M/kiti Chadema mkoa wa Morogoro naye kung'olewa kama Katibu wake Sep 03.

DT125

JF-Expert Member
Oct 19, 2011
380
573
Mtoa taarifa aliyepo Morogoro ambaye juzi alinijuza kuwepo taarifa ya kujiuzulu katibu wa mkoa huo na mie kuitoa kama tetesi JF na baadae kuthibitika. Sasa amenijulisha kuwepo mpango wa kumng'oa Mh. Suzana Kiwanga (MB viti maalumu) kwenye nafasi ya Mkoa wa Morogoro.

Wajumbe kutoka wilaya za mkoa huo watakutana Sept 03 mwaka huu kupanga safu ya uongozi ngazi ya mkoa chini ya usimamizi wa Dr. Slaa ili kuimarisha uongozi mkoani hapo ili moto uliowashwa na M4C usipoe mpaka 2015. Wajumbe wa wilaya za Kilombero na Manispaa ya Morogoro wanadaiwa kuwashawishi wajumbe toka wilaya nyingine ili wamtose M/kiti huyo.

Tuhuma zinazoelekezwa kwake ni pamoja na;

  1. Anaendesha chama mkoa kwa simu kwani makazi yake ni Kinondoni DSM na huonekana Morogoro tu kama kuna ugeni wa Kitaifa au vikao vya chama.Na kukwamisha shughuli za chama za kila siku.
  2. Siyo mtu wa kujitoa kwa mali kukijenga chama pamoja na kupata ubunge. Kwa mfano;Mkoa hauna ofisi hata M4C imewalazimu kazi zao kupanga Mt. Uluguru Hotel. Mkoa na wialaya wamepanga kachumba kadogo mno tena kachumba kalikotengenezwa na wanachama wa kawaida.Hajaleta gari yake hata moja kwenye oparesheni inayoendelea, hata yeye anadadia gari ya Dr. Slaa.
  3. Anadaiwa kuwa mwanasiasa za kutengeneza makundi kwenye chama, anatuhumiwa kuvuruga uongozi wa chama wilaya ya Kilombero enzi za uhai wa Marehemu Regia Mtema kipenzi cha wana Kilombero na sasa anavuruga mkoa mzima. Haoni ghalama anapotaka kumwangamiza mwenzake. Kwa mfano aliwahi kuwasafirisha wajumbe toka Kilombero wakati wa uhai wa marehemu Regia agenda ikiwa kutaka kuwatosa wajumbe wa kamati tendaji wilaya waliokuwa wakimuunga mkono marehemu.
  4. Anadaiwa amekwamisha kupatikana kadi za kutosha wilayani, kwenye kata mpaka matawini. Kwani anatuhumiwa kununua kadi sh 300/= zote zinazotengwa kwa mkoa wa Morogoro na kuanza kuziuza mwenyewe kwenye mikutano kwa sh. 1500/=bila kuwasilisha mgawo wa mauzo hayo kwenye wilaya, kata na matawini hata kwenye oparesheni M4C yuko busy kuuza kadi.
  5. Anadaiwa kuwa na uelewa mdogo ambao hauendani ya kasi ya chama hiki kwa sasa.

Mtoa taarifa ambaye yupo kwenye msafara wa M4C mkoani Morogoro anaeleza kuwa M/kiti huyo wa mkoa anahaha ni namna gani amwingie Dr. Slaa ili amshawishi azipe pengo tu la katibu wake aliyejiuzuru.

Tayari kuna vijana wasome wanahaha kuziwania nafasi hizo za ngazi ya mkoa na tayari wanapiga kampeni za chinichini.
 
Huyu hata mimi huwa nina wasiwasi naye sana
  1. Ni mkurupukaji hata Bungeni
  2. Ana jazba sana
  3. Anaonekana msanii
Huyu inabidi aondolewe tupewee Baraba!
 
kama haendani na kasi ya 3g bora achie ngazi kuliko kusubiri kuenguliwa na chama
 
Kama ni uchafu utoke kwenye chama chetu. Hatulei maradhi sisi. Tunataka watu wasafi na wenye uchungu na maendeleo na watakaoleta mabadiliko ya kweli sio kujaza matumbo yao.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Safi sana wanaMorogoro kama mtu hafai pigeni chini wekeni atakaye wafaa na kusaidia chama kwenye ukombozi mambo ya kuleana waachieni CCM
 
Mh! Kumbe huyu mama ni analog bado, chadema na digital so haendani na kasi na ufanisi
 
