M4C inachangisha kwa ajili ya nini; kiasi gani kimepatikana hadi hivi sasa...

Ni vema kukawa na utaratibu wa kutoa mshindo nyuma(Feedback) kwa watanzania.Mwanakijiji umetoa changamoto nzuri kwa viongozi wa CDM.

Maswali mazuri sana, mimi pia nitatoa laki moja lakini ningependa kuchangia baada ya maswali ya MMM kujibiwa.
Samahani kama tayari CDM walishatoa matumizi na mapato ya uchaguzi lakini kama bado ningependa pia kujua kwani nilichanga mara nyingi sana kupitia simu yangu lakini sikupata mrejesho

Uaminifu ni IMANI!!!

siasa ni DINI YA HAKI KAMA ULIVYO MSINGI MKUU WA DINI ..... HAKI!!! waumini wa siasa ya haki huiamini dini yao kama jinsi wanachama wanavyo waamini viongozi wao na viongozi wao kuamini kusimama katitika misingi ya haki!!

kiongozi ambaye amesimamia misingi isiyojenga HAKI hujenga waumini wa siasa wasio simamia HAKI!!!
ref CCM

chadema ilijengwa, inajengwa na itajengwa kwa msingi wa IMANI YA HAKI bila kujali kiongozi au wanachama........ kwa sababu hii watanzania wengi wamekuwa na IMANI na CHADEMA KUWA KIMBILIO LAO LA KUWAFUNGULIA MINYORORO MIZITO YA UTUMWA!!!

OKOMBOZI WA FIKRA (M4C)NI UFUNGUO WA MINYORORO YA UTUMWA WA FIKRA!!

Majanikv,

Kavishe mimi nakuahidi nitachangia 50000 , ila sitahudhuria maandamano kwa sababu maalum , mipango ikikamilika nicheck , do not worry , hata polisi wanaunga mkono M4C ! Niamini kaka .

Last edited by a moderator:
Mzee Mwanakijiji
Maswali ya kototo we mzee, hivi inamana bado hujui fedha za M4C huwa zinatumikaje kama sio kuuza sura humu ukidhan ni FB? Msitake kuaminisha umma kwamba michango ya M4C ni kwa ajili ya watu wachache pia unauliza ni nani anasimamia fedha za M4C inamna CDM haina mhasibu au kazi za wakina Antony Komu pale makao makuu?
Pumba zenu hizi na akili kama za green guards zipelekeni huko huko magambani na CUF.

Form 6 HKL safi sana bora umemwambia

Last edited by a moderator:
naunga mkono swali hili la Mwanakijiji ni vyema likapatiwa jibu, nakumbuka kuna michango ilitolewa pale Jangwani DSM na kuna watu wengi walikuwa na maswali kama hayo kwamba hizi hela zitakuwa zimefikia kiasi gani na zinatumiakaje?

kwa sasa watu hawaoni umuhimu wa kufanya hivyo lakini miaka inavyoenda utapita upepo mchafu na kuonekana zoezi zima ni ufisadi mkubwa.

moja ya mapungufu ya M4C ambayo kuna watu wamekuwa wakieleza, panakuwa na nguvu kubwa mno ikitokea makao makuu. wenye eneo husika hawahusishwi kikamilifu. na huu udhaifu pia uangaliwe ni vizuri wanaotoka makao makuu wawe wageni ili kuwa impower wenyeji. (mawazo tu)

Hili swali limekaa kishambenga shambenga, kwani huyu muuliza swali hapajui CHADEMA makao makuu? alishakwenda kuhitaji hizi details akanyimwa? au ndio anataka kuamsha Hisia kuwa hela hizi ni kwa ajili ya akina Mbowe and CO? Kweli mtoa mada una mapenzi mema na CHADEMA?

Msingi wa michango ya wananchi kwa taasisi yoyote ni uwazi na uwajibikaji. Lazima CDM irudi kwa iliyowachangisha kueleza kiasi kilichopatikana na ni kwa vipi kimetumika vinginevyo tutawaaminije kwenye makusanyo ya kodi mtakapokuwa madarakani. Naunga mkono kwa asiilimia zote hoja ya Mzee Mwanakijiji. Haiwezi kuwa safari tu ya watu kuchangishwa bila feedback.

Last edited by a moderator:
wewe mwenye akili timamu unajiita mbumbumbu?

Mkuu haina sababu ya kumjibu mjinga achana naye kwanza kabisa nilipo kuta hoja hii nikawapigia baadhi ya viongozi wa cdm nika wasome wakasema watakuja kutolea ufafanuzi embu tusubiri kama ni kweli watatolea ufafanuzi hata Mnyika pia naweza kuja kutolea ufafanuzi kama atapata nafasi

Haya maswali yanatakiwa pia kujibiwa kwa kadiri harakati za M4C zinavyozidi kupamba moto. Ni muhimu kuyajibu ili kuonesha uwajibikaji, uwazi, na umakini.

a. M4C inachangisha fedha kwa ajili ya nini?
b. Kiasi gani cha fedha kinachokusanywa kinabakia katika maeneo husika (Mwanza in this case; kanda ya ziwa) - it has to be by percentage.
c. Hadi harakati hizi zilipoanza ni kiasi gani kimepatikana na kiasi gani kimeshatumika kufikia lengo la (a)?
d. Nani anasimamia fedha za M4C?
E. Nani anayesimamia project nzima ya M4C na anawajibika kwanini akiongozwa na utaratibu gani?

Binafsi najitolea kuchangia kidogo: Tsh. 100,000/= kuendeleza harakati!

