Ma-First Lady wa Afrika na dhana ya ukoloni mamboleo.... a.k.a. Utandawizi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ma-First Lady wa Afrika na dhana ya ukoloni mamboleo.... a.k.a. Utandawizi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MwanaHaki, Jul 9, 2010.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Jul 9, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Alipokuwapo Mama Maria Nyerere enzi zake Ikulu, kazi yake ilikuwa ni moja tu. Kulea watoto na kumsaidia mumewe. Basi.

  Akafuata Mama Sitti Mwinyi, naye alifanya hivyo hivyo.

  Tatizo lilianza pale walipokuja hawa "wasomi", akianzia Anna Mkapa. Ikaanzishwa dhana ya First Lady. Ikabuniwa EOTF. Kazi kwa kwenda mbele... kila 'misaada' ya wafadhili ilipokuja ilipitia EOTF, ukiritimba fulani ukajengeka pale....

  Kwa Mwalimu Salma Kikwete (Ualimu si kazi ya kustaafu...), mambo ni yale yale na WAMA.

  Sasa tujiulize...

  Hii dhana ya First Lady inamsaidia nani haswa? Kwa nini tuwe na "Mama wa Kwanza", kama wataalam wa Kiswahili walivyodadavua....

  Kisha, tujiulize zaidi...

  Hizo NGO za hawa ma-First Lady (tukianzia Tanzania) zinawasaidia nani haswa, ikizingatiwa kwamba wanapoondoka Ikulu wanaondoka nazo, na wakiwa Ikulu wanatumia rasilmali za Taifa... majengo ya ofisi, magari ya Ikulu, pesa za walipakodi, n.k.

  Ma-First Lady wa Afrika wana taasisi yao, inaitwa OAFLA - Organisation of African First Ladies (Home | Organization of African First Ladies against HIV/AIDS).

  Huu utandawazi wa kuiga kila kitu cha MZUNGU unatupeleka pabaya. Iko siku wananchi - wenye nchi - watadai haki zao... iko siku!

  ./Mwana wa Haki
   
 2. N

  Nyauba JF-Expert Member

  #2
  Jul 9, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 1,098
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  kwa bongo first lady mama mkapa alikuwa mbunifu zaidi na ameset trend wote wanaofuata wanaiga..muda si mrefuu tutaona madhara ya kuiga bila kuwa na passion na uwezo nachoo..

  EOTF mpaka sasa imefanya kazi nzuri kuwanyanyua akina mama wajasiriamali nchini..
   
 3. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #3
  Jul 9, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  kwa mujibu wa protokoli za diplomasia ( na maybe usalama wa taifa), first lady anatakiwa kupatiwa ulinzi masaa 24 na hivyo kuweka ugumu kwa hawa ma first lady kuendelea na shughuli walizokuwa nazo kabla ya kuukwaa u first lady.

  mama hawa ambao wamekuwa wakifanya kazi day in day out ( na pengine kuwa na kipato kuliko cha waume zao na kuendesha familia wakati mwengine) hawangependa kukaa tu nyumbani kwa kuwa MUMEWE amepata cheo.

  ndio nafikiri wanajikuta wakianzisha hizi NGO angalau ziwashughulishe kidogo
   
 4. doup

  doup JF-Expert Member

  #4
  Jul 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  Labda wanaziitaji hizo NGO kuondoa stress; si unajua hadi kufuli a.k.a chupi za waume zao zinafuliwa na usalama wa taifa.
  atafanya nini sasa!!?.

  Na walio wengi mawazo hayo ya kuanzisha NGO huwa si yao; kuna wajanja ujipendekeza na kuwatumia.
   
 5. Obuntu

  Obuntu JF-Expert Member

  #5
  Jul 9, 2010
  Joined: Feb 6, 2008
  Messages: 512
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Mkuu,

  hivi kuna uhusiano kati ya neno "dope" na "doup"?
   
 6. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #6
  Jul 9, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mwanahaki,
  Umesahau Mama Sitti ndiye aliyekuwa mjasiriamali wa kwanza Ikulu. Huyu ndiye aliyetuuzia bia za Stella Artois na majenereta ya umeme.
  Nilitaka tu kuliweka hilo sawa.
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Jul 9, 2010
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu wangu Mama Mkapa hakuset trend yoyote kaikuta EOTF na kaweza kuitumia kwa manufaa yake zaidi.She is a business woman haya maswala ya First Lady yameangukia mguuni kwake akiwa pekee na goli wazi hakuna hata goolkeeper.. akatufunga kwa kisigino.
   
 8. doup

  doup JF-Expert Member

  #8
  Jul 9, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  dope => ?
   
 9. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #9
  Jul 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180

  Alikwenda mbali zaidi kwani kulikuwa na tetesi kuwa ana plots 1000 hapa Dar!:pray:
   
 10. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #10
  Jul 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,809
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  I love JF!:lock1:
   
 11. Maria Roza

  Maria Roza JF-Expert Member

  #11
  Jul 9, 2010
  Joined: Apr 1, 2009
  Messages: 6,773
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  hivi mbona wake au waume wa mabalozi hawataki kufanya kazi maana wanawakilisha nchi sasa hawa kwann wanafanya kazi lakini???
   
Loading...