembea kwa miguu,baiskeli na magari pamoja na kusababisha vumbi kwa wakaaji wa maeneo ya barabara hizo jambo linalo sababisha magonjwa n.k

2. MIRADI HII INAUPIGAJI NA UFISADI
GREDA za manispaa zinafanya kazi ndogo sana ukilinganisha na LITA za mafuta zinayoandikiwa/jaziwa,
mathalani kazi ya lita 200lt, ma GREDA hayo huaandikiwa LITA 800lt na zaidi. Hii inasababishwa na uzembe wa usimamizi wa utekelezaji wa miradi hi inayofanyika kihunii.
3. HAWACHONGI NA KUJAZA VIFUSI
yapo maeneo korofi ambayo huhitaji angalau yawekewe vifusi japo kidogo ndipo barabara ichongwe, lakini wao huchonga kwa kukariri tuu pasipo utaalam kutumika, ambapo badala ya kutengeneza hujikuta wanaharibu kabisa. Mfano; unapochonga sehemu yenye mchanga/vumbi pasipo kuweka vifusi/maji barabara huharibika haraka na hugeuka kero kwa watumiaji

NAWAOMBA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA, KAMATENI NA MTIE NDANI HAWA MADIWANI NA MAAFISA MANISPAA WANAOTUMIA MAGREDA HAYA KUJINUFAISHA.
 
Nakupongeza mleta uzi kwa kulisemea hili la madiwani na wenyeviti wa mitaa kujinufaisha kutokana na uchongaji wa barabara. Sio tu wanafanya ubadhilifu kwa kuiba mafuta ya GREDA bali wenyeviti wa mitaa hasa MBEZI BEACH sehemu za TANK BOVU mwenyekiti anatuchangisha fedha za kununulia mafuta ili hali greda huwa limetengewa hela za mafuta na manispaa!! Huyu mwenyekiti aitwae PANTALEO ndio anaeendeleza ufidadi huu zaidi ya kuuza viwanja vya watu!! Kuna umuhimu DC wa Kinondoni kukomesha wizi huu.
 
Hao wote uliowataja hapo lao ni moja, njia sahihi ingekuwa uwepo ukurasa wa wazi wa kutolea taarifa juu ya utekelezaji wa miradi husika, wananchi wapewe uhuru wa kutoa taarifa kwa serikali pale wanapoona hayo yanatendeka.

Viongozi waliotajwa huwa wanazimwa kinamna na wahusika, 2018 barabara nyingi zimechongwa bila kumwagiwa maji wala kushindiliwa, ili kuthibitisha hili ingeundwa tume ya kupita kwenye maeneo husika na kuwahoji wananchi hadharani kama hayo yalifanyika
 
AISEE HAYA NDIYO MADUDU NAYOSEMA
 
kabisa mkuu
 
Jamaa alitaka kukuingiza chaka

Tunapojadili mambo ya maendeleo yetu sio busara kuingiza ushabiki wa vyama; barabara zinapohalibika wanaoathirika ni wananchi wote irrespective of their party affiliation!
 
kuna watu huwa siwaelewi kabisa kichwani mwao vyama mbele
 
Muwe mnahudhuria mikutano ya wananchi kwenye mitaa. Huko ndiyo kwenye platform ya kutolea malalamiko kama haya, lakini wengi wenu huwa hamuhudhurii mikutano hii
 
kuna watu huwa siwaelewi kabisa kichwani mwao vyama mbele

Hata hao viongozi mkuu, wapo wanaoshindwa kutofautisha uhitaji wa huduma za jamii na itikadi. Na wengine wanadiriki hata kujikomoa wao na familia zao ati tu kwasababu yakipelekwa maendeleo walipo aina fulani ya wapigakura haitawafurahisha wao pamoja na kuwa wanaishi humohumo
 
turudi kwenye hoja sasa
 
turudi kwenye hoja sasa

Itafutwe namna shirikishi na rahisi ya kuwafanya wananchi kuwafikishia viongozi wa ngazi za juu malalamiko yao, kwamfano; ziwepo kurasa za mtandao (web pages) kwa kila mkoa, ndani yake kuwepo wilaya zake zote na katika kila wilaya kuwe na tarafa na kata zake, wananchi wa maeneo husika waandike malalamiko yao huko, Ikulu ione, iwaagize wakuu wa maeneo husika kufuatilia malalamiko husika na kuyatolea taarifa. Kinachotuangusha kwa sasa ni gap kubwa kati ya mwananchi wa chini na uongozi wa juu wa nchi, wabunge na madiwani hawafiki kila sehemu za wapiga kura wao, matokeo yake uongozi wa juu unachukulia kuwa mambo yote yapo sawa kumbe ni kinyume chake
 
mi nazani hizo gharama wakabiziwe tarula , tarula wanawataalam wakuweza kufanya kwa usahihi zaidi
 
