M4C inachangisha kwa ajili ya nini; kiasi gani kimepatikana hadi hivi sasa...

Hii ni moja ya challenge zinazoikabili chadema kama wapambanaji wakuu wa ufisadi na nguzo kuu katika matumaini ya ukombozi mpya kwa watz. Tafadhali wasemaji wa chama kama haiwezekani kuweka hapa jf walau sehemu ya majibu basi myaweke kwenye website yenu yawe public hasa swali la pili la mzee
 
Kila siku tunang'ang'ania serikali iweke wazi mikataba inayoingia na wawekezaji...lakini pesa za harambee ya M4C ni vigumu kupata mchanganuo. Wahusika tuwekeni wazi tujue hiyo itaongeza imani zaidi kwenu
 
michango husika asilmia kubwa hubaki pale kama uliona madawati yale shule nyingi zilipata ,pia chama kama chama ruzuku haitoshi kufanya kazi ya kujenga chama ,gharama za mafuta ,na mambo kadhaa hizi hela huziba pengo lile .hivyo basi nakusihi uendelee kutoa michango yako ,kutoa ni moyo hujalazimishwa kwa namba zile zile na pia nikupongeza kwa swali lako nzuri makofi tafadhali
 
Nimekuwa muumini mzuri wa vyama vya SIASA kuendeshwa na WANACHAMA na washabiki wao ili tufike mahala RUZUKU inayotokana na KODI zetu sote tulio na tusio na vyama ielekezwe kwenye huduma za jamii. Uchangishaji huu wa M4C nadhani unalenga huko
 
Hili swali limekaa kishambenga shambenga, kwani huyu muuliza swali hapajui CHADEMA makao makuu? alishakwenda kuhitaji hizi details akanyimwa? au ndio anataka kuamsha Hisia kuwa hela hizi ni kwa ajili ya akina Mbowe and CO? Kweli mtoa mada una mapenzi mema na CHADEMA?

Mkuu Mwanakijiji ameuliza maswali ya msingi sana kwani hii ndiyo njia ya kuonyesha uwajibikaji na transparency na laziama ianzia ndani ya chama

Binafsi naungamkono hoja ya mwanakijiji
 
Haya maswali yanatakiwa pia kujibiwa kwa kadiri harakati za M4C zinavyozidi kupamba moto. Ni muhimu kuyajibu ili kuonesha uwajibikaji, uwazi, na umakini.

a. M4C inachangisha fedha kwa ajili ya nini?
b. Kiasi gani cha fedha kinachokusanywa kinabakia katika maeneo husika (Mwanza in this case; kanda ya ziwa) - it has to be by percentage.
c. Hadi harakati hizi zilipoanza ni kiasi gani kimepatikana na kiasi gani kimeshatumika kufikia lengo la (a)?
d. Nani anasimamia fedha za M4C?

Binafsi najitolea kuchangia kidogo: Tsh. 100,000/= kuendeleza harakati!

Wale wengine wa hapa ambao nao wanataka kupledge please do with me... how much u want to give for M4C. Napendekeza CDM iteue mtu wa kucoordinate michango ya watakaotoa kutoka kwenye mitandao.

Kuna wakati mtu unaweza kujiuliza swali kama hilo, lakini ukiwa ndani ya wahusika wenyewe na kujua pengo lililopo katika matumizi yao na mikakati waliyo nayo kama mfukoni unazo utaamua bora kupunguza moja ya matatizo mengi waliyo naya.

Rafiki yangu kanitumia email na kuniambia Barack Obama wa Marekani licha ya chama chake kufaulu nafasi ya urasi lakini bado michango inaombwa na watu wanaendelea kuchangia. Kama hao ni hivyo sembusi chama kama Chadema?
 
Mimi nitakuwepo na kuchangia kwa jumla nitatumia laki unusu kwa kiingilio cha dinner na 50000 kwa mchango moja kwa moja, ni suala la msingi tukiwa na taarifa za michango hii, itatupa moyo kuchangia zaidi.
 
kichwa kama sambusa ya kuokota.[/QUOTE]

KUMBE NA WE MMK HUNAGA AKILI TIMAMU.. HIYO RESPONSE YAKO IMEBEBAJE HOJA YAKO.?
 
Hili swali limekaa kishambenga shambenga, kwani huyu muuliza swali hapajui CHADEMA makao makuu? alishakwenda kuhitaji hizi details akanyimwa? au ndio anataka kuamsha Hisia kuwa hela hizi ni kwa ajili ya akina Mbowe and CO? Kweli mtoa mada una mapenzi mema na CHADEMA?

Mtoa mada anamapenzi ya kweli sio mapenzi ya upofu! Wana cdm wengi wanamapenzi ya woga na upofu.hakuna haja kwenda makao kama mtu yoyote anajua majibu ya maswali hayo atuwekee hapa. Vinginevyo tutaanza kuamini ya mitaani.:confused:

Sent from my GT-I9300 using Tapatalk 2
 
Ukitaka kuyapima mawazo na maoni ya Watanzania kuhusu rushwa na ufisadi unaweza kupata mitazamo yao katika maswali kama haya ambayo hata hayahitaji fikra zamifu kupata majibu lakini kwa vile hatuoni tatizo ndani ya nyumba yetu wakati jirani yetu analiona, hata huo ushauli tutakao mpatia jirani hawezi hata kuusikiliza achilia mbali kuufanyia kazi.

Haijalishi muuliza swali ni nani na ana malengo gani, cha muhimu ni kumpatia jibu la swali lake maadamu hilo swali sio personal na linahitajika liwe kwenye public domain.

Nitashangaa kwa chama makini kama CHADEMA hakitakuwa na utaratibu wa uratibu na kuonyesha mapato na matumizi ya pesa katika vitabu vyake.

Tusubiri wasemaji wa chama humu jf kwa majibu mbadala.
 
Unafikiri umezungumza kitu cha akili; kichwa kama sambusa ya kuokota.

leonimecheka sana kidogo nife lol, mwanakijiji umenipa raha sana ijumaa ya leo, ngoja niongeze glass yangu ya san miguel hapa kupambana na hii winter . Kuhusu mada ni kweli CDM wamefanya fund raising arusha na pia dar es salaam lakini hadi leo hatujangaziwa kiasi kilichokusanywa na kimetumikaje, ni vizuri uongozi wa chama utoe taarifa hizi vinginevyo sioni ubavu wa watu kusimama kuikosoa CCM.
 
Hakuna sababu yoyote ya usiri; naamini kuna mtu atatoa majibu tu mazuri na kufunga huu mjadala.
 
kuchangia madawati na huduma za jamii dhambi lkn kuchangia huo ujinga wenu mnaona ni sawa, mnatuandaa vp kuwa wazalendo? naendelea kusema kuwa chama bado hakijakomaa ni kama puto linalopaa kwa kutumia upepo likikutana na mwiba kdg ndio mwisho wake.
 
Swali la msingi, je endapo takwimu hizo zikitoka zitatumikaje kukiattach chama?????

Pili, je zipo au hazipo kabisa????? Najua CDM ni chama makini kinapaswa kuwa na takwimu hizi endapo ikibidi waliochanga kuzihitaji isiwe za kutafuta maana itakuwa ni wakati muafaka kuzitoa.
 
Back
Top Bottom