M/kiti wa kijiji ngerengere akwapua zaidi ya million 15 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

M/kiti wa kijiji ngerengere akwapua zaidi ya million 15

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mapambano Yetu, Aug 27, 2012.

 1. Mapambano Yetu

  Mapambano Yetu JF-Expert Member

  #1
  Aug 27, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 180
  Kulingana na maadili ya kazi yangu siruhusiwi kujihusisha na siasa. Lakini kinachonishangaza ni mfumo mbovu uliojengeka wa kulindana pale kiongozi anapofanya makosa. Nakubaliana Dr Slaa kwamba watanzania tumelishwa limbwata, hivyo tunakubali yote yanayofanywa na viongozi wetu. Siku za hivi karibuni M/KITI tena (mstaafu aliyekuwa na cheo kikubwa jeshini) ametangaza kujiuzuru uenyekiti wa kijiji huku nyuma akikabiliwa nashutuma za kukwapua zaidi ya millioni 15. cha kushangaza watendaji ngazi ya kata na tarafa wamekuwa kimya na kulifanya jambo la siri kwao. na si hilo tu taarifa kutoka miongoni mwao zinasema kuna kiasi kikubwa cha pesa kilichokwapuliwa mbali hizo za M/KITI. NGERENGERE ni eneo dogo sana kiutendaji lakini eneo hili linaongoza kwa vitendo viovu na ukandamizaji wa democrasia. Kila kiongozi anataka aonekane yuko juu ya mwingine. Ukipingana na taratibu zao unaundiwa njama mbovu ikiwemo kuhamishwa NGERENGERE. Mtendaji wa kata kawa mwanasiasa na sasa anashulika na siasa badala ya kuhudumia watu wake. Kila ziara ni yeye na diwani wake anatoa takwimu za uongo kurubuni wananchi vijijini. Tunafahamu wazi kuwa viongoz karibu wote wa kisiasa hapa NGERENGERE ni CCM, lakini sio kigezo kwa Mtendaji wa kata, Kijiji, Afisa tarafa, viongoz wa majeshi kushughulika na siasa badala ya shughuli muhimu kulingangana na madaraka yao. Mfumo kuwatisha waliochini yenu hausaidii hata kidogo zaidi unaongeza chuki lawama kwenu. Pia nawasihi acheni ufisadi wa madawa na pesa za maendeleo ya wananchi. Msifikili hatujui mnayoyafanya tunajua sana lakini ndoa tuliyofunga na serikali ndo inatufunga midomo. Mbunge na Diwani simamieni maendeleo ya walio wachagua na sio kukaa mbali na maeneo yenu ya kazi. Utendaji mbovu wa kazi kwa wale wote waliochini yenu utawaponza ninyi. na itageuka na kueleweka kuwa mna ubia na wote walio chini yenu. Tumieni busara kutatua matatizo na sio vitisho na kuwafukuza/kuwahamisha walio chini yenu pale wanapowakosoa. Pia kuwanyima haki zao hukusaidii hata kidogo. TUNAONA, TUNAPIMA NA TUNASHAURI LAKINI ITAFIKA WAKATI TUTAPINGA INGAWA HATURUHUSIWI
   
 2. Kashaijabutege

  Kashaijabutege JF-Expert Member

  #2
  Aug 27, 2012
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 2,699
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Weee soldier, angalia CCM hawataniwi. Utashangaa hata tu-Vii twako watatukwangua.
   
 3. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #3
  Aug 29, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Hapo Ngerengere ndio asli ya Mke wangu hapo. Kama huko hapo ulizia tu Mzee Mnifu. Lakin pia Mwenyekiti wa hapo ni school mate wangu Tambaza anaitwa Kaimu Pagai. Ngoja nitafuatilia habari hii kwa simu huko Ngerengere kujua usahihi wake.
   
 4. Mapambano Yetu

  Mapambano Yetu JF-Expert Member

  #4
  Sep 4, 2012
  Joined: Aug 14, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 960
  Trophy Points: 180
  Pagai ndo mtuhumiwa
   
 5. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #5
  Sep 5, 2012
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Nakumbuka Rais wenu Mkapa aliwahi kusema kuna watu wana wivu wa Kike. Japo wanaharakati wa haki za akina mama walilalama sana lakin ukweli unazidi kubaki pale pale. Kijana una wivu wa kike.

  Nimeongea nae Maj Kaim Zubeir Pagai (Rtd) ambaye ni mwenyekiti amesema Tuhuma hizo ni batili kabisa na uzandikiwa hali ya juu sana kwa kijana wa kiume kuutoa. Mahakama ipo wazi na vyombo vingine va sharia vipo wazi kama una malalamiko peleka huko ili kuiokoa jamii . Kwani kuleta hapa Jamii forum hakusaidii au kuisaidia jamii hiyo ya watu wa Ngerengere.

  Acha wivu wa kike kwa kuweka habari za uongo na chuki binafsi kw a Schoolmate wangu Kaimu.
   
Loading...