Lwakatare vituko vitupu: Polisi wasaka maandiko yake ofisi za CHADEMA, Salva amtetea Michuzi

Si wawakamate wote wanaopongezana ili kupata ukweli, nchi hii kweli inadouble standard, nakumbuka enzi za mwalimu wote hawa wangekuwa kiti moto!
 
Mkuu Maboso, the burden of proof lies with the prosecution, the same applies to allegations, anae prove ni alie allege in case hii subject matter ya video, mimi nimeoiona kwa naked ayes tuu kuwa video ile ni "bonafine genuine", hivyo wenye jukumu la ku proove kuwa imekuwa doctored ni hao wanaoamini ni ya kughushi.

NB. Video kuwa "bonafide genuine" ni jambo moja, kufikishwa kwa Rwakatare mahakamani ni jambo jingine!, admissibility ya e-evidence kwa video hiyo kukubalika kama ushahidi ni jambo jingine, na Rwakatare kuwa na kesi ya kujibu nalo ni jingine tena!, hoja kubwa ya msingi iliyopo hivi sasa ni "jee Rwakatare was "a solo" artist au hiyo single ni ya "bendi?!". Kama ni solo, kesho mtamshuhudia mahakamani, kama sio single yake bali ya bendi!, hapo sasa ndipo kazi ilipo!.

Pasco.

mike, mike, hapoo.kauli zinazosikika mwanzoni mwa video inayoitwa bonafide genuine sijui walikuwa wanajaribisha nini? pasco walikuwa wanapiga picha ya harusi au ndiyo secrete camera zilivyo?
 
JK ameleta maafa sana hapa Tz na ameinajisi sana nchi yetu lakini kama kweli Mungu yupo basi na tuzidi kusali na kuomba
 
Acha uvivu wa kufikiri unadhani teknolojia ni bure hadi iwekwe humu jamvini? Una shingapi mi nikuuzie hiyo teknolojia?
 
Ok,kiufupi Salva amekanusha suala la Ikulu kuhusika na utekaji na kuua raia,akioanisha kwa
kitendo cha rais kumtembelea Kibanda'

Ila anakubaliana kuwa ikulu inahusika na email hizo kwa kushare wao kwa wao kama watumishi,
kosa ni wale walioingilia mawasiliano hayo na kuleta email JF!!!

Na anakubaliana juu ya Michuzi kwapongeza maafisa wa TISS.

Na anakubaliana kuwa watanzania wanposikitishwa na suala hili la video ya Lwakatare yeye
michuzi anafurahia na kuwapongeza waliofanikisha hilo.

Rweyemamu anataka kutuaminisha nini watanzania kuhusu ikulu yetu,je inatumiwa kwa maslahi
ya akina michuzi na ccm ili kukandamiza raia wake kwa maslahi binafsi!!!!
 
Sakata hili la Kibanda na Lwakatare litaisha kwa gazeti la Tanzania Daima kufungiwa. Mtakumbuka jinsi sakata la Ulimboka lilivyoondoka na MwanaHalisi. Hii ndio Bongo
 
We Pimbi kweli,
Salva alioko Ikulu mwenyewe anaikubali ile email ni halisi, wewe huku nje unadai imepikwa.

Wewe simbilisi vipi mbona unatoa povu, au umebanwa na mlango? Huyo Salva anaongea na Tanzania daima peke yake?
 
Kutrace source ya email ni kazi rahisi sana kwangu. Kuna thread ilikuja na hayo mawasiliano ya emails nikamuomba muhusika wa hiyo post anipatia baadhi ya vitu ili nitrace na wanajukwaa wote tuujue ukweli lakini jamaa akatokomea. Hii inanipa wasiwasi kuwa huenda hizo emails zilisukwa ili kuaminisha watu kuwa ile video ulikuwa mpango wa TISS.

Nimeona hata katika michango ya ile video watu wametoa maoni mbalimbali ikiwemo technology za kung'amua uhalisia wa ile video. Lakini hakuna hata mmoja ambaye kajitolea kutumia hizo technology ili kutupa ukweli wanajukwaa.

Ninaamini kuwa humu ndani hakuwezi kukosa wataalam. Sasa kukaa kimya kunanifanya niamini ile video ni ya ukweli kabisa.

ndiyo ni member mwenzetu humu! Je tutajuaje kama ni mng'oa meno na kucha! Jamaa alipatia kukupotezea
 
Inasikitisha pale ambapo ofisi no. 1 inakuwa mtuhumiwa namba moja wa mateso ya raia wake. Inafika mahali matamko kutoka huko yanatolewa utafikiri mtu katoka usingizini akili yake bado haijakaa sawa (anaweweseka hivi)kama kumtembelea victim wa mateso ndio proof yakutohusika then leo msemaji wa ikulu, pamoja na ushahidi hapo chini, anatuongezea ushahidi kuthibitisha kuhusika kwa ikulu kwenye sakata la kuteswa kwa dr.

Facts: 1) rais hakuenda kumuona dr ulimboka (mtanisahihihisha)

2) mtu wa ikulu alitajwa na mhusika (dr) kwamba ndio aliye andaa mazingira ya yeye kutekwa
3) mpaka sasa polisi hawajamhoji dr wala mtuhumiwa wa ikulu (rama)
4) gazeti lililotoa utambulisho wa ofisa wa tiss limefungiwa (ili lisieendelee kutoa ukweli zaidi?!)
 
Kutrace source ya email ni kazi rahisi sana kwangu. Kuna thread ilikuja na hayo mawasiliano ya emails nikamuomba muhusika wa hiyo post anipatia baadhi ya vitu ili nitrace na wanajukwaa wote tuujue ukweli lakini jamaa akatokomea. Hii inanipa wasiwasi kuwa huenda hizo emails zilisukwa ili kuaminisha watu kuwa ile video ulikuwa mpango wa TISS.

Nimeona hata katika michango ya ile video watu wametoa maoni mbalimbali ikiwemo technology za kung'amua uhalisia wa ile video. Lakini hakuna hata mmoja ambaye kajitolea kutumia hizo technology ili kutupa ukweli wanajukwaa.

Ninaamini kuwa humu ndani hakuwezi kukosa wataalam. Sasa kukaa kimya kunanifanya niamini ile video ni ya ukweli kabisa.

Naona umejiunga leo leo kwa ajili ya kufanya utetezi. Ukweli ukidhihiri, uongo hujitenga. Unataka kutuaminisha kuwa yale mawasiliano ya imeili yalikuwa ya uongo? Unataka kuyafananisha na ile mail iliyokuwa forwarded kwa mtu halafu Mchange akadai ni mawasiliano baina yake na Saanane?
 
hapa ndipo napomkumbuka mzee wa tindi KALI a.k.a MWANA HALISI -kubenea MAANA anaweka mwanzo mwishoooo
 
Mkuu Maboso, the burden of proof lies with the prosecution, the same applies to allegations, anae prove ni alie allege in case hii subject matter ya video, mimi nimeoiona kwa naked ayes tuu kuwa video ile ni "bonafine genuine", hivyo wenye jukumu la ku proove kuwa imekuwa doctored ni hao wanaoamini ni ya kughushi.

NB. Video kuwa "bonafide genuine" ni jambo moja, kufikishwa kwa Rwakatare mahakamani ni jambo jingine!, admissibility ya e-evidence kwa video hiyo kukubalika kama ushahidi ni jambo jingine, na Rwakatare kuwa na kesi ya kujibu nalo ni jingine tena!, hoja kubwa ya msingi iliyopo hivi sasa ni "jee Rwakatare was "a solo" artist au hiyo single ni ya "bendi?!". Kama ni solo, kesho mtamshuhudia mahakamani, kama sio single yake bali ya bendi!, hapo sasa ndipo kazi ilipo!.

Pasco.

Pasco,ukiitazama kwa makini ile clip haina uhalisia kabisa.Ndio maana wanasheria wanasema kabla haujamhukumu mtu hakikisha beyond reasonable doubt mtu huyo ana hatia.Ukiangalia kuna watu wanaongea,kuna binti amepita,hivi maongezi sensitive kama hayo yanaweza kufanyika kwenye mazingira kama hayo,yasiyo na utulivu?Hivi huyu binti hawezi kuitwa akaulizwa?Inaelekea Lwakatare alikuwa anaongea na watu wengine, je mbona kwenye hii clip wanatajwa majina tu na sura zao hazipo,hivi Lwakatere hana familia akijua anayoyatenda yataathiri familia yake pia?Ukijiuliza maswali haya utapata uhakika kuwa clip hiyo ni mchezo mchafu uliochezwa naomba niwaite wahuni,wasilitakiwa taifa letu mema.

Ukitafakari kwa umakini bila kuweka UCHADEMA au UCCM,tuweke haki na Utanzania kwanza hii clip siyo ya kweli na aliyetenda hayo polisi walistahili kumtafuta kwanza huyo kabla ya Lwakatare.Ninahofia mwisho wa siku serikali yetu italipa pesa nyingi za kumharibia mtu jina lake,na hii itakuwa imekula kwetu watanzania walipa kodi kwa ujinga,ukosefu wa weredi na kutumia madaraka au nafasi walizonazo kwa watu tuliowapa madaraka.Inasikitisha sana,siyo hiyo tu bali si uungwana,dini zote zinakataa haya.
 
WAKATI afya ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, ikiendelea vizuri, daktari wa serikali aliyefika polisi kumwangalia anadaiwa kukwepa kumpatia matibabu.

Hatua hiyo ilimlazimu Lwakatare kupatiwa matibabu na kaka yake ambaye ni daktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

Lwakatare ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na hivyo kuhitaji uangalizi wa karibu, alikamatwa na Jeshi la Polisi Jumatano ya wiki iliyopita baada ya kuonekana katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii akidaiwa kupanga mikakati ya kudhuru baadhi ya watu.

