Lyatonga Mrema anajuta kujiuzuru uwaziri au anafanya kazi ya UWT? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lyatonga Mrema anajuta kujiuzuru uwaziri au anafanya kazi ya UWT?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Watanzania, Mar 22, 2010.

 1. W

  Watanzania JF-Expert Member

  #1
  Mar 22, 2010
  Joined: Jul 7, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Ninajiuliza kila siku, hasa baada ya mwenendo wa Mrema kutokueleweka kisiasa.

  Kuanzia pale alipoamua kuwa upande wa CCM wakati wa Msiba wa Marehemu Chacha Wangwe, na kuwa kinyume na Chadema amekuwa haeleweki. Sasa hivi yeye yuko ‘bize' kuwaponda wenzake wa vyama vya upinzani. Kitu ambacho sielewi ni; Mrema anajuta kujiuzuru uwaziri wa mambo ya ndani na kujiengua CCM au anaendelea kufanya kazi yake ambayo yasemekana ni usalama wa taifa?
   
 2. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #2
  Mar 22, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,171
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Huyu amepauka kisiasa na kiuchumi pia. Hana jipya, anatumia utu uzima tu kuishi hapa mjini.
   
 3. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #3
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Nimewahi kusikia kuwa alipata ajali mbaya ikaathiri ubongo wake.
  Hebu ngoja nitoke nje nikaangalie leo kuna mwezi gani, maana nasikia wenzetu hawa hawashikiki mwezi ukiwa mchanga
   
 4. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #4
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  CHADEMA kwa matusi na propaganda mmezidi; sijui mkipata madaraka itakuwaje?

  Huyo Mrema japo ana record nzuri ya utendaji na ndio maana kuna Watanzania tutaendelea kumwunga mkono.

  Mnapoteza muda bure kupambana na Mrema ambaye atashinda Vunjo mtake msitake. Pelekeni mapambano yenu kwa hao mafisadi CCM na sio kuamua kumchafua Mrema kwasababu tu hakubaliani na nyie CHADEMA.
   
 5. Sumbalawinyo

  Sumbalawinyo JF-Expert Member

  #5
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 22, 2009
  Messages: 1,286
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  Chadema=chama cha wachagga
  mrema naye mchagga..
  Sasa vita vya nini nyie wanandugu?
   
 6. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #6
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Hao Wachaga ni opportunists, Mrema alipokuwa maarufu mwaka 1995 wote walikimbilia kwake na kuitema CCM. Sasa wanaona amefulia wanamkimbia kama ukoma.

  Baada ya kuona CHADEMA inakuja juu wote wamekimbilia huko, ikifulia watarudi CCM haraka kuwahi ulaji.

  Hawana msimamao hao, wanafuata ulaji tu.
   
 7. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #7
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Acha fikra potofu wewe!! kwa hiyo waliompa ubunge Zitto kigoma ni wachagga? Dr. slaa karatu? Tarime?
   
 8. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #8
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  akili fupi daima hupenda kujadili na kuunga mkono upuuzi na tetesi ambazo hazina mashiko.
   
 9. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #9
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  sijua hata kama hodi alipiga huyu!!
   
 10. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #10
  Mar 23, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  umakini ni kitu muhimu sana usomapo thread za watu kabla ya kuchangia
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Mar 23, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Huko aliko pia anaendelea na ajira yake maalum kuhakikisha upinzani unakosa mwelekeo.
   
 12. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #12
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Akili fupi pia hupenda kuwajadili wenye akili fupi. Werevu wamesoma na kudharau, wenye akili fupi wamekimbilia kwenye mipasho.
   
 13. nzalendo

  nzalendo JF-Expert Member

  #13
  Mar 23, 2010
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,875
  Likes Received: 2,683
  Trophy Points: 280
  Nchi yetu mzuri uwe chadema ccm au usiwe na chama yote pouwah kwa mtazamo wangu vyama havina ishuuu .....
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280

  Heshima kwako Muheza2007,

  Nipojiunga na JF mwanzoni nilidhani inamilikiwa na CHADEMA ambao wako hapo kutetea jambo lolote hata kama halina mantiki,napata faraja watu kama wewe kutambua mapema hila na ghiliba za baadhi ya wachangiaji kutaka kuifanya JF ipo kwaaajili ya kutetea propaganda za CHADEMA.
   
