Ma Conciliori wa Ma Don wa kimafia nchini kuingia kazini

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,033
2,000
Wanasheria wanaotumiwa na mafisadi nchini kina ken fungamguu na wengine hivi sasa wanajiweka sawa kuvuna kutoka wawekezaji wa acacia na iptl. Kikwazo kikubwa kwao ni kutumbuliwa kwa kiasi kikubwa wala rushwa serikali. Rushwa ndio silaha kubwa kufanikisha dhuluma ya uporaji rasilimali za taifa. Kwa hivi sasa fisadi na wawekezaji dhalimu wanahangaika kuwanunua wanasheria mahiri na viongozi wa upinzani na wengine watakaoweza kujiuza kwao ili kuepuka hasara kubwa watakayopata kwa kutakiwa kulipa kile cha watanzania walichokula kwa njia ya udanganyifu. Itakua jambo muhimu ili kuliokoa taifa kwa viongozi wakuu kisiasa wote na wanasheria mahiri wote kuonyesha uzalendo kwa kushikamana. Miaka 60 hivi iliyopita Patrice Lumumba aliyekua waziri mkuu wa kwanza na kiongozi wa serikali ya DR Congo aliondolewa na kuuliwa mara moja kwa kuonyesha tu nia ya nchi yake kudhibiti madini yake. Baada ya muda wote huu nchi zetu lazima sasa zionyesha ukomavu kupigana na kushinda vita ya kiuchumi. Siri kubwa ni umoja.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom