Ma Auditor wamebaini Ufisadi wa Kutisha CCBRT, Wafanyakazi wawili wamefutwa kazi!!!

Mwamakula

JF-Expert Member
Nov 7, 2010
1,890
382
Wakaguzi wa hesabu wamebaini Ufisadi Mkubwa Hospitali ya Macho CCBRT ambapo imebainika kwamba mishahara ya wafanyakazi kutoka Hazina ,haijawahi kulipwa!!

Pia Watendaji wakuu CCBRT walifanya njama na Wahasibu na Kutengeneza majina hewa na kuyapeleka hazina , ambapo serikali ilikuwa inalipa wakati watu hao hawapo duniani.

Wizi huo umeonyesha kukithiri muda mufupi baada ya serikali kuanza kushirikiana na CCBRT ambapo kuna fungu la mishahara kutoka Hazina lilitengwa kuboresha Mishahara ya wafanyakazi!!

Wafanyakazi wawili wanaofahamika kwa Majina ya Bi Leonida na Bw Mohamedi wamefukuzwa kwa saa 24 kutokana na kashifa hiyo.

Mishahara ya wafanyakazi mwezi wa tatu imesimamishwa kupisha uchunguzi wa dharura!!
 
Hali mbaya, sasa mishahara ya wafanyakazi kusimamishwa hapo inakuwaje?
 
Ingekuwa inafanyika kila pahala, na kwa kila idara, wizara, halmashauri basi nchi hii ingekuwa mbali kabisa...
 
Halafu ni taasisi ya kidini hii jamani sasa zile za kiraia hali itakuwaje?Serikali naiomba uchukuwe hatua kali ikiwemo kurudishiwa fedha zake zote zilizofujwa kwa kipindi chote hicho!!
 
Sasa jiulize tangu MoU ya kanisa na Serikali mwaka 1992 hilo CCBRT ndio nimesikia leo wakifanyiwa auditing???

a. huu utaratibu ni uwizi na ni hatari kwa taifa..mashirka ya kanisa yameshaibia taifa hili kwa muda mrefu ni wakati wa kusema ukweli.
 
Acha kuendekeza Udini Wezi hawana dini ni wezi tu!!!!!!
 
kwani waliofukuzwa ni wahasibu?mbona hauweleweki.Kama mishahara hewa,si hazin a wangetoa kwenye vyombo vya habari??hata kama njiani inakuja,mbona sasa habari haieleweki??hebu tufafanulie tupate news! kingine,hao waliofukuzwa wamefukuzwa na nani??na CCBRT au wakaguzi au hazia,tudadavulie kidogo muhimu sana hii
Wakaguzi wa hesabu wamebaini Ufisadi Mkubwa Hospitali ya Macho CCBRT ambapo imebainika kwamba mishahara ya wafanyakazi kutoka Hazina ,haijawahi kulipwa!!

Pia Watendaji wakuu CCBRT walifanya njama na Wahasibu na Kutengeneza majina hewa na kuyapeleka hazina , ambapo serikali ilikuwa inalipa wakati watu hao hawapo duniani.

Wizi huo umeonyesha kukithiri muda mufupi baada ya serikali kuanza kushirikiana na CCBRT ambapo kuna fungu la mishahara kutoka Hazina lilitengwa kuboresha Mishahara ya wafanyakazi!!

Wafanyakazi wawili wanaofahamika kwa Majina ya Bi Leonida na Bw Mohamedi wamefukuzwa kwa saa 24 kutokana na kashifa hiyo.

Mishahara ya wafanyakazi mwezi wa tatu imesimamishwa kupisha uchunguzi wa dharura!!
 
hii habari mbona inasikitisha,lakini mtoa habari haueleweki,kama wanalipa hewa,sasa mbona wafanyakazi hawagomi?na hao waliofukuzwa ndio walioiba au??menejiment si ingetakiwa imsimamishe Mhsibu mkuu hapo??au ndio hao??haijakaa vizuri hii habari,fafanua
 
Waanze na wizara ya elimu kama awajamtukuna waziri na naibu wake
marehemu wameshanuka bado wanakula mshahara mbaya wanaingizwa kwenye per diem za safari sijui wanaruka na ungo ama lah...hii ni matokeo kikwete alioleta na akuna wa kumlaumu ameacha watu wanaiba benki kuu na kuwaambia bila aibu warudishe mpaka siku kadhaa unahisi hata wewe utaacha kuiba ulipo
 
halafu ni taasisi ya kidini hii jamani sasa zile za kiraia hali itakuwaje?serikali naiomba uchukuwe hatua kali ikiwemo kurudishiwa fedha zake zote zilizofujwa kwa kipindi chote hicho!!
acha kufikiria kwa masaburi wewe.mwiz ni mwizi tu.iwe makanisan au misikitin,ndo maana watu wakimaliza ibada wanafunga milango,wangekuwa wana acha wazi kama hakuna wezi
 
acha kufikiria kwa masaburi wewe.mwiz ni mwizi tu.iwe makanisan au misikitin,ndo maana watu wakimaliza ibada wanafunga milango,wangekuwa wana acha wazi kama hakuna wezi

Wanajamii Forum kwanza nawapongeza kwa kujadili mambo ya ufisadi kwani hatuyahitaji katika sehemu yoyote. Ni kweli watu wawili wamesimamishwa kazi na si kufukuzwa kama ilivyoandikwa na wanajamii forum wenzangu. Pia si sahihi kuwa mishahara imechelewa kwa sababu ya auditing, lahasha, ni kwa sababu anayeandaa mishahara alikumbwa na kazi nyingi za muhimu pia kama za mishahara ambazo si lazima ziandikwe hapa, mishahara ilitolewa tar 28.3 ni kama siku mbili zaidi ya tar iliyozoweleka na wafanyakazi wa CCBRT. Ata hivyo hakuna makubaliano yoyote kati ya mwajili na wafanyakazi kuwa mishahara itoke tar 26 au 28! Haya ni mazoea tu katika maisha kazini.Tuhuma ni muhimu kuzifanyia kazi wakati wahusika wako nje ya eneo la kazi ili kuleta ufanisi zaidi katika upelelezi. Tuendelee kupata habari sahihi zaidi hapo baadaye na si majungu kwa organization kubwa na muhimu kama CCBRT.
 
Halafu ni taasisi ya kidini hii jamani sasa zile za kiraia hali itakuwaje?Serikali naiomba uchukuwe hatua kali ikiwemo kurudishiwa fedha zake zote zilizofujwa kwa kipindi chote hicho!!

CCBRT siyo taasisi ya Kidini ni secular NGO.
 
uchunguzi huu pia upitishwe katika taasisi za serikali ndipo mtachoka wenyewe!!
nchi hii ina kazi kwelikweli
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom