Kite Munganga
Platinum Member
- Nov 19, 2006
- 1,773
- 950
Jana nimeona M7 akishuka kwenye ndege ya rais wa TZ?? na akapokewa na Kibaki kwa furaha sana,hii ilinifanya kutafakari hapo nyuma M7 alipokuwa kiongozi wa kwanza kumtambua Kibaki bila woga wowote kama JK alivyofanya, pia ikanikumbusha kuwa huyu bwana ana sekeseke lake na bwana Kony na naweza sema ni la kudumu, bado nikakumbuka hapo nyuma alivyoweza badili Katiba ya kwao kwa manufaa yake. Haiingiii akilini kuwa huyu anafaa kuwa miongoni mwa wapatanishi kwani KATIBA kwake ni tatizo na katiba ya Kenya ni tatizo, Vivyo hivyo kwa BMW yeye tatizo la Zanzibar lilimshinda leo kapata wapi ufundi wa kutatua tatizo la katiba ya jirani yake wakati kwake muafaka mpaka leo ni ndoto, bado watu tunakumbuka yale mauaji ya Zenj yasiyo na majibu mpaka leo achilia mbali kufungua kiosk white house, mie naona hao wamepeleka usanii wa kisiasa tu. Wana JF natoa hoja,