Lwakatare: Siwezi kuwa mzururaji wa vyama vya siasa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lwakatare: Siwezi kuwa mzururaji wa vyama vya siasa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Apr 1, 2009.

 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Lwakatare: Siwezi kuwa mzururaji wa vyama vya siasa

  na Mobin Sarya

  MJUMBE wa Baraza Kuu la Chama cha Wananchi (CUF), ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho, Wilfred Lwakatare, amesema hawezi kudhalilisha utu wake kwa kugeuka mzururaji kwenye vyama vya siasa.

  Akizungumza na Tanzania Daima Jumatano jana kuhusiana na uvumi uliozagaa kwamba ameakiasi chama hicho na anakusudia kukihama baada ya kuenguliwa nafasi yake ya unaibu Katibu Mkuu, Lwatare alisema atakuwa amewasaliti wapiga kura wake kwa kufanya hivyo.

  “Siwezi kujidhalilisha kiasi hicho, nitakuwa nimewasaliti wafuasi wangu pamoja na wajumbe wa CUF nchi nzima walionichagua kwa kishindo katika uchaguzi uliopita kuwa mjumbe wa Baraza kuu, nikapata kura nyingi kuliko mjumbe yeyote nikifuatiwa na Juma Haji Duni,” alisema Lwakatare.

  Alisema kwa matokeo hayo yanadhihirisha wazi jinsi anavyokubalika na kupendwa ndani ya chama hicho, ingawa Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba amemuacha katika uteuzi wa nafasi ya Naibu Katibu Mkuu Bara kama alivyofanya kwa Juma Haji Duni.

  Hata hivyo, alisema hawezi kujua sababu iliyosababisha asiteuliwe kwenye nafasi hiyo tena, ingawa anaamini mwenyekiti wake ameamua kutumia uwezo wake kikatiba na kumchagua, Joran Bashange kutoka Morogoro.

  Lwakatare alisema anachojivunia ni kwamba wananchi wa Jimbo la Bukoba ndio mtaji wa kisiasa, wala hilo la kuachwa haliwezi kumsumbua ingawa wajumbe wengi kutoka mikoani wamekuwa wakihoji kwanini ameachwa

  ________________________

  The real leader nilisema hapa kuwa mtu asibabaike na ukubwa wa Chama, jambo muhimu ni kule anakotoka ikiwa wananchi wanaimani na wewe hata ukiwa mfagia ofisi basi watakuunga mkono tu, ndio nikasema wale wa wafuasi wa Sultani CCM ikiwa kweli wanajiamini kuwa ni watetezi wa wananchi hata wasione tabu kumhama Sultani CCM na kujiunga Chama kingine chochote kile kubaki na Sultani CCM ni kubaki na damu ya kifisadi rangi ya kifisadi na kabila la kifisadi na mambu ya kifisadi, majumuisho ni kuwa ukihama huko kama ulipokuwa CCM ulipata kura 999 basi ukihamia upinzani utapata 1000 ,imani ya wananchi kwako itazidi na kuona kuwa ni kweli upo kwa kutetea maslahi yao na kuupinga udhalim kwa Tanzania nzima ,ila kubakia kwa Sultani CCM ni kutafuta ugonjwa wa moyo na sindikizo la damu.

  Huu ni wakati muwafaka wa kuihama CCM usingojee mpaka Sultani amekutafutia mgombea mbadala ikifikia hapo basi ujue ndio mwanzo wa kupigwa buti na haitokubalika kurukia chama kingine na wananchi wakakukubali ,huu ndio msimu mzuri wa kuhamia Chama kingine ili kutunza wapiga kura wako ambao wamechoshwa na siasa zisizo na faida na sera za Sultani CCM zisizo tekelezeka.

