M4C chini ya kamanda Mawazo yaendelea kuvunja ngome ya CCM Geita | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

M4C chini ya kamanda Mawazo yaendelea kuvunja ngome ya CCM Geita

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OMUSILANGA, Sep 23, 2012.

 1. O

  OMUSILANGA JF-Expert Member

  #1
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 384
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ndiyo wakuu, heshima kwenu. Katika kutimilika kwa kauli ya mjinga akijitambua,mwelevu upo matatani ,hali imeendelea kujidhihirisha wiki hii ktk jimbo la Busanda, mkoani geita.

  Kwa mujibu wa maelezo ya Kamanda Mawazo Seleman, diwani wa zamani wa kata ya Sombetini, Arusha, aliye jivua gamba na kuvaa gwanda ni kuwa katika kata ya Katoro walivuna wanachama 150, kata ya Kaseme ktk vijiji vya kaduda na magenge walivuna wanachama 200, jana ktk kata ya Lwamugasa walivuna wanachama 200, jana hiyo hiyo jioni katika maeneo ya Kilombero moja walivuna wanachama 78 na Kilombero mbili walivuna wanachama 110.

  Leo mashambulizi yata endelea katika kata ya Bulela. Hivyo kwa uhalisia tu M4C wiki hii imevuna jumla ya wanachama wapatao 738. Haya ni maeneo ya vijijini ndani kabisa ambapo ccm chini propaganda za Nape wamekuwa wakijidai kuwa ni mtaji kwao. Je kwa mrejesho huu bado ccm ina mtaji vijijini? Zaidi tuta endelea kujuzana kuhusu harakati hizi. Naomba kuwasilisha.
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Sep 23, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Tulianza na Mungu na Tutamaliza na Mungu.........:rockon:
   
 3. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #3
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  kila la kheri
   
 4. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #4
  Sep 23, 2012
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Chadema inanze kufundisha wapiga kura kulinda kura zao baada ya kupiga, wakifanya hivyo CCM bye bye 2015....
   
 5. Sabung'ori

  Sabung'ori JF-Expert Member

  #5
  Sep 23, 2012
  Joined: Jul 19, 2011
  Messages: 2,087
  Likes Received: 150
  Trophy Points: 160
  *Wanachama wake 300
  watimkia Chadema
  ZAIDI ya wanachama 308 wa
  Chama Cha Mapinduzi (CCM)
  wilayani hapa, wamejiunga na
  Chama cha Demokrasia na
  Maendeleo (CHADEMA).
  Wanachama hao wamejiunga
  na Chadema kupitia mikutano
  mbalimbali ya Operesheni
  Sangara ya chama hicho chini ya
  kauli mbiu yake ya Vuguvugu la
  Mabadiliko (M4C).
  Mikutano hiyo inayofanyika
  katika vijiji mbalimbali vya
  Wilaya ya Geita, inaongozwa na
  aliyekuwa Diwani wa Sombetini
  mkoani Arusha kuptia CCM,
  aliyehamia Chadema, Alphonce
  Mawazo.
  Wanachama hao ambao baadhi
  yao ni wafuasi wa CUF,
  wanatoka vijiji vya Bukondo,
  Kaduda na Katoro, huku kati ya
  hao, 100 ni wanachama wapya
  wasiokuwa na vyama.
  Wakizungumza na Mtanzania
  kuhusiana na sababu za
  kujiunga na Chadema,
  wanachama hao walisema ni
  kutokana na Serikali ya CCM
  kukithiri kwa ufisadi.
  Walisema ufisadi na wizi wa
  fedha za umma umekuwa
  mkubwa serikalini, hali ambayo
  imefanya Serikali ishindwe
  kutatua kero mbalimbali
  zinazowakabili wananchi wa
  kipato cha chini.
  Mkazi mmoja wa Kijiji cha
  Kadudu, aliamua kujiunga na
  Chadema pamoja na wake zake
  wawili, kutokana na kuchoshwa
  na uonevu aliofanyiwa na
  Mtendaji wa Kijiji hicho, Fundi
  Makanza.
  Mtendaji huyo anadaiwa
  kumweka ndani mkazi huyo
  kwa kosa la kuwaandaa watu
  kujitokeza katika mkutano wa
  hadhara uliokuwa uhutubiwe
  na viongozi wa Chadema.
  Alisema ameamua kujiunga
  Chadema pamoja na wake zake
  wawili baada ya kuchoshwa na
  manyanyaso ya mtendaji huyo
  aliyejigeuza Mungu mtu na
  kwamba ameigeuza ofisi yake
  kuwa Mahakama.
  “Nashukuru viongozi wa
  Chadema wamenitoa, kutokana
  na shukurani hizi nimeamua
  nihamie Chadema maana
  pamoja na kuwa kada mzuri wa
  CCM sioni mabadiliko yoyote
  zaidi ya manyanyaso ya kila siku
  tunayofanyiwa na mtendaji.
  “Ukifikishwa ofisini kwake ni
  kama umefikishwa
  mahakamani, maana yeye
  huyohuyo ni mtendaji, ni polisi
  na mahakama, kwa hali hiyo
  unawezaje kuipenda CCM na
  kuendelea kubaki
  huko?”alilalama mwananchi
  huyo.
  Chanzo:Gazeti la Mtanzania
   
 6. KIJOME

  KIJOME JF-Expert Member

  #6
  Sep 23, 2012
  Joined: Jun 7, 2012
  Messages: 3,079
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 145
  Ndio somo lililopo mkuu kuna kauli mbiu,piga kura linda kura yako.
   
 7. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #7
  Sep 23, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,200
  Likes Received: 10,545
  Trophy Points: 280
  CDM go go go......Tilianza na Mungu tunamaliza na Mungu
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Sep 23, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  huko si nasikia serikali ya ccm imepewa tsh 22mil ili kuwalipa posho polisi ili wachome nyumba za wananchi.
   
 9. m

  moseskwaslema Member

  #9
  Sep 23, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 92
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  pamoko sana makamanda wa m4c
   
 10. Havizya

  Havizya JF-Expert Member

  #10
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 1,573
  Likes Received: 169
  Trophy Points: 160
  M4C noumar! Mwendo mdundo mpaka 2015, hakuna kulala mpaka kieleweke!
   
 11. DALLAI LAMA

  DALLAI LAMA JF-Expert Member

  #11
  Sep 23, 2012
  Joined: Jan 31, 2012
  Messages: 8,617
  Likes Received: 401
  Trophy Points: 180
  hongera Mawazo,WEWE ULISEMA UNAITAKA KARATU,toka hapo UDSM uende kupiga kambi M4C KARATU MKUU Japo ni chadema ila utaendeleza harakati
   
 12. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #12
  Sep 23, 2012
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Ndiyo dawa iliyobaki kumwadhibu dhalim ccm.
  Ndipo watajua kuwaTz ina wenyewe.
   
 13. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #13
  Sep 23, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Asante OMUSILANGA kwa taarifa mkuu!
  Hivi Synovate hawawezi kutupatia idadi ya wanachama hai na watiifu kwa ccm?
  Masikini Kikwete wa watu!
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,391
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Kama mtoto wa miaka mitatu anajua people power, basi tena.
   
 15. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Mkuu hawawezi kabisa. maana data zao wakishazipata wanapeleka "kivukoni" zikapikwe! Wanaposoma wanakuwa kama Samwel Kivuitu. Kwamba hata yeye hajui chochote. Amepewa asome tu!
   
Loading...