M4C Mikoa ya Kusini: Moto wa Chadema wawatisha mawaziri | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

M4C Mikoa ya Kusini: Moto wa Chadema wawatisha mawaziri

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by rosemarie, Jun 8, 2012.

 1. rosemarie

  rosemarie JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 6,767
  Likes Received: 1,023
  Trophy Points: 280
  MKUCHIKA, GHASIA, CHIKAWE NA MEMBE WAENDA KUUZIMA, CCM KUJIPIMA NGUVU JANGWANI KESHO

  Geofrey Nyang'oro, Mchinga | Mwananchi

  VUGUVUGU la Mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chadema katika mikoa ya Lindi na Mtwara, limewatisha mawaziri wanne wanaotoka katika mikoa hiyo, ambao wamelazimika kurejea majimboni mwao kusafisha hali ya hewa.

  Mawaziri waliorejea majimboni kufanya kilichoelezwa ni shughuli za kiserikali ni pamoja Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

  Kwa wiki takribani ya pili sasa, Chadema kimekuwa kikiendesha operesheni hiyo ya vuguvugu la mabadiliko katika mikoa hiyo ya kusini mwa nchi.

  Jana, taarifa zilizopatikana mkoani Lindi zilisema Ghasia alifanya mkutano katika jimbo lake la Mtwara Vijijini akiwa katika harakati za kufuta nyayo za Chadema.
  Oparesheni hiyo ya Chadema jana na leo ilitarajiwa kuingia jimbo la Mtama ambalo linaongozwa na Membe.

  Vuguvugu hilo linaongozwa na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, ambao ni Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambao wanatarajia kuhutubia mikutano yao katika kata aliyozaliwa Membe.

  Mkuchika alithibitisha jana kuwa yuko jimboni kwake Newala, na alipoulizwa kama lengo lake ni kufuta nyayo za Chadema, aling'aka, "Kwani kila siku nikija nyumbani kwangu huwa mnaniuliza, mimi nimekuja nyumbani kwangu bwana. Niacheni nipumzike nyumbani kwangu."

  Membe alipotafutwa kuzungumzia taarifa hiyo simu yake haikuwa hewani, lakini Msemaji wa wizara hiyo, Assah Mwambene alipoulizwa alipo bosi wake alithibitisha kwamba yuko jimboni kwake.

  Jana, vuguvugu hilo lilikuwa katika Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, lakini lilikumbana na upepo mzito wa kisiasa baada ya bendera mpya za CCM kuonekana kupamba kona mbalimbali za jimbo hilo.

  Waziri Ghasia na Chikawe pia hawakupatikana kupitia kwa simu zao kuzungumzia taarifa hizo.

  Msigwa ashambulia mawaziri
  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliwashambulia mawaziri hao wanaotoka majimbo ya mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, akihoji ni kwanini wanaikumbatia CCM.

  Msigwa alisema CCM imeshindwa kuwasaidia kuleta maendeleo katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania, ndiyo sababu, watu wanaishi katika hali ya umasikini wa kutisha.

  "Mimi ninawashangaa wabunge wa majimbo ya Lindi na Mtwara wakiwamo mawaziri Hawa Ghasia, Mkuchika na Bernard Membe ni kwa nini wanakiunga mkono CCM wakati majimbo yao yamekithiri kwa umaskini," alisema Msigwa na kuongeza;

  "Nashangaa Membe, Hawa Ghasia na Mkuchika sijui kiburi wanakipata wapi. Ndiyo sababu wamehama majimbo yao na kuishi Dar es Slaam, haiwezekani leo mikoa wanayotoka, wilaya na hata majimbo yakawa na sura kama ilivyo sasa. Nitakwenda kuwabana bungeni,'' alisema Msigwa.

  Msigwa alitamba kuwa yeye na wabunge wote wa Chadema wanaishi kwenye majimbo yao, ndiyo sababu wamekuwa wakifanikiwa katika mikakati yao ya kutetea na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

  Sugu alia umaskini
  Katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) alisema ukarimu wa wakazi wa Lindi na Mtwara kwa CCM ndio uliosababisha mikoa hiyo kuwa katika lindi la umaskini.
  Mbilinyi alisema wabunge kupitia chama hicho hawana uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na mfumo wa chama hicho kukumbatia matajiri na kuachana na maskini.

  Alisema ndani ya CCM, watu wa kipato cha chini hawawezi kupata ubunge, akitoa mfano kwamba fomu ya ubunge ya CCM inachukuliwa kwa Sh100, 000 ilihali ya Chadema ni Sh50,000.

  "Nawasihi vijana wenzagu kuungana na kuwa na ujasiri wa kuamua katika masuala ya kimaendeleo. Mimi nilikuwa mitaani na muziki wangu, lakini nikatokea Chadema na kunipa nafasi ya kugombea ubunge ,lakini ningekwenda CCM wasingenipa nafasi ya kugombea kwa sababu ya umaskini wangu," alisema Mbilinyi na kuongeza:

  "Hivyo, basi wazee na vijana nawasii kuachana na CCM kwa sababu chama hicho kimekosa mwelekeo tangu alipofariki Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, CCM iliyobaki ni ya wanjanja sio wewe ulioko kijijini."

  CCM kujipima nguvu Jangwani
  Wakati Chadema ikizidi kuwasha moto wa vuguvugu la mabadiliko, Chama tawala CCM kesho kitafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, kutoa msimamo wake kuhusu mambo muhimu yanayogusa taifa.

  Mkutano huo unafanyika ikiwa zimepita takribani wiki mbili tangu Chadema wafanye mkutano mkubwa katika viwanja hivyo uliohudhuriwa na mamia ya watu, na kuzindua kampeni yake ya M4C', yenye lengo la kushika dola mwaka 2015.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana katika mtandao wa chama hicho tawala jana, iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa huo, Juma Simba ilieleza kwamba mkutano huo utaanza saa 8 mchana.

  Simba alisema katika taarifa hiyo kwamba, chama hicho kitatumia mkutano huo kuwaeleza Watanzania msimamo wake kuhusu hatma ya maisha yao.

  "Utaeleza hatma ya maisha ya Watanzania katika suala la ajira, miundombinu ya barabara, reli, bandari na anga, bei za bidhaa mbalimbali, umeme na rasilimali za taifa," alisema Simba.

  Alifafanua kwamba jambo jingine litakaloelezwa katika mkutano huo, ni msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa Katiba Mpya pamoja na vurugu za Zanzibar.

  Katika mkutano huo watakuwapo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali na kutoa ufafanuzi juu ya masuala hayo, yaliyoainishwa kama msimamo wa chama hicho.

 2. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,930
  Likes Received: 1,462
  Trophy Points: 280
  Wameshachelewa gari lina kasi ya ajabu!
   
 3. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  wanaanya, chadema inawalazimisha wafanyekazi na wasipo fanya hivyo hata hiyo kambi ya upinzani itabidi mwaka 2015 washirikiane na matawi yao kama cuf, nccr manunuzi maana hawatatosha.
   
 4. e

  ebrah JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2012
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 397
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Eee Mungu wetu we ujuaye kupima Nafsi za watu hawa , unajua mawazo, mipango na hila zao katika kuficha maovu Yao, kuwapumbaza watanzania na kuzidi kutunyonya, nakuomba usimame ututetee mbele ya Hawa simba waliojipanga kutunyonya na kutuangamiza kwa manufaa Yao na ya watoto Wao! Naomba uharibu lugha zao wasiweze kunia mamoja siku zote na njia zao zote ziwe utelezi wasifanikiwe katika hila zao
   
 5. mashami

  mashami Senior Member

  #5
  Jun 8, 2012
  Joined: May 8, 2012
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nape jr mbona hajaja humu kusema watapika pilau,mchele,au ndizi ili tuje na kachumbari?
   
