Lwakatare vituko vitupu: Polisi wasaka maandiko yake ofisi za CHADEMA, Salva amtetea Michuzi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lwakatare vituko vitupu: Polisi wasaka maandiko yake ofisi za CHADEMA, Salva amtetea Michuzi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Salary Slip, Mar 17, 2013.

 1. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 44,884
  Trophy Points: 280
  WAKATI afya ya Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, ikiendelea vizuri, daktari wa serikali aliyefika polisi kumwangalia anadaiwa kukwepa kumpatia matibabu.

  Hatua hiyo ilimlazimu Lwakatare kupatiwa matibabu na kaka yake ambaye ni daktari katika Hospitali ya Taifa Muhimbili.

  Lwakatare ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari na hivyo kuhitaji uangalizi wa karibu, alikamatwa na Jeshi la Polisi Jumatano ya wiki iliyopita baada ya kuonekana katika video iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii akidaiwa kupanga mikakati ya kudhuru baadhi ya watu.

  Chanzo chetu kilisema kuwa daktari huyo wa serikali alifika polisi Kanda Maalumu ya Dar es Saalam juzi kwa ajili ya kumwangalia Lwakatare, baada ya baadhi ya magazeti kuripoti afya yake kudhoofu.

  Kwamba alimwangalia Lwakatare na kuahidi kuwa anaenda na angerudi baadaye kumletea dawa lakini hadi jana alikuwa hajarudi, hatua iliyoifanya familia ya Lwakatare kumwita ndugu yao, Dk. Lwakatare ampatie matibabu.

  "Hali yake kwa sasa kwa kweli ni nafuu, kaka yake alimletea dawa," kilisema chanzo chetu.

  Akizungumza kwa simu wakili wa Lwakatare, Nyaronyo Kicheere alisema kuwa mteja wake anaendelea vema sasa.

  Aliongeza kuwa jana polisi walikwenda makao makuu ya ofisi za CHADEMA kutafuta karatasi zozote ambazo mteja wake aliwahi kuandika kwa mkono ikiwa ni sehemu ya kuendelea na upelelezi.

  Alisema kuwa maofisa wa polisi walikwenda makao makuu ya CHADEMA wakiwa na Lwakatare pamoja na yeye mwenyewe kuchukua sampuli za karatasi zenye mwandiko wa Lwakatare.

  Hata hivyo, jambo hilo lilifanyika bila kuwepo uongozi wa chama katika ofisi hizo kwani ilikuwa ni siku ya mapumziko.

  Akizungumza na gazeti hili kwa simu, Mkurugenzi wa Sheria na Katiba wa CHADEMA, Tundu Lissu alisema ili kuingia kukagua eneo fulani, polisi wanahitajika kuwa na waranti ya kupekua.

  Alisema kuwa waranti hiyo hutolewa na polisi au mahakama, na kwamba hata kama walikuwa nayo ilikuwa vizuri zaidi kama wangewataarifu wenye ofisi.

  Kuhusu Lwakatare kufikishwa mahakamani leo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Advera Senso alisema kuwa upelelezi bado unaendelea, na kwamba huenda akafikishwa.

  Alipoulizwa kwa simu ni kwanini hana uhakika na hilo, Senso alisema: "Nimekwambia huenda atapelekwa mahakamani."

  Ikulu yaruka
  Siku moja baada ya gazeti hili kuripoti madai ya kunaswa mawasiliano ya siri ya ofisa mmoja wa Ikulu, akiwapongeza vijana walioandaa video ya Lwakatare na kwamba hiyo ni kete kubwa kwa CCM, ofisi hiyo imeibuka na kukanusha taarifa hizo.

  Ikulu imesema kuwa ofisi ya Rais Jakaya Kikwete isibebeshwe msalaba wa watu wengine kwani haiwezi kuhusika kwa namna yoyote kuteka, kuua au kuwashambulia raia wake.

  Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu wakati akizungumzia tukio la kushambuliwa kwa Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.

  Rweyemamu alitoa ufafanuzi huo akijibu taarifa ya gazeti hili juzi iliyonasa na kuchapisha mawasiliano ya ofisa mmoja wa Ikulu akipongeza kazi ya Idara ya Usalama iliyofanikiwa kuandaa video ya Lwakatare.

  Salva alisema Ikulu kamwe haiwezi kuhusika na vitendo vya kuteka raia wake kwani jukumu lake ni kulinda haki za raia wake wote.