  Mlioko kwa Sultani CCM upepo wa mabadiliko unaitembelea Tanzania na kuanguka kwa Sultani CCM kunanyemelea kwa kasi kubwa sana isivyotegemewa ,huwezi kuamini ikiwa unajipa moyo kuwa kwa sasa CCM haiwezi kuondoka madarakani huko ni kujidanganya kukubwa ambako hujawahi kujidanganya toka uzaliwe ,ndio maana yake una macho lakini huoni una masikio lakini husikii ndio katika nyinyi mnaong'ang;ania kubakia na CCM ,mkiamini kuwa CCM ndio iliyowafikisha hapo na kuwacha kuwaamini wananchi ambao ndio waliowapa kura ,nakuhakikishieni kuwa ikiwa umewaamini wananchi wako unaweza kwenda Chama chochote kile na ukahama nao na wakakupa kura zako ni hatari kubakia kwa Sultani CCM kwani wananchi walio wengi hawana imani nae au imani imewatoka ,wewe waliokuchagua na kukufikisha bungeni huna unalowafanyia ,kauli zako na kuunga mkono kwako huko bungeni si kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi wa kijijini kwako au WaTanzania kwa ujumla bali unatumiaka na Wafuasi waliokusdi nguvu kuwavushia miradi yao ya utapeli ,au uongo ?

  Wewe unadai kujengewa barabara kwa wapiga kura wako,unadai kujengewa zahanati kwa wapiga kura wako unadai kila unachoona kitakuonyesha kuwa wewe upo bungeni kwa kuwaletea maendeleo ,toka uhamie hapo hujafanikiwa hata kuwapelekea kiwembe cha kujinyolea kutoka serikalini kama ni faida ya wewe kuwepo hapo ,hivi wananchi hao wakuchague kwa jambo gani ,umepiga makelele kuwadaia lakini hakuna hata moja lililotekelezwa miradi yote inayopitishwa huwa ni miradi hewa kwa wananchi na miradi faida binafsi kwa wengine ,hama Chama cha Sultani CCM kwa kuwaridhisha wananchi wako ,ni bora uwepo upinzani utaisabika ni mkweli kuliko kubaki kwa mtawala CCM utakuwa unapoteza wapiga kura wako na kuwapa fursa ya kuhamia kwengine maana kama waliokupigia kura 2005 ni 100 ukirudi utawakuta wamebaki 50 tena wagonjwa wahoi bintaaban huna la kuwambia jipya ukipiga kampeni za kuwafurahisha 25 watakuona muongo mkbwa kama wewe hakuna utabakiza 25 hawa ni ndugu na jamaa zako wa karibu watabaki wakuchune wakikumaliza wataondoka atabaki mkeo na watoto ambao hawajafikia hata umri wa kupiga kura lazima uulize kama lile shamba la pamba lipo maana toka upate ubunge hujaonekana hujui hata moja.

  Weka kando yote kama hujaamka basi amka na mapema mkakati wa Sultani CCM ni kupandikiza wenzao hadi huko vijijini baada ya kuona kuwa kuna hatari ya ule mtindo wa kupandikiza ukubwani kuwa na mvutano na kuwagawa mapande hivyo wanahakikisha huko huko kijijini mtu wao mvivu anapita. Wewe uliekuwa unaonekana kidomodomo unawekwa kando na mapema njia na mipango wenyewe mnaijua hivyo hama Chama na mapema kwani kuwemo CCM ni kutafuta lawama na wanachi.
   
 2. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #2
  Apr 1, 2009
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Bravo Wilfred! That is what a true politician should really be -- standing by principles!
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Apr 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Angalia mkuu, wanasiasa hawakawii kubadilika
   
 4. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #4
  Apr 1, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi kwani Juma Duni Haji si aliteuliwa tena kuwa Naibu Katibu Mkuu Visiwani. Ama sijaelewa maneno ya Lwakatare yanayoonesha pia Juma Duni Haji hakuteuliwa. Lakini kwa yote Lwakatare kaonesha ukomavu, jinsi CUF ina nguvu BK mjini, nadhani bado ana nafasi 2010 kama atapitishwa, japo yaweza tokea mizengwe ya CCM kama ya 2005.
   
 5. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #5
  Apr 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Hapo aliposema hajui sababu naweza kumsaidia ,Lwakatare ameshakuwa ,aarufu nchi nzima ,hivyo ili kukijenga Chama Mwenyekiti ameonelea aongeze safu ya kuwafanya kuwepo kwa elimu ambayo itawafanya wanasiasa wa CUF wawe wengi katika kujulikana na wananchi watakuwa tayari kumsikiliza yeyoyote yule ikiwa huyu hayupo aliekuwepo anatosha kabisa,kule Zanzibar kulikuwa kunabadilishwa badilishwa viongozi sana wa CUF wanahamishwa hamishwa na kupewa madaraka japo ya master ukumbi au mkutano just kukaribisha wageni na pale unakuwa unarapu kivyako ili kuizoea stage ya mapambano ya kisiasa ,nasema Tambwe Hiza alikuwa hajulikani alipokuwa CCM na umachachari wake umepatikana katika stage za CUF nakumbuka hata huyo mvaa Hat wa Chadema ,siku moja alikaribishwa kwenye stage za siasa za CUF pale Zenji amini usiamini ujeshi na ukamando wote ulimtoka kila wakati akionekana kupandisha pumzi kwa nguvu na kuzishusha kwa ufupi alikuwa haamini umati wa watu waliohudhuria ,unamshinda hata Raisi wa Jamhuri ya Muungano kwa jinsi ya watu wanavyohudhuria mikutano ya CUF si mchezo kama hujawahi kupanda jukwaa la kisiasa na kukutana na umati wa mikutano ya CUF kule Zenji basi lazima utatetemeka miguu na kutetemeka katika maneno na si ajabu hata sauti ikawa inapotea,Mvaa Hat mwenyewe alikiri kuwa hajawahi kuhutubia umati mkubwa kama huo ni mara yake ya kwanza ,nasema nae alipata ukakamavu wa kusimama kwenye jukwaa,so Lwakatare ameshakuwa mwalimu na ni mtu ambae nampa nafasi hata mlipovumisha siasa hapa nilisema kuwa ana hiari yake,CUF si Chama Cha kiongozi yeyote yule ni mtu na wapiga kura wake waliomchagua na ni demokrasia ,tofauti na wengine ambao wameondoka na huko wanakofikia wanatoa maneno ya ufedhuli ili kuwafurahisha wengine ,zaidi ni mtu mwenyewe kujiharibia nafikiri na kupoteza umaarufu baada ya kuwa mwanasiasa unakuwa unatumiwa na kupoteza hadhi yako ya kuupata ubunge au uongozi katika nchi hii ,yuko mwengine ambae akijulika kwa jina la Shaibu Akwilombe huyu aliondoka CUF nafikiri sijui alielekea Chadema au yupo CCM kwa kweli alikuwa msemaji mzuri sana ndani ya CUF karibu mikutano mingi alikuwa akizungumza na kupata sapoti kubwa ya usikilizaji yeye zaidi alikuwa anapata watu wenye akili kumsikiliza kwani alikuwa anatoa lecture safi sana kwa vijana na ikitoa ushawishi mkubwa kwa vijana ,yeye sijui kapotelea wapi ,maana umaarufu aliokuwa ameanza kujipatia ulikuwa si wa kawaida ,alikuwa anelekea katika safu ya powerfull leaders kwa speech zake baaada ya kuondoka CUF sijamuona kusikika ,hii ni hasara ya kuhama hama vyama na zaidi pale unapohama halafu ukapandishwa jukwaani useme ovyo unauliwa kisiasa bila ya wewe mwenyewe kujua ndio hapo sasa Tambwe anaambiwa atubu ,sijui kama mwenyewe amefahamu kwa kina jembe hilo.
   
 6. Timtim

  Timtim JF-Expert Member

  #6
  Apr 1, 2009
  Joined: Feb 9, 2008
  Messages: 603
  Likes Received: 64
  Trophy Points: 45
  Pamoja na yote naamini (chama) palipo na maslahi ndipo mwanasiasa anaegemea.
   
 7. mpenda pombe

  mpenda pombe JF-Expert Member

  #7
  Jun 5, 2017
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 1,188
  Likes Received: 387
  Trophy Points: 180
  Upo sahihi mkuu.
   
Loading...