 6. t

  tara Senior Member

  #6
  Jun 8, 2012
  Joined: Jun 5, 2012
  Messages: 190
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nahisi wao wanaweza kuruhusiwa kuandamana,sababu za kiinterejensia hazionyeshi kama kuna vurugu zinaweza kutokea na isitoshe jeshi la polisi litatosha kabisa kusimamia maandamano....
   
 7. democratic

  democratic JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 21, 2011
  Messages: 1,644
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  vipi mpaka sasa hivi intelejensia ya polisi imebaini chochote?
   
 8. Non stop

  Non stop Senior Member

  #8
  Jun 8, 2012
  Joined: Nov 29, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Its a shame for CCM,. sasa wanafuata nyayo za CDM for sure it is too late.
   
 9. u

  umumura Member

  #9
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Nao wateule (Chadema) wakamshinda yule joka anajidai kuvua gamba (CCM) kwa damu ya Mwana-Kondoo,na kwa neno la ushuhuda wao la ukombozi wa nchi;ambao hawakupenda maisha yao hata kufa.Kwa hiyo shangalieni enyi mbingu na nchi,nanyi mkaao humo watanzania.Ole wa nchi na bahari! kwa maana yule Ibilisi (CCM) ameshuka kwenu mwenye ghadhabu nyingi,AKIJUA YA KUWA ANA WAKATI MCHAHCE TU 2015.
   
 10. KirilOriginal

  KirilOriginal JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2012
  Joined: Feb 13, 2012
  Messages: 1,925
  Likes Received: 446
  Trophy Points: 180
  Tunasubiria matusi ya MKAPA hana jipya zaidi ya kutetemesha kifua na matusi
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Lazima kieleweke ,CCm walisema Kusini ni ngome yao wanajinyea nini,walidhani wananchi wote wa kusini hawajitambui,aibu imewafika wakiona wanawake kwa waume ,vijana kwa wazee wakipanga misululu kugombea kununua kadi yeba inatia hamasa saa ya ukombozi ii karibu,Chadema kazeni mwendo mutuvushe salama kwenye mawimbi ya 2015
   
 12. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  nashauri baada ya huo mkutano chadema waendelee kupiga za uso ili ccm iendelee kusahau wajibu wake mpaka 2015 na uzuri wa chadema haiwezi kufilisika kwa sababu sisi wananchi ndiyo tutachanga hela za kuwakimbiza.
   
 13. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #13
  Jun 8, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nape na ccm ni kama kupe na ng'ombe. Ng'ombe anapo pelekwa machinjioni,kupe haonyeshi kuchukua hatua. Ng'ombe anapo chinjwa,kupe hachukui hatua. Ng'ombe akichunwa ,kupe hachukui hatua. Ngozi ya ng'ombe iki kauka ndo kupe ana anza kuhangaika. POLE SANA NAPE WA MAGAMBA.
   
 14. L

  LOVI MEMBE JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2012
  Joined: Mar 16, 2012
  Messages: 1,121
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  ndio hakujaendelezwa kwakuwa wanaona kule ndiko waliko mazezeta amuke ccm inawaona mazezeta watu wa kusini. Kataeni kuwa mtaji wa mafisadiinanitia uchungu kuona nchi na hasa kwetu tuko mstari wa mbele kuwaunga mkono mafisadi ambao wakibanwa wanashindwa kutoa hata maelezo ya kujitetea jinsi walivyoiibia nchi yetu kwa muda marefu tuamke tuwatoe washenzi hawa hawana adabu. Kwanza warudishe hela walizoibia nchi yetu. Miaka 50 ya kudidimiza nchi yetu lazima kieleweke
   
 15. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: contentheading"]
  [/TD]
  [TD="class: buttonheading, width: 100%, align: right"]
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
  [TABLE="class: contentpaneopen"]
  [TR]
  [TD="class: createdate"]
  Thursday, 07 June 2012 19:58
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]MKUCHIKA, GHASIA, CHIKAWE NA MEMBE WAENDA KUUZIMA, CCM KUJIPIMA NGUVU JANGWANI

  KESHO

  Geofrey Nyang'oro, Mchinga

  VUGUVUGU la Mabadiliko (M4C) linaloendeshwa na Chadema katika mikoa ya Lindi na Mtwara, limewatisha mawaziri wanne wanaotoka katika mikoa hiyo, ambao wamelazimika kurejea majimboni mwao kusafisha hali ya hewa.