Nakupongeza mleta uzi kwa kulisemea hili la madiwani na wenyeviti wa mitaa kujinufaisha kutokana na uchongaji wa barabara. Sio tu wanafanya ubadhilifu kwa kuiba mafuta ya GREDA bali wenyeviti wa mitaa hasa MBEZI BEACH sehemu za TANK BOVU mwenyekiti anatuchangisha fedha za kununulia mafuta ili hali greda huwa limetengewa hela za mafuta na manispaa!! Huyu mwenyekiti aitwae PANTALEO ndio anaeendeleza ufidadi huu zaidi ya kuuza viwanja vya watu!! Kuna umuhimu DC wa Kinondoni kukomesha wizi huu.
hizo kazi wakasimishe kwa TARULA
 
habari za weeked:
Pasipo kupoteza mda, Nasikitishwa na utaratibu wa kihuni unaofanywa na baadhi ya madiwani kwa kushilikiana na manispaa kuchonga barabara za mitaa nchi kwetu,
SABABU ZA KUWAKAMATA
  1. UTARATIBU WA KUCHONGA NI MBOVU
Barabara za mitaa hazichongwi kwa utaratibu unaotakiwa, Barabara ambazo zinakuwa katika hali ya kutumika vizuri zinatifulia na kuharibiwa na hayo magreda ya manispaa ambapo ni kinyume na utaratibu wa ujenzi;
hawazingatii utaratibu wa ujenzi unaowataka kumwaga maji punde tu baada ya kuchonga barabara hizi, hii ni kutokana na kupunguza vumbi pamoja na kushindiria ili barabara iweze kutumika na wote ipasavyo,
Kinyume na utaratibu huo, Madiwani wamegeuza barabara hizi kuwa ni miradi ya kujinufaisha na hakuna anaefuatilia,Hakuna mtaalam anaesimamia kazi zaidi ya Dreva wa GREDA anaechonga kwa kufuata maelekezo ya diwani pekee,GREDA linatifua hovyo na kufanya barabara inakuwa kero kutumika hata kwa watembea kwa miguu,baiskeli na magari pamoja na kusababisha vumbi kwa wakaaji wa maeneo ya barabara hizo jambo linalo sababisha magonjwa n.k

2. MIRADI HII INAUPIGAJI NA UFISADI
GREDA za manispaa zinafanya kazi ndogo sana ukilinganisha na LITA za mafuta zinayoandikiwa/jaziwa,
mathalani kazi ya lita 200lt, ma GREDA hayo huaandikiwa LITA 800lt na zaidi. Hii inasababishwa na uzembe wa usimamizi wa utekelezaji wa miradi hi inayofanyika kihunii.
3. HAWACHONGI NA KUJAZA VIFUSI
yapo maeneo korofi ambayo huhitaji angalau yawekewe vifusi japo kidogo ndipo barabara ichongwe, lakini wao huchonga kwa kukariri tuu pasipo utaalam kutumika, ambapo badala ya kutengeneza hujikuta wanaharibu kabisa. Mfano; unapochonga sehemu yenye mchanga/vumbi pasipo kuweka vifusi/maji barabara huharibika haraka na hugeuka kero kwa watumiaji

NAWAOMBA WAKUU WA WILAYA NA MIKOA, KAMATENI NA MTIE NDANI HAWA MADIWANI NA MAAFISA MANISPAA WANAOTUMIA MAGREDA HAYA KUJINUFAISHA.

Waanze na waliojenga Barabara ya Sanawari ya juu, ni usanii mtupu.

Nashauri waziri au naibu waziri afanye ziara ya ghafla kwa kuwa kama ni lami sio ya aina hii.

Huu ni zaidi ya usanii.

Mvua ikinyesha kesho au keshokutwa itakuwa mbaya kuliko ilivyokuwa awali.

Naomba sana wahusika wakamatwe mara moja.
 
aisee
 
Back
Top Bottom