M4c ni noma!

Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,326
5,264
Nimeshuhudia kupita itv news ya saa 2 wananchi wakimzomea makongoro mahanga na kuimba mafisadi ,nikajiuliza hakuna tena wafuasi wa ccm hata wa kukodi kwani hata tanga jk alipokelewa. na cuf
 
Nimeiona hii na mtangazaji aliiacha iende hewani bila kinyongo. Wengine wakiimba mwizi...mwiziiii.....
 
Jamani ili ni funzo kwetu tusikubali kuhujumiwa katika uchaguzi tuzilinde kura zetu kila tunapofanya uchguz, kwani hii idara ya mahakama imejaa maswayiba pia makada wa ccm hatutafika, hatutapata haki pale
wahenga walisema ukiona kiza kimezidi ujue kunaelekea kukucha, 4sure ukombozi unakuja 4sure m4c will put us high
peoplees powerrrrrr
 
Hii inasikitisha kwa wanaotegemewa kutoa haki ndiyo wapindisha haki wakubwa kwa visingizio vya sheria...wakati unakuja mafisadi mpaka wa sheria watakosa pa kuficha sura zao...nakwambia si mbali. Mpendazoe kashindiwa mahakamani lakini wananchi wanamjua mbunge wao. Jipe moyo Mpendazoe wakati wa haki kusimama umekaribia sana.
 
kama refari ni wewe,mshika kibendera ni wewe,mshangiliaji ni wewe na mchezaji ni wewe unategemea nini.Ili play ground iwe fair lazima tuwe na katiba iliyowekwa na wananchi bila matakwa ya serikali husika ndo maana M4C lazima tuisupport ili kuleta mabadiliko ya kweli
 
Makongoro kwa hali ilivyo ni mbunge wa CCM na familia yake kwani ukiona watu wanamzomea ujue sio chaguo lao mfano ungine ni Kafumu wa Igunga kwani nae kila akikanyaga Igunga Kizomeo kwa kwanda mbele.
 
Namuonea huruma sana Makongoro heri aachane na siasa!!aibu sana amebebwa live bila chenga!!wakate rufaa angalau itacheleweshwa ila angalau kuliko kuhalalisha mwizi
 
Baada ya hukumu ya Jana iliyo waacha wananchi wengi kwenye majonzi ilishangaza pale wananchi walivyoanza kumzomea aliyetangazwa kuwa ni mshindi ndugu Mahanga fisadi! Fisadi! Mwizi! Mwizi Huku akiwa anakimbilia kwenye gari akatokomea kwa mwendo wa ajabu. Mimi nilikuwa nafikiri madikteta wanakuwa Marais tu Kumbe hata wabunge? Sijui huko bungeni anawakilisha watu gani
 
Hii inasikitisha kwa wanaotegemewa kutoa haki ndiyo wapindisha haki wakubwa kwa visingizio vya sheria...wakati unakuja mafisadi mpaka wa sheria watakosa pa kuficha sura zao...nakwambia si mbali. Mpendazoe kashindiwa mahakamani lakini wananchi wanamjua mbunge wao. Jipe moyo Mpendazoe wakati wa haki kusimama umekaribia sana.

Lema ana msemo huu[sikiliza! Wao wana pesa sisi tuna Mungu,msihofu,tutatumia mahakama ya Mungu,piga kura,linda kura na ngojea ushindi].TUSIHOFU NGUVU YA PESA BALI KATIKA KWELI YA MUNGU.
 
Baadhi ya majaji ni makada wa CCM na wanaendeshwa na CCM au wanaganga njaa tu hao! Bila kupindisha sheria na kutoa hukumu uchwara kale kaghorofa anakojenga pale mikocheni, regent estate Mgombani street kasingemalizika! Kujenga nyumba mikocheni na kama ana mpango kuishi mikocheni basi huko ni kuhama Segerea.
 
Baada ya hukumu ya Jana iliyo waacha wananchi wengi kwenye majonzi ilishangaza pale wananchi walivyoanza kumzomea aliyetangazwa kuwa ni mshindi ndugu Mahanga fisadi! Fisadi! Mwizi! Mwizi Huku akiwa anakimbilia kwenye gari akatokomea kwa mwendo wa ajabu. Mimi nilikuwa nafikiri madikteta wanakuwa Marais tu Kumbe hata wabunge? Sijui huko bungeni anawakilisha watu gani

Nimesoma hiyo taarifa kwenye gazeti la mwananchi la leo.Ama kweli watanzania wameamka
 
Nimesoma hiyo taarifa kwenye gazeti la mwananchi la leo.Ama kweli watanzania wameamka

WANANCHI WATAAMKA KAMA WATASOMA, WATAJISOMEA, NA KUTAFUTA TAARIFA WENYEWE BILA KUTEGEMEA MAGAZETI YA KISHABIKI.

MIMI NIMEJIFUNZA KITU KIMOJA KUHUSU WATANZANIA. WENGI WETU NI WAVIVU WA KUSOMA NA KUJISOMEA.

Tunapenda majibu rahisi na mepesi kutoka majikwa ya kisiasa.

Sisi WATANZANIA ni wepesi kulaumu wengine na sisi wenyewe hatutaki kutambua mapungufu yetu. Sisi ni wepesi kuwaamini tunaowashabikia na kuwapenda. TUTAJUTA HAPO BAADAYE KWA UVIVU WETU WA KUSOMA, UVIVU WETU WA KUTOJISOMEA, UVIVU WETU WA KUTOJITAFUTIA TAARIFA.

Nina maswali kadhaa kwa wanaojiita GREAT THINKERS WA JAMII FORUMS:

  1. Nani amesoma sheria ya uchaguzi ambayo imeandikwa kwa lugha ya Kiswahili kabla ya kulaumu?
  2. Je wananchi wangapi walisoma HUKUMU kabla ya kulaumu?
  3. Nani amesoma vifungu has cha 108 cha sheria hii kuhusu wajibu wa anayefungua kesi za uchaguzi?
  4. Magezeti gani yaliandika mwenendo wa kesi neon kwa neon badala ya vichwa vya HABARI VYA KISHABIKI?
  5. Je wananchi wangapi walisoma ushahidi wa pande zote mbili zilizotolewa mahakamani?

Bila kuacha uvivu wa kufikiri na UVIVU WA KUSOMA NAKALA HALISI ZA HUKUMU demokrasia haitajengeka hapa Tanzania. Bila kuacha uvivu wa kujisomea na kusoma TUTAJADILI KATIBA KISHABIKI.
 
Back
Top Bottom