 15. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #15
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Ngongo,

  Kuna watu hapa kazi yao kusema CCM wote ni Mafisadi, hapo wana maana hata mama Nyerere ni Fisadi. Ukiwageuzia kibao kwa makusudi na kuwaambia CHADEMA ni ya Wachaga, wanaanza kutukana eti Mbona kuna Zitto. Kama mnaona kuna Zitto ambaye sio Mchaga basi hata CCM kuna watu kama mama Nyerere ambao ni wasafi. Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu uchungu.
   
 16. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #16
  Mar 23, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  leta analysis za kisomi kwanini CHADEMA ndio wanaomshambulia Mrema, A.L NIJUACHO NA AMBACHO NI REALITY Mrema si tishio kwa Mpinzani yoyote, ni mtu ambae jamii yoote kwa ujumla imeelewa rangi zake halisi........
  labda anabifu na Mzee Sitta.
  CHADEMA walimkataa Mrema akiwa juu baada ya kutoka CCM, ITAKUWAJE LEO WAANZE KUINGIA NAE VITANE.
  watu wenye mind duni huyaangalia haya mambo kwa fikra fupi vivyo hivyo
   
 17. m

  muheza2007 JF-Expert Member

  #17
  Mar 23, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 233
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  Mkuu,

  Naona umegundua makosa yako ya mwanzoni na sasa kuamua kujadili issue. Hapo tunaweza kujadiliana. Mimi nilikuwa nawapima CHADEMA kwa kuwarushia kijembe kama wanavyofanya kwa CCM ili nione je wataepuka matusi?

  Sikukosea maana kweli mkakimbilia kwenye matusi na kuniita nina akili fupi. Hapo research yangu imekamilika.

  Vipi CCM wote ni mafisadi?
   
 18. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #18
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Sijui unategemea jibu la aina gani kwa swali la aina hiyo? Lakini kwa kifupi tu ni kwamba mtu yeyote anayeshabikia CCM kama ilivyo hivi sasa na kuona kwamba kila kitu ni shwari ndani ya chama hicho basi huyo ni FISADI kwa maana yake halisi! Ama, ana matarajio/ndoto za kifisadi. Tuache unafiki, CCM hivi sasa inaendeshwa kifisadi na inahitaji mapinduzi makubwa sana kuirejesha kwenye misingi yake ya maadili. Mrema anajua vizuri sana hilo.

  Msitake kupoteza lengo kwa kufanya ni suala la ulinganisho na CHADEMA au chama chochote cha upinzani. CCM ni chama tawala kinachodhibiti hazina yetu yote (inaelekea sasa hata namna tunavyofikiri).

  Kuna mtu hapa kauliza ikiwa na Mama Maria Nyerere naye ni fisadi. Huko ni kupotea hoja. Akamuulize kwanza kama Mama ana raha na hicho chama kama kilivyo hivi sasa. Mmeshasikia maoni ya wana-CCM wengine walioamua kuweka kando unafiki.
   
 19. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #19
  Mar 23, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 670
  Trophy Points: 280
  Rekodi nzuri basi iambatane na uwezo wa kufikiri; uwezo wa kimkakati. Huwezi kusikia kauli za sasa za Mrema ukapata faraja kuwa huyu ni mtu timamu achilia mbali kuwa kiongozi wa maana. Hata hao anaowapigia chapuo bila shaka pembeni wanabakia kumshangaa na kumsikitikia tu. Na akirogwa arudi CCM watamweka uwani na kumsahau moja kwa moja. He is, simply, embarassing!
   
 20. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #20
  Mar 23, 2010
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Jifunze tofauti ya ' wachaga wengi ni chadema na chadema wengi ni wachaga' then soma message ya jamaa unaweza kuilewa vizuri, utaona mifano uliyoitoa ni sahihi lakini haina uhusiano.
   
Loading...