  Mawaziri waliorejea majimboni kufanya kilichoelezwa ni shughuli za kiserikali ni pamoja Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Hawa Ghasia, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora), George Mkuchika, Waziri wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe.

  Kwa wiki takribani ya pili sasa, Chadema kimekuwa kikiendesha operesheni hiyo ya vuguvugu la mabadiliko katika mikoa hiyo ya kusini mwa nchi.

  Jana, taarifa zilizopatikana mkoani Lindi zilisema Ghasia alifanya mkutano katika jimbo lake la Mtwara Vijijini akiwa katika harakati za kufuta nyayo za Chadema.

  Oparesheni hiyo ya Chadema jana na leo ilitarajiwa kuingia jimbo la Mtama ambalo linaongozwa na Membe.

  Vuguvugu hilo linaongozwa na viongozi wa ngazi za juu wa Chadema, ambao ni Katibu Mkuu Dk Willibrod Slaa na Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe ambao wanatarajia kuhutubia mikutano yao katika kata aliyozaliwa Membe.

  Mkuchika alithibitisha jana kuwa yuko jimboni kwake Newala, na alipoulizwa kama lengo lake ni kufuta nyayo za Chadema, aling'aka, "Kwani kila siku nikija nyumbani kwangu huwa mnaniuliza, mimi nimekuja nyumbani kwangu bwana. Niacheni nipumzike nyumbani kwangu."

  Membe alipotafutwa kuzungumzia taarifa hiyo simu yake haikuwa hewani, lakini Msemaji wa wizara hiyo, Assah Mwambene alipoulizwa alipo bosi wake alithibitisha kwamba yuko jimboni kwake.

  Jana, vuguvugu hilo lilikuwa katika Jimbo la Mchinga mkoani Lindi, lakini lilikumbana na upepo mzito wa kisiasa baada ya bendera mpya za CCM kuonekana kupamba kona mbalimbali za jimbo hilo.

  Waziri Ghasia na Chikawe pia hawakupatikana kupitia kwa simu zao kuzungumzia taarifa hizo.

  Msigwa ashambulia mawaziri
  Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliwashambulia mawaziri hao wanaotoka majimbo ya mikoa ya Kusini ya Lindi na Mtwara, akihoji ni kwanini wanaikumbatia CCM.

  Msigwa alisema CCM imeshindwa kuwasaidia kuleta maendeleo katika mikoa hiyo ya kusini mwa Tanzania, ndiyo sababu, watu wanaishi katika hali ya umasikini wa kutisha.

  "Mimi ninawashangaa wabunge wa majimbo ya Lindi na Mtwara wakiwamo mawaziri Hawa Ghasia, Mkuchika na Bernard Membe ni kwa nini wanakiunga mkono CCM wakati majimbo yao yamekithiri kwa umaskini," alisema Msigwa na kuongeza;

  "Nashangaa Membe, Hawa Ghasia na Mkuchika sijui kiburi wanakipata wapi. Ndiyo sababu wamehama majimbo yao na kuishi Dar es Slaam, haiwezekani leo mikoa wanayotoka, wilaya na hata majimbo yakawa na sura kama ilivyo sasa. Nitakwenda kuwabana bungeni,'' alisema Msigwa.

  Msigwa alitamba kuwa yeye na wabunge wote wa Chadema wanaishi kwenye majimbo yao, ndiyo sababu wamekuwa wakifanikiwa katika mikakati yao ya kutetea na kuwaletea maendeleo wananchi wao.

  Sugu alia umaskini
  Katika mkutano huo, Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Sugu) alisema ukarimu wa wakazi wa Lindi na Mtwara kwa CCM ndio uliosababisha mikoa hiyo kuwa katika lindi la umaskini.

