M/kiti ccm taifa kukigawa rasmi chama baada ya sherehe za uhuru wa Tanganyika!!

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Dec 22, 2010
16,987
20,271
Hali inayoendelea ndani ya ccm ni balaa tu! Mapacha wa tatu wamemkalia kooni m/kiti wa chama pamoja na mdomo wake uitwao Nape!Uchunguzi binafsi nilioufanya toka ndani ya ccm unabainisha kuwa sasa chama kimeshikiliwa kwa dhana ya sherhe za uhuru tu! Baadhi ya watu muhimu ndani ya ccm wanadiriki kusema ndio maana m/kiti anaona kiti cha moto pale magogoni! Wadau hao wanasema juhudi zote za kuumaliza upinzani zimegonga mwamba sasa hivi kilichobaki ni huruma ya watz tu kwani ndani ya chama watu wanaishi kwa matumaini tu!Hii tafsi yake nini wana jf?
 
naam! uchunguzi wako binafsi naona una kaukweli kiasi kikubwa sana. ngoja waweseke, hakuna utawala usiokuwa na mwisho.
 
Zinasubiriwa siku tisini au 120 toka walipojivua gamba!
 
m/iti ccm amesha kigawa chama chake siku nyingi hata kabla ya hizo sherehe za uhuru.mgawanyiko huo ulianza tangu kipindi cha taasisi ya mwalimu nyerere kilipo mtaka afanye maamuzi magumu ya kuwashughulikia mafisadi ndani ya chama na serikali yake.tangia hapo kumekuwa na mgawanyiko wa ndani,nje,wa siri na hadharani.walioko katika kundi lake ni kwa sababu ya kulinda masilahi yao lakini ukweli hawako ndani ya ccm.
 
mkuu niko nawe. ila naongeza tu kuwa sidhani kama kuna mtu wa kweli aliye bado ndani ya ccm. nasema hivi kwa sababu ccm halisi kwa sasa haipo. iliyopo ni dhana ya ccm lakini kama chama halisi hakipo. tukionacho sio chama cha kisiasa bali chama kama kinavyotambuliwa kisheria. maslahi ya pamoja ya wanachama, ukiacha kuendelea kuwa na madaraka, hakuna kingine. na pande zote zilizopo zingependa ccm iendelee kubaki madarakani, hata kama ni upande mwingine utakaokuwa madarakani. sababu kuu ni kulinda maslahi yao...tena ya binafsi na wala si ya chama au nchi. ndio maana wapo waliochangia kuwa pamoja na midahalo yao inayoendelea, watakuja ungana kwenye general elections. hii ni kweli kwani bila hivyo ccm iking'olewa, wote wamekwisha.
 
Back
Top Bottom