Lyatonga Mrema: CCM wamenichezea rafu Uchaguzi Serikali za Mitaa, aonya

cutelove

JF-Expert Member
Oct 3, 2017
3,317
7,509
Mwenyekiti wa TLP amesema CCM na wasimamizi wa serikali za mitaa wamemchezea rafu, anasema mfano Moshi, mawakala wa chama chake wameondolewa kwenye vituo vya kupigia kura.

Ameonya kama hali ndo hii, kuna uwezekano wa kutokea machafuko huko mbeleni.
****




Wakati uchaguzi wa serikali za mitaa ukiendekea katika kijiji cha Kiraracha, jimbo la Vunjo mkoani Kilimanjaro, mwenyekiti wa TLP, Agustino Lyatonga Mrema, amelalamika kufanyiwa hujuma na baadhi ya mawakala wake kuondolewa kwenye vituo.

Mrema ameyasema hayo leo wakati akizungumza kuhusu uchaguzi huo, ambapo amesema hatendewi haki licha ya kuwa na kijiji kimoja pekee.

Mrema ambaye anashiriki katika uchaguzi kwenye kijiji cha Kiraracha pekee ambako ndiko anakoishi, akichuana na CCM, amedai kuwa aliamua kushiriki uchaguzi huo ili kumsaidia Rais John Magufuli lakini hajatendewa haki.

"Hali ni mbaya, kwani mimi nilikuja kushiriki uchaguzi huu kwa nia njema kumsaidia Rais wangu kwa sababu walitaka kuonyesha kuwa hakuna utawala bora, watu walisusa na kugoma, mimi nikasema ingawa sina halmashauri nibaki na kijiji hiki kimoja."

Aliongeza, “nilisema ushindani uwe kwenye sanduku la kura, lakini haikutokea hivyo, magari yote ya serikali ya Moshi yamehamia Kiraracha, kuna mawakala wangu wametolewa kwenye vituo, hali ikiwa hivi nchi itaharibika."

Akizungumzia malalamiko hayo, msimamizu wa uchaguzi Moshi Vijijini, Juma Tukosa, amesema hali inakwenda vizuri na wakala anayemlalamikia Mrema, alikuwa anakunywa pombe katika eneo la kituo na kuambiwa aziondoe, ndipo alipoanza kulalamika anaondolewa kituoni.

"Hakuna wakala aliyeondolewa, ila katika kituo kimoja wakala wa TLP, alikuwa na bia tatu ndani ya kituo, alipoambiwa aziondie bia hizo, akaanza kulalamika anaondolewa lakini hajaondolewa bado yupo kituoni," amesema Tukosa.
 
Hivi huyu Mrema si ndiyo alisema kwenye kikao chao cha Halmashayri kuu ya TLP wamekubaliana kupitisha jina la John Magufuli kutoka chama cha CCM kuwa ndiyo mgombea,wao kwenye uchaguzi mkuu mwaka 2020??

Huyo sasa amejigeuza kutoka mwanasiasa na kuwa comedian!
 
Mwenyekiti wa TLP amesema CCM na wasimamizi wa serikali za mitaa wamemchezea rafu, anasema mfano Moshi, mawakala wa chama chake wameondolewa kwenye vituo vya kupigia kura.

Ameonya kama hali ndo hii, kuna uwezekano wa kutokea machafuko huko mbeleni.

Source: Mwananchi

Huu uzi unajaza sever yetu bila sababu, hamishieni facebook
 
Pole Mrema,wenzako waliona mbali
IMG_20191124_185354.jpeg
 
Back
Top Bottom