  Mbilinyi alisema wabunge kupitia chama hicho hawana uwezo wa kuwaletea wananchi maendeleo kutokana na mfumo wa chama hicho kukumbatia matajiri na kuachana na maskini.

  Alisema ndani ya CCM, watu wa kipato cha chini hawawezi kupata ubunge, akitoa mfano kwamba fomu ya ubunge ya CCM inachukuliwa kwa Sh100, 000 ilihali ya Chadema ni Sh50,000.

  "Nawasihi vijana wenzagu kuungana na kuwa na ujasiri wa kuamua katika masuala ya kimaendeleo. Mimi nilikuwa mitaani na muziki wangu, lakini nikatokea Chadema na kunipa nafasi ya kugombea ubunge ,lakini ningekwenda CCM wasingenipa nafasi ya kugombea kwa sababu ya umaskini wangu," alisema Mbilinyi na kuongeza:

  "Hivyo, basi wazee na vijana nawasii kuachana na CCM kwa sababu chama hicho kimekosa mwelekeo tangu alipofariki Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, CCM iliyobaki ni ya wanjanja sio wewe ulioko kijijini."

  CCM kujipima nguvu Jangwani
  Wakati Chadema ikizidi kuwasha moto wa vuguvugu la mabadiliko, Chama tawala CCM kesho kitafanya mkutano wa hadhara katika viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam, kutoa msimamo wake kuhusu mambo muhimu yanayogusa taifa.

  Mkutano huo unafanyika ikiwa zimepita takribani wiki mbili tangu Chadema wafanye mkutano mkubwa katika viwanja hivyo uliohudhuriwa na mamia ya watu, na kuzindua kampeni yake ya M4C', yenye lengo la kushika dola mwaka 2015.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyopatikana katika mtandao wa chama hicho tawala jana, iliyotolewa na Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa huo, Juma Simba ilieleza kwamba mkutano huo utaanza saa 8 mchana.

  Simba alisema katika taarifa hiyo kwamba, chama hicho kitatumia mkutano huo kuwaeleza Watanzania msimamo wake kuhusu hatma ya maisha yao.

  "Utaeleza hatma ya maisha ya Watanzania katika suala la ajira, miundombinu ya barabara, reli, bandari na anga, bei za bidhaa mbalimbali, umeme na rasilimali za taifa," alisema Simba.

  Alifafanua kwamba jambo jingine litakaloelezwa katika mkutano huo, ni msimamo wa chama hicho kuhusu mchakato wa Katiba Mpya pamoja na vurugu za Zanzibar.

  Katika mkutano huo watakuwapo viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali na kutoa ufafanuzi juu ya masuala hayo, yaliyoainishwa kama msimamo wa chama hicho.

  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]
   
 16. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Haya Nape Nnauye anasema hakutishika; Angalia Mawaziri wenye Majimbo walivyoshituka na kukimbilia Ulaji wao Majimboni

  Ni kweli CHADEMA ilifanya kweli huko KUSINI mwa Tanzania... Hata kama Kikwete anasema ni wakati wa Vijana

  anajidanganya Angalia Nchi zenye Demokrasia ya Kweli kama India na United States wao wana Mchanganyiko wa Wazee

  Na Vijana, Unachanganya Hekima sio kuondoa Hekima za Wazee kabisa; Naona Kikwete anafanya hivyo kujilinda

  kwasababu hao Viongozi Vijana watampa neema kwa kuwafungulia Milango kuliko kumuuliza Maswali juu ya Makosa yake

  Madarakani; Nitafurahi Sana kama Vyama Vingine Vya Upinzani havitafuata huo Mkumbo wa CCM; ni mtego
   
 17. Suzie

  Suzie JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2012
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 1,264
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Ukiona wanafikicha pua ujue hali ya hewa ishachafuka na hiyo sio oxygen tena
   
 18. LiverpoolFC

  LiverpoolFC JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2012
  Joined: Apr 12, 2011
  Messages: 11,001
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 160

  Nimeipenda hii! Wapo pabaya kwa 99.9%
   
Loading...