  "Ikulu haiwezi kuhusika na mambo ya kijinga kama haya. Inachokifanya ni kuhakikisha inawasaka wahusika ili wafikishwe kwenye vyombo vya sheria na ndiyo maana hata Rais Kikwete alimtembelea Kibanda kule Afrika Kusini alikolazwa," alisema Salva.

  Alisema anamfahamu Kibanda, ameumizwa na jinsi alivyovamiwa na kupigwa na kusababishiwa maumivu na majeraha ya kudumu.

  "Kibanda ni mdogo wangu, mimi ndiye niliyempokea na kumfundisha kazi, siwezi kufurahia alichofanyiwa," alisema.

  Kuhusu mawasiliano ya ofisa wa Ikulu, Salva alimtaja afisa huyo kuwa ni Muhidin Michuzi ambaye ni mmoja wa wapiga picha wa rais.

  Akifafanua kuhusu mawasiliano hayo ya Michuzi, Salva alisema haikuanzia kwake kwani naye alitumiwa na mtu mwingine.

  "Yale mawasiliano hayakuanzia kwa Michuzi. Yeye alitumiwa tu, alichokifanya ni ku-‘share' ile taarifa na watumishi wengine wa Ikulu. Hapa kosa lake nini?" alihoji Salva.

  Hata hivyo, Salva alitahadharisha kwamba ni kosa kisheria kwa mtu yoyote kuingilia mawasiliano ya mtu na kuyaweka hadharani.

  Alivitaka vyombo vya habari kuviachia vyombo vya dola kuchunguza tukio la kushambuliwa kwa Kibanda badala ya kuandika habari za mitaani.


  CHANZO: Tanzania Daima online la tarehe 18/03/2013.
   
 2. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2013
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Majibu ya mkurupuuzi wa ikulu huayananikera kweli kweli,hakuna cha weledi wala umakini wa mtu aliesoma bali ni. Mipasho na mapovu tu,kweli magogoni kumepata watu wa sampuli yake ambao watakumbukwa kwa matendo yao ya kisampuli sampuli!!!
   
 3. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Hili gazeti limekosa weledi linaokoteza taarifa uswahilini na kuona ni taarifa mhm
   
 4. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Tanzania daima linapaswa liwe gazeti la udaku kama yale ya shigongo, yanayoandika habari za kufumaniana na kunyang'anya wapenzi mitaani.
   
 5. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,403
  Likes Received: 14,030
  Trophy Points: 280
  Salva anadhani JK kwenda kumtembelea Kibanda hospital basi ni ushahidi tosha wa ikulu kutohusika.
  Salva acha hoja za watoto wa lapili B
   
 6. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2013
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 44,403
  Likes Received: 14,030
  Trophy Points: 280
  Hahahahahaha
  Tunajua mko njiani kulifungua maana linawaacha kama mlivyo zaliwa

   
 7. Maboso

  Maboso JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 4,305
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Kutrace source ya email ni kazi rahisi sana kwangu. Kuna thread ilikuja na hayo mawasiliano ya emails nikamuomba muhusika wa hiyo post anipatia baadhi ya vitu ili nitrace na wanajukwaa wote tuujue ukweli lakini jamaa akatokomea. Hii inanipa wasiwasi kuwa huenda hizo emails zilisukwa ili kuaminisha watu kuwa ile video ulikuwa mpango wa TISS.

  Nimeona hata katika michango ya ile video watu wametoa maoni mbalimbali ikiwemo technology za kung'amua uhalisia wa ile video. Lakini hakuna hata mmoja ambaye kajitolea kutumia hizo technology ili kutupa ukweli wanajukwaa.

  Ninaamini kuwa humu ndani hakuwezi kukosa wataalam. Sasa kukaa kimya kunanifanya niamini ile video ni ya ukweli kabisa.
   
 8. utaifakwanza

  utaifakwanza JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 1, 2013
  Messages: 14,101
  Likes Received: 1,714
  Trophy Points: 280
  Tanzania daima linapaswa liwe gazeti la udaku kama yale ya shigongo, yanayoandika habari za kufumaniana na kunyang'anya wapenzi mitaani.
   
 9. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #9
  Mar 18, 2013
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 15,797
  Likes Received: 2,380
  Trophy Points: 280
  Kumbe na wewe umenote hiyo kitu betwEen lines,
  Hajuhi anayelia sana kwenye msiba unaweza kuta ni muhusika.
  Kumbe ndio maana mkweree fasta kaenda kupiga picha na kwenye magazeti front page, kumbe ni strategies za Ikulu kuwa itaonekana unahuruma na uhusiki.
   