Chanzo chetu kilisema kuwa daktari huyo wa serikali alifika polisi Kanda Maalumu ya Dar es Saalam juzi kwa ajili ya kumwangalia Lwakatare, baada ya baadhi ya magazeti kuripoti afya yake kudhoofu.

Kwamba alimwangalia Lwakatare na kuahidi kuwa anaenda na angerudi baadaye kumletea dawa lakini hadi jana alikuwa hajarudi, hatua iliyoifanya familia ya Lwakatare kumwita ndugu yao, Dk. Lwakatare ampatie matibabu.

"Hali yake kwa sasa kwa kweli ni nafuu, kaka yake alimletea dawa," kilisema chanzo chetu.

Akizungumza kwa simu wakili wa Lwakatare, Nyaronyo Kicheere alisema kuwa mteja wake anaendelea vema sasa.

Aliongeza kuwa jana polisi walikwenda makao makuu ya ofisi za CHADEMA kutafuta karatasi zozote ambazo mteja wake aliwahi kuandika kwa mkono ikiwa ni sehemu ya kuendelea na upelelezi.

Alisema kuwa maofisa wa polisi walikwenda makao makuu ya CHADEMA wakiwa na Lwakatare pamoja na yeye mwenyewe kuchukua sampuli za karatasi zenye mwandiko wa Lwakatare.

Hata hivyo, jambo hilo lilifanyika bila kuwepo uongozi wa chama katika ofisi hizo kwani ilikuwa ni siku ya mapumziko.

Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu alisema ili kuingia kukagua eneo fulani, polisi wanahitajika kuwa na waranti ya kupekua.

Alisema kuwa waranti hiyo hutolewa na polisi au mahakama, na kwamba hata kama walikuwa nayo ilikuwa vizuri zaidi kama wangewataarifu wenye ofisi.

Kuhusu Lwakatare kufikishwa mahakamani leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso alisema kuwa upelelezi bado unaendelea, na kwamba huenda akafikishwa.

Alipoulizwa kwa simu ni kwanini hana uhakika na hilo, Senso alisema: "Nimekwambia huenda atapelekwa mahakamani."

Ikulu yaruka
Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti madai ya kunaswa mawasiliano ya siri ya ofisa mmoja wa Ikulu, akiwapongeza vijana walioandaa video ya Lwakatare na kwamba hiyo ni kete kubwa kwa CCM, ofisi hiyo imeibuka na kukanusha taarifa hizo.

Ikulu imesema kuwa ofisi ya Rais Jakaya Kikwete isibebeshwe msalaba wa watu wengine kwani haiwezi kuhusika kwa namna yoyote kuteka, kuua au kuwashambulia raia wake.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu wakati akizungumzia tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.

Rweyemamu alitoa ufafanuzi huo akijibu taarifa ya gazeti hili juzi iliyonasa na kuchapisha mawasiliano ya ofisa mmoja wa Ikulu akipongeza kazi ya Idara ya Usalama iliyofanikiwa kuandaa video ya Lwakatare.

Salva alisema Ikulu kamwe haiwezi kuhusika na vitendo vya kuteka raia wake kwani jukumu lake ni kulinda haki za raia wake wote.

"Ikulu haiwezi kuhusika na mambo ya kijinga kama haya. Inachokifanya ni kuhakikisha inawasaka wahusika ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na ndiyo maana hata Rais Kikwete alimtembelea Kibanda kule Afrika Kusini alikolazwa," alisema Salva.

Alisema anamfahamu Kibanda, ameumizwa na jinsi alivyovamiwa na kupigwa na kusababishiwa maumivu na majeraha ya kudumu.

"Kibanda ni mdogo wangu, mimi ndiye niliyempokea na kumfundisha kazi, siwezi kufurahia alichofanyiwa," alisema.

Kuhusu mawasiliano ya ofisa wa Ikulu, Salva alimtaja afisa huyo kuwa ni Muhidin Michuzi ambaye ni mmoja wa wapiga picha wa rais.

Akifafanua kuhusu mawasiliano hayo ya Michuzi, Salva alisema haikuanzia kwake kwani naye alitumiwa na mtu mwingine.

"Yale mawasiliano hayakuanzia kwa Michuzi. Yeye alitumiwa tu, alichokifanya ni ku-‘share' ile taarifa na watumishi wengine wa Ikulu. Hapa kosa lake nini?" alihoji Salva.

Hata hivyo, Salva alitahadharisha kwamba ni kosa kisheria kwa mtu yoyote kuingilia mawasiliano ya mtu na kuyaweka hadharani.

Alivitaka vyombo vya habari kuviachia vyombo vya dola kuchunguza tukio la kushambuliwa kwa Kibanda badala ya kuandika habari za mitaani.


CHANZO: Tanzania Daima online la tarehe 18/03/2013.
Salva hawezi kujua yanayotendwa na akina IGHONDU na manyang'au mengine yanayokalia taasisi inayoitwa TISS!
 
Back
Top Bottom