Mtoa taarifa aliyepo Morogoro ambaye juzi alinijuza kuwepo taarifa ya kujiuzulu katibu wa mkoa huo na mie kuitoa kama tetesi JF na baadae kuthibitika. Sasa amenijulisha kuwepo mpango wa kumng'oa Mh. Suzana Kiwanga (MB viti maalumu) kwenye nafasi ya Mkoa wa Morogoro. Wajumbe kutoka wilaya za mkoa huo watakutana Sept 03 mwaka huu kupanga safu ya uongozi ngazi ya mkoa chini ya usimamizi wa Dr. Slaa ili kuimarisha uongozi mkoani hapo ili moto uliowashwa na M4C usipoe mpaka 2015. Wajumbe wa wilaya za Kilombero na Manispaa ya Morogoro wanadaiwa kuwashawishi wajumbe toka wilaya nyingine ili wamtose M/kiti huyo.
Tuhuma zinazoelekezwa kwake ni pamoja na;

  1. Anaendesha chama mkoa kwa simu kwani makazi yake ni Kinondoni DSM na huonekana Morogoro tu kama kuna ugeni wa Kitaifa au vikao vya chama.Na kukwamisha shughuli za chama za kila siku.
  2. Siyo mtu wa kujitoa kwa mali kukijenga chama pamoja na kupata ubunge. Kwa mfano;Mkoa hauna ofisi hata M4C imewalazimu kazi zao kupanga Mt. Uluguru Hotel. Mkoa na wialaya wamepanga kachumba kadogo mno tena kachumba kalikotengenezwa na wanachama wa kawaida.Hajaleta gari yake hata moja kwenye oparesheni inayoendelea, hata yeye anadadia gari ya Dr. Slaa.
  3. Anadaiwa kuwa mwanasiasa za kutengeneza makundi kwenye chama, anatuhumiwa kuvuruga uongozi wa chama wilaya ya Kilombero enzi za uhai wa Marehemu Regia Mtema kipenzi cha wana Kilombero na sasa anavuruga mkoa mzima. Haoni ghalama anapotaka kumwangamiza mwenzake. Kwa mfano aliwahi kuwasafirisha wajumbe toka Kilombero wakati wa uhai wa marehemu Regia agenda ikiwa kutaka kuwatosa wajumbe wa kamati tendaji wilaya waliokuwa wakimuunga mkono marehemu.
  4. Anadaiwa amekwamisha kupatikana kadi za kutosha wilayani, kwenye kata mpaka matawini. Kwani anatuhumiwa kununua kadi sh 300/= zote zinazotengwa kwa mkoa wa Morogoro na kuanza kuziuza mwenyewe kwenye mikutano kwa sh. 1500/=bila kuwasilisha mgawo wa mauzo hayo kwenye wilaya, kata na matawini hata kwenye oparesheni M4C yuko busy kuuza kadi.
  5. Anadaiwa kuwa na uelewa mdogo ambao hauendani ya kasi ya chama hiki kwa sasa.

Mtoa taarifa ambaye yupo kwenye msafara wa M4C mkoani Morogoro anaeleza kuwa M/kiti huyo wa mkoa anahaha ni namna gani amwingie Dr. Slaa ili amshawishi azipe pengo tu la katibu wake aliyejiuzuru. Tayari kuna vijana wasome wanahaha kuziwania nafasi hizo za ngazi ya mkoa na tayari wanapiga kampeni za chinichini.

kama tuhuma ni za kweli atoswe tu tusilee wanafiki katika chama
 
Kadi ya sh 300 yeye anauza 1500 bado tu hamjakubali? Suzana ni jembe ulaya, umeweza kuifanya M4C ikuchangie na wewe.
 
Kadi ya sh 300 yeye anauza 1500 bado tu hamjakubali? Suzana ni jembe ulaya, umeweza kuifanya M4C ikuchangie na wewe.

vipi umepata moto.! Ninyi mnatishia sisi tunafanya kweli.!
 
vipi umepata moto.! Ninyi mnatishia sisi tunafanya kweli.!

Nakubaliana na wewe mkuu, wengi wa hao VYASAKA ni wafuasi wa kundi la Zitto inabidi washughulikiwe mapema kabla mambo hayajaharibika meku.
 
Kama haendani na kasi hii na kama tuhuma zikithibitika pasi shaka basi akae pembeni ili wengine wafanye kazi na yeye ajifunze!

Tukumbuke chadema ni chama makini!
 
Nakubaliana na wewe mkuu, wengi wa hao VYASAKA ni wafuasi wa kundi la Zitto inabidi washughulikiwe mapema kabla mambo hayajaharibika meku.

kwa hiyo zitto ndio anawatuma kuendesha chama kisanii.?
 
Back
Top Bottom