M/Rais Mhe. Samia Suluhu, Hassan ataka Uwajibishaji/Utumbuaji ufuate taratibu na Sheria

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan amewataka viongozi wa serikali na vyama vya siasa nchini kufuata taratibu na sheria za utumishi wa umma katika kuwajibisha wakosaji. Amewataka viongozi hao kuwapa nafasi ya kujieleza watumishi hao kabla ya kuwawajibisha/kuwatumbua.

Ni kama Mama Samia anakosoa aina na namna ya utumbuaji wa majipu unaoendelea hapa nchini. Nini kimemsukuma Mama Samia kusema hivyo? Nimeona na kusikia tu kupitia ITV Habari.

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Iringa)
 
Labda atakuwa kaongea kuwapa info wanaoiga utumbuaji wa mkuu wake..!!
 
Katumwa kuweka sawa hali ya kisiasa hasa baada ya mkuli kulaumiwa kila kona.
Namiye naona ni namna fulani ya kujiweka tayari "kuupokea" Uenyekiti wa Ccccm, zoezi lililoota mbawa wiki chache zilizopita, pamoya na mambo mengine, sababu ya "utumbuaji wa ma jeep".
 
Akizungumza leo hapa Geita,amepinga utaratibu wa kutumbua watumishi wa serikali bila kufuata taratibu na sheria.Alikuwa akizungumza na watumishi wa sekta ya afya mkoani Geita katika maathimisho ambayo kitaifa yanafanyika Geita.Ikumbukwe kuwa katika hotuba yake msemaji wa Kambi ya Upinzani Katiba na Sheria Mh.Tundu Lisu aliionya serikali kuacha kujichukulia sheria mkononi.
 
Wataunga mkono watu wote wenye uelewa maana hakuna sababu ya kukataa kufuata sheria wakati wameapa kuzilinda..hata kama wanachofanya kina wafurahisha wananchi lazima wafuate sheria maana ndio msingi wa utawala bora
 
Back
Top Bottom