Lwandamina na falsafa za Barcelona "Yanga SC".

demigod

JF-Expert Member
Jan 2, 2015
8,250
15,116
KOCHA Mkuu mpya Yanga, George Lwandamina taratibu ameanza mipango ya kuisuka timu yake mpya, haraka mambo matatu muhimu yameanza kuchomoza, huku baadhi ya mastaa wakikumbana na moto wake kwenye kukumbushana majukumu ya kazi.

Tangu aanze mazoezi, Lwandamina ameonyesha kikosi chake kitakuwa cha soka la haraka akipambana kuhakikisha kila mchezaji hapotezi muda kwa kukaa na mpira kwa sekunde tatu bila sababu za msingi.

Mzambia huyo amekuwa akiwataka wachezaji kupiga pasi za haraka zinazofika na kutoa pasi kwa mtindo wa gusa achia. Sasa ole wake mchezaji atembee baada ya kuachia pasi, atakumbana na balaa la kocha huyo Mzambia aliyetokea Zesco FC. Katika mazoezi hayo amekuwa akitaka kila anayetoa pasi haraka anafungua nafasi nyingine ya kupewa pasi nyingine ili kurahisisha mashambulizi ya haraka na pia kumpa chaguo la kutosha kwa mtu mwenye mpira. Alionekana kuwa mkali kwa kutoa adhabu kwa walioonekana kushindwa kufanya alichotaka kifanyike hasa kupoteza mpira. Jukumu lingine la tatu ambalo Lwandamina ametaka lifanyike ni kukaba kwa haraka mara baada ya mpira kupotea ambapo endapo timu pinzani itapata bao na likatokea kufungwa kupitia uzembe wa nafasi yako katika kukaba basi utakutana na adhabu kali.

Aliwapa adhabu za kukumbushana Juma Abdul, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haruna Niyonzima na Andrew ‘Dante’ walioonekana kuzembea katika kukaba na kutoa pasi za uhakika.

Walipewa adhabu kuzunguka eneo la uwanja walilokuwa wakilichezea na hata kwa adhabu hiyo aliwataka kukimbia haraka na ukichelewa kukamilisha mzunguko huo na timu yako ikafungwa ukiwa nje adhabu inaongezeka mara moja.

Akizungumzia mazoezi hayo Lwandamina alisema anataka kuona kikosi chake kikicheza soka la haraka na pasi za uhakika ambapo hayo yote anataka yawe katika akili za wachezaji wake.

Alisema anataka kuona Yanga inacheza soka la kwenda mbele kwa kupiga pasi za haraka na katika ukabaji pia kila mchezaji akishiriki lakini pia akipiga marufuku pasi za kurudi nyuma bila ya sababu za msingi.

“Ili ushinde unahitaji kutambua ni wapi unatakiwa upeleke mpira wa haraka na pia kuhakikisha unafungua nafasi kurahisisha uliyempa afanye vipi, sasa katika hilo lazima muda uzingatiwe ndiyo maana nimekuwa sitaki kuona mchezaji akichelewa kwa kukaa sana na mpira,”alisema.

“Tunatakiwa pia kukaba kwa pamoja pale mpira unapopotea na hili la kukaba hakuna mwenye msamaha lakini pia nisingependa kuona pasi za kurudi nyuma zinakuwa ni kama tabia.”
 
kwa wachezaji gani hapa Tanzania? hawa hawa wa chai maharage, pilau ya njegere, chips za mafuta ya transforma? au wengine?
 
Hyo ndio yanga mpya mikia mtaisoma namba ndo mana mmeanza kutafta visingizio mapema maana mshaanza kupoteana aliyekua anawapa jeuri ameona mnamzingua kaachana na mpango
 
KOCHA Mkuu mpya Yanga, George Lwandamina taratibu ameanza mipango ya kuisuka timu yake mpya, haraka mambo matatu muhimu yameanza kuchomoza, huku baadhi ya mastaa wakikumbana na moto wake kwenye kukumbushana majukumu ya kazi.

Tangu aanze mazoezi, Lwandamina ameonyesha kikosi chake kitakuwa cha soka la haraka akipambana kuhakikisha kila mchezaji hapotezi muda kwa kukaa na mpira kwa sekunde tatu bila sababu za msingi.

Mzambia huyo amekuwa akiwataka wachezaji kupiga pasi za haraka zinazofika na kutoa pasi kwa mtindo wa gusa achia. Sasa ole wake mchezaji atembee baada ya kuachia pasi, atakumbana na balaa la kocha huyo Mzambia aliyetokea Zesco FC. Katika mazoezi hayo amekuwa akitaka kila anayetoa pasi haraka anafungua nafasi nyingine ya kupewa pasi nyingine ili kurahisisha mashambulizi ya haraka na pia kumpa chaguo la kutosha kwa mtu mwenye mpira. Alionekana kuwa mkali kwa kutoa adhabu kwa walioonekana kushindwa kufanya alichotaka kifanyike hasa kupoteza mpira. Jukumu lingine la tatu ambalo Lwandamina ametaka lifanyike ni kukaba kwa haraka mara baada ya mpira kupotea ambapo endapo timu pinzani itapata bao na likatokea kufungwa kupitia uzembe wa nafasi yako katika kukaba basi utakutana na adhabu kali.

Aliwapa adhabu za kukumbushana Juma Abdul, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Haruna Niyonzima na Andrew ‘Dante’ walioonekana kuzembea katika kukaba na kutoa pasi za uhakika.

Walipewa adhabu kuzunguka eneo la uwanja walilokuwa wakilichezea na hata kwa adhabu hiyo aliwataka kukimbia haraka na ukichelewa kukamilisha mzunguko huo na timu yako ikafungwa ukiwa nje adhabu inaongezeka mara moja.

Akizungumzia mazoezi hayo Lwandamina alisema anataka kuona kikosi chake kikicheza soka la haraka na pasi za uhakika ambapo hayo yote anataka yawe katika akili za wachezaji wake.

Alisema anataka kuona Yanga inacheza soka la kwenda mbele kwa kupiga pasi za haraka na katika ukabaji pia kila mchezaji akishiriki lakini pia akipiga marufuku pasi za kurudi nyuma bila ya sababu za msingi.

“Ili ushinde unahitaji kutambua ni wapi unatakiwa upeleke mpira wa haraka na pia kuhakikisha unafungua nafasi kurahisisha uliyempa afanye vipi, sasa katika hilo lazima muda uzingatiwe ndiyo maana nimekuwa sitaki kuona mchezaji akichelewa kwa kukaa sana na mpira,”alisema.

“Tunatakiwa pia kukaba kwa pamoja pale mpira unapopotea na hili la kukaba hakuna mwenye msamaha lakini pia nisingependa kuona pasi za kurudi nyuma zinakuwa ni kama tabia.”
Weka kabisa ulipotoa habari:: MWANASPOTI
ili kila mtu ajue sio mawazo yako
 
Jamaa fundi mpira wa kisaaa unahitaji kasi kubwa... Yeye anaangalia jinsi ya kuwafunga Zesco. Zamalek. Mamelod sio mikia
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom