M4C imeshindwa kuiteka TANGA?

nimehudhuria mkutano wa chadema Tanga wiki iliyopita ulikuwa na watu wachache sana kulinganisha na wingi wa wakaziwa tanga.

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
Tanga ni Pemba ya Tanganyika usishangae kuona CUF ina nguvu kuliko CDM,cha msingi ni mabadiriko haijalishi yameletwa na nani, watanzania tunapaswa kukiweka pembeni hiki chama cha familia za kupita bila kupingwa kwa njia iliyo muafaka na yenye ufanisi kulingana na mahali husika bila kujali itikadi za vyama mbadala.
 
nchi nyingi zina wahafidhina wake yaani watu wasiopendelea mabadiliko.TANGA watu wake wengi wako kihivyo. taratibu elimu ya uraia ikiwakaa watabadilika watapenda mabadiliko kama walivyo fanya mikoa mingine.
 
kwa muda wa mwezi mmoja nimekuwepo jijini Tanga ,pamoja na mambo mengine nilitumia muda wangu kuwahoji wakazi wa Tanga juu ya muelekeo wa kisiasa.kimsingi inaonekana chadema haijakubalika ndani ya mkoa wa Tanga na mbadala mkubwa wa ccm kwa Tanga ni CUF.
Sasa najiuliza je M4C imeshindwa kushawishi wakazi wa Tanga?
KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
Nakumbuka Igunga kuna watu walijidanganya hivyo hivyo...mara oh! Chadema haina chake Igunga, mara oh! CUF ina mtaji Igunga na mara oh! Chadema haitaambulia chochote Igunga. Mikoa ya Kusini nako hivyo hivyo...Chadema haikubaliki Lindi na Mtwara ni ngome ya CUF! Unakumbuka hali ilivyokua huko Ruvuma?

Morogoro nayo ilikuwa hivyo hivyo...wambea wakadai na hata kutishia Chadema isithubutu kukanyaga Morogoro na kweli kijana wa watu kapoteza maisha. Arumeru Tendwa aliitangazia hali ya hatari Chadema kama ingethubutu kutotii onyo la wazee wa mila na hata Tabora inasemekana "chuma cha pua" Sitta amejiapia kwamba ngome yake haipenyeki! Yetu macho!

jingalao, hii ya Chadema ni tsunami, ukisikia iko njiani unaipisha...binadamu hashindani na tsunami, waulize Wajapani. Tanga iko njiani. Twanga kotekote itakapotua Tanga, hutasubiri utangaziwe kupitia redioni, mawimbi yake yatakutoa hata ukiwa ndotoni. M4C inaisogelea Tanga na ambaye hatakuwa tayari kuipisha, ajitayarishe kusombwa na mawimbi...
 
Rasilimali zikimalizika tu watavunja mkataba wa Muungano ili wajitenge kwi kwi kwi.... hizi njemba zinajifanya zina akili sana katika kuwazuga Watanganyika.

Kwi! sasa wanataka muungano wa mkataba!
 
nchi nyingi zina wahafidhina wake yaani watu wasiopendelea mabadiliko.TANGA watu wake wengi wako kihivyo. taratibu elimu ya uraia ikiwakaa watabadilika watapenda mabadiliko kama walivyo fanya mikoa mingine.
Uko sahihi. Halafu cha ajabu wakazi wengi wa huko hali zao za maisha sio nzuri?
 
Kama ulikwenda na kumuuliza babu yako, obvious ni lazima majibu yawe hayo. Ingawa sio mbaya ila usifanye generalization kwa sample ya watu 3 kati ya 2M.
 
Jina la mleta dhread lina shida,
M4C itakuwa mikoa ya pwani,Tanga,mwishoni mwa October,itakumbukwa kuwa ilipangwa kwa kanda kuanzia na kanda ya kati,kabla ya policcm kuanza kuua wananchi.Hata hivyo itaendelea kama ilivyokuwa ratiba ya awali,
 
Nakumbuka Igunga kuna watu walijidanganya hivyo hivyo...mara oh! Chadema haina chake Igunga, mara oh! CUF ina mtaji Igunga na mara oh! Chadema haitaambulia chochote Igunga. Mikoa ya Kusini nako hivyo hivyo...Chadema haikubaliki Lindi na Mtwara ni ngome ya CUF! Unakumbuka hali ilivyokua huko Ruvuma?

Morogoro nayo ilikuwa hivyo hivyo...wambea wakadai na hata kutishia Chadema isithubutu kukanyaga Morogoro na kweli kijana wa watu kapoteza maisha. Arumeru Tendwa aliitangazia hali ya hatari Chadema kama ingethubutu kutotii onyo la wazee wa mila na hata Tabora inasemekana "chuma cha pua" Sitta amejiapia kwamba ngome yake haipenyeki! Yetu macho!

jingalao, hii ya Chadema ni tsunami, ukisikia iko njiani unaipisha...binadamu hashindani na tsunami, waulize Wajapani. Tanga iko njiani. Twanga kotekote itakapotua Tanga, hutasubiri utangaziwe kupitia redioni, mawimbi yake yatakutoa hata ukiwa ndotoni. M4C inaisogelea Tanga na ambaye hatakuwa tayari kuipisha, ajitayarishe kusombwa na mawimbi...

M4C with No Apology.
 
Si kweli kwamba chadema haikubaliki Tanga! Sisi tunao ishi huku tunaona mabadiliko yanayo jibu kiu za wanaTanga. Leo hii huwezi kwenda jimbo lolote la uchaguzi katika mkoa wa Tanga bila kukuta bendera za Chadema, juzi nimeshangaa nilienda milimani sana jimbo la Muheza (Amani) nimekutana na bendera za chadema vijijini na badiliko hilo ni baada ya ziara ya zitto kabwe na john heche walipo kuja kuleta hoja ya mkonge. Vipi kama m4c ikija kijiji kwa kijiji mtaa kwa mtaa?!
Mabadiliko ni mpango wa Mungu hayata acha jiwe bila kupinduliwa.

Sent from BlackBerry 8520 authorized by JamiiForums.
 
M4C tanga haijafika ila kwa lushoto chadema ina nguvu sana na ni sehemu ya Tanga..
 
Ni suala la muda na hatimae ratiba, kimkakati na hasa kiufundi.

Hakuna anayependa maisha magumu, elimu, afya na miundombinu dun. Hivyo suala si cdm bali uwezo wa tim za m4c ndan ya cdm kupambanua namnagan haki za watanzania zinavyo porwa na mafisadi ndan ya ccm na kuwasababishia hali ngum ya maisha.

Walisema moro m4c haitakanyaga, nyote mashahid pamoja na fujo za polisiccm bado kilieleweka.

Hivyo muda wa watanzania wa tanga kukombolewa kimkakati ukiwadia cdm itatia timu na kwa kishondo watathibitisha kwamba wapo kuwakomboa watanzania.
 
Back
Top Bottom