 10. Abdillahjr

  Abdillahjr JF-Expert Member

  #10
  Mar 18, 2013
  Joined: Oct 3, 2011
  Messages: 694
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Naona upo night shift hapo Lumumba,tafadhali itendee haki tanzania ya wazalendo,badilisha hiyo username/id yako,waangalie wenzio sio majuha kua na ritz,rejao,chama and the like!! Kazi njema ila yana mwisho!!
   
 11. S

  Salary Slip JF-Expert Member

  #11
  Mar 18, 2013
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 26,955
  Likes Received: 44,884
  Trophy Points: 280
  Jipe moyo!One day yes!
   
 12. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #12
  Mar 18, 2013
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,569
  Likes Received: 896
  Trophy Points: 280
  Kwa hiyo Polisi kuchukua video Kutoka Youtube / Jamii Forum wao hawajaokoteza ni sahihi.
   
 13. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #13
  Mar 18, 2013
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 638
  Trophy Points: 280
  Anakanusha halafu hapo hapo anatishia. Inaashiria anaficha ukweli
   
 14. kibogo

  kibogo JF-Expert Member

  #14
  Mar 18, 2013
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 9,569
  Likes Received: 896
  Trophy Points: 280
  Mkuu hapo kwenye RED kwa mtazamo wangu watu hawawezi kukurupuka tu kufanya hayo wanataka Lwakatare apelekwe Mahakamani na na hayo yatafanyika hapo baadae ili kuuthibitishia umma ukweli juu ya hilo
   
 15. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #15
  Mar 18, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,473
  Likes Received: 22,709
  Trophy Points: 280
  Mkuu Maboso, the burden of proof lies with the prosecution, the same applies to allegations, anae prove ni alie allege in case hii subject matter ya video, mimi nimeoiona kwa naked ayes tuu kuwa video ile ni "bonafine genuine", hivyo wenye jukumu la ku proove kuwa imekuwa doctored ni hao wanaoamini ni ya kughushi.

  NB. Video kuwa "bonafide genuine" ni jambo moja, kufikishwa kwa Rwakatare mahakamani ni jambo jingine!, admissibility ya e-evidence kwa video hiyo kukubalika kama ushahidi ni jambo jingine, na Rwakatare kuwa na kesi ya kujibu nalo ni jingine tena!, hoja kubwa ya msingi iliyopo hivi sasa ni "jee Rwakatare was "a solo" artist au hiyo single ni ya "bendi?!". Kama ni solo, kesho mtamshuhudia mahakamani, kama sio single yake bali ya bendi!, hapo sasa ndipo kazi ilipo!.

  Pasco.
   
 16. Maboso

  Maboso JF-Expert Member

  #16
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 4,305
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Teknolojia haina siasa wala propaganda mkuu.
   
 17. Maboso

  Maboso JF-Expert Member

  #17
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 4,305
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Pasco,
  Mimi pia naiona ile video ina uhalisia kabisa ndio maana nasema hao wanosema ni feki basi watumie utaalamu wao waproove. Kwa upande wa zile email, mie kwangu naona ni za kupikwa ndio maana nilitaka niproove hilo humu humu jamvini. Maana ninachokiona ni juhudi za hali ya juu za kutengeneza mazingira kutaka kutuaminisha kuwa TISS wamehusika na ile video.
   
 18. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,143
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 145
  Wakati wewe unalishangaa gazeti, mimi namshangaa Lweyemamu, kwa jinsi anavyojibu maswali kihuni. Ameulizwa swali kuhusiana na majisifu ya viongozi wa Ikulu kuhusu video, yeye anajibu kuhusu kuumizwa kwa Kibanda. Si angejibu kwanza suala la nani ameandaa video? Ngoja tuone hii movie inakoishia, japo sidhani kama hii itatosha kuimaliza CHADEMA.
   
 19. master peace

  master peace JF-Expert Member

  #19
  Mar 18, 2013
  Joined: Dec 19, 2012
  Messages: 1,451
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hongera mkuu naona uko zamu, bado masaa ili muumbuke vizuri, umeona magogoni wanavyo jichanganya?
   
 20. Maboso

  Maboso JF-Expert Member

  #20
  Mar 18, 2013
  Joined: Feb 18, 2013
  Messages: 4,305
  Likes Received: 2,632
  Trophy Points: 280
  Kutoa ushahidi humu jamvini hakumaanishi kutabadilisha structure ya ile video hivyo kuaffect ushahidi mahakamani. Unzuri ni kwamba teknolojia haina siasa. Kwa maana hiyo there is no proof kuwa ile video ni feki.
   
Loading...