Wale wengine wa hapa ambao nao wanataka kupledge please do with me... how much u want to give for M4C. Napendekeza CDM iteue mtu wa kucoordinate michango ya watakaotoa kutoka kwenye mitandao.

Asante sana kiongozi kwa kuja na maswali ya msingi sana katika kuleta uwajibikaji na uwazi. Ukweli niliwahi kumwambia Heche personally nipo tayari kutoa hata shilingi Million moja au zaidi kwani ninaamini ana katika mabadiriko ya kweli. Lakini kama ulivyoelza hapo juu ni muhimu kujua kwa uwazi kabisa ni kwa kiasa gani kwa namna gani ufanisi na malengo ya hii movement yanaweza kufikiwa, nani anawajibika kwa nani na kwa nini au lipi, ni kwa kasiai gani halengo haya yamefikiwa na ni yapi.
Project hii ni tanmgible kwa kiasi gani kwa mchangiaji? well, kama ni issue ya maandalizi ya campaign 2015 ni jambo jema tena sana tu, lakini lazima wananchi tufahamishwe vyema kabisa na control ya hii fundi ilivyo.
Yangu ni hayo.

Chadema iko kuendeleza uchaga uchaga kwa kutumia migongo ya wapumbavu wachache wasiojitambua

Jana nimeulizwa swali kama hili hii ni michango ya watu tunatakiwa kuwa nayo transparency tusifiche kitu imepatika sh tano tuonyeshe hiyo sh tano imetumika vipi ili kesho tupata sh kumi.

Mimi nadhani wale wa arusha pale ilikofanyika wangetupa hesabu walikusanya sh ngapi zikatumika sh ngapi + pale dar serena ambapo ahadi na fedha tasilimu zilikua milioni 500 lengo likua bilioni 5 je zilifikiwa je hawa wa dar wana plan gani tena kufikisha hiyo amount kabla mwaka haujaisha.

Mimi nafikiri tufanye kitu fulani hivi mimi nahuzunika nilikosa na dar masomo yalinibana lakini kidogo sasa niko free sasa kiongozi yoyote wa dar wakishatupa mahesabu ya pesa zilizopatikana tuje na kitu kingine matembezi ya amani.

Let say kushikiri matembezi hayo utalipia sio chini ya 20000 tu target watu 5000 wa daressalaam nina uhakika tutawapata kama tutaanza matangazo mapema mpaka kwenye social media viongozi wote washiriki mimi nitakua bega kwa bega hapa tuna uhakika wa kupata 1 bilioni ili kufikia lengo la bilioni 5.

Hayo matembezi mfano wa wilaya ya kinondoni yanaongozwa na mdee na mnyika,mnyika anachukua watu wote wa kimara huku kuelekea jangwani,mdee anaongoza kutokea kawe kupitia hadi jangwani,na sehemu nyingine itakavyopangwa.

Hii itasaidia nini tunapohitimisha baadae kwenye mkutano mkubwa watu wataku inspired to contribute more wengi wataelewa vizuri lengo la m4c,tutakitangaza chama dar yote maana kila kona kutakua na matembezi kuelekea jangwani,tunakata ngebe za ccm rasmi,

Pili pale jangwani kuwe na hotuba nzito itayolezea chadema tuko tayari sasa kuongoza nchi tuna uwezo.

Sasa tunawezaje kuwapata hao watu 5000 maandalizi yaanze leo matembezi yawe mwezi 3 tuseme wanachama wenye mapenzi ya kweli ya chadema wana miezi 3 kuweka 20000 ya matembezi kusaidia movement ya m4c,mtu atakua na siku 90 kila siku anaweza kuweka 200 kwa miezi 3 akaweza pata ticket na ingependezwa wote tuwe ndani ya tshirt za m4c.

Naomba kuwasilisha na mikoa mingine waige hii idea tunapoita watu hotel fulani tunaonyesha kuna tabaka fulani tunalitenga hapana tufanye matembezi tena tukifanya na mikoa mingine matembezi ndo chama kitambulika mapema sana.

All the best kwa jioni ya leo

Fred kavishe
Hiyo ni bonge la idea,I think CDM needs to take it seriously,itakifikisha chama kukaribia malengo ya M4C.

Sent from my BlackBerry 9810 using JamiiForums

Haya maswali yanatakiwa pia kujibiwa kwa kadiri harakati za M4C zinavyozidi kupamba moto. Ni muhimu kuyajibu ili kuonesha uwajibikaji, uwazi, na umakini.

a. M4C inachangisha fedha kwa ajili ya nini?

b. Kiasi gani cha fedha kinachokusanywa kinabakia katika maeneo husika (Mwanza in this case; kanda ya ziwa) - it has to be by percentage.

c. Hadi harakati hizi zilipoanza ni kiasi gani kimepatikana na kiasi gani kimeshatumika kufikia lengo la (a)?

d. Nani anasimamia fedha za M4C?

E. Nani anayesimamia project nzima ya M4C na anawajibika kwanini akiongozwa na utaratibu gani?

Binafsi najitolea kuchangia kidogo: Tsh. 100,000/= kuendeleza harakati!

Wale wengine wa hapa ambao nao wanataka kupledge please do with me... how much u want to give for M4C. Napendekeza CDM iteue mtu wa kucoordinate michango ya watakaotoa kutoka kwenye mitandao.

Believe me, huwezi kupatiwa jibu lenye akili kwani ufisadi umeingia CHADEMA na hakuna aliyetayari kuukemea kwa sababu common intrest ni 2015. Mimi ningekuwa mbunge wa CHADEMA nisingekubali kuchangia bakuli lililotoboka. Kimsingi bakuli lina tundu kubwa na aliyelitoboa anafahamika ila ukimpenda mke penda na tabia zake.

Back
Top Bottom