Lwakatare: Sina tatizo na Rais Magufuli, mimi ni nyani mzee

Hawa ndiyo wabunge tunaotaka. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi wote jimboni mwake: wa vyama vyote na wasio na vyama, waliompa kura na wasiompa kura. Lengo kuu la mbunge ni kuleta maendeleo kwa jimbo lake. Maendeleo na ufisadi ni incompatible.

Big up Lwakatare. Hope wabunge vijana kama akina Mdee, Lissu na Lema watajifunza kwa hawa wazee wao.
 
Hayo ni maoni yake,ila kuna ufisadi mwingi bwana yule anaogopa kuugusa,.e.g escrow
Escrow ilitokea wakati wa awamu ya nne ambayo ilishamiri upigaji deals. Ninauhakika kama ingekuwa awamu hii kamwe haingetokea. Watu kama mwanasheria mkuu wa wakati huo na mkurugenzi mtendaji wa tanesco wa wakati ule wangetumbuliwa kabla deal hilo la escrow halijafanyika.
 
Hawa ndiyo wabunge tunaotaka. Mbunge ni mwakilishi wa wananchi wote jimboni mwake: wa vyama vyote na wasio na vyama, waliompa kura na wasiompa kura. Lengo kuu la mbunge ni kuleta maendeleo kwa jimbo lake. Maendeleo na ufisadi ni incompatible.

Big up Lwakatare. Hope wabunge vijana kama akina Mdee, Lissu na Lema watajifunza kwa hawa wazee wao.
Hapo umepatia kabisa, mimi ni mpenda upinzani lakini ukiwa mbunge lazima uangalie maslahi ya watu wako wote, waliokupigia na wasiokupigia

na hicho magufuli anakijua na anajua ufisadi ndo uliokuwa unahafifisha ccm. kama anajitahidi kuuondoa lazima tumuunge mkono ili tuangalie 2020 tutakuwa tumefika wapi kimaendeleo
 
MOTOCHINI kheri ya mwaka mupya! Huonekani jukwaani mkuu, au ulienda kula migebuka na mawese na ukakuta mitandao ya 4G haipatikani huko? Karibu tena, ila mzee wako kaharibu tena huko kwenye senene kajisahau kuwa yeye ni kiongozi wao akafikiri wale wako Darfur
bado uko Korea Chakaza? Heri ya mwaka mpya
 
"Mimi sina tatizo na Mh Rais Magufuli, anaendesha nchi vizuri. Kilio cha siku nyingi chetu sisi wapinzani ni kumpata Rais anayepinga rushwa na ufisadi kimesikika. Magufuli anaifanya kazi hiyo vizuri. Tumuungeni mkono.
Nakanusha maneno yanayosambazwa mitandaoni na kundi la watu nisiojua lengo lao.
Huwa sijibizani na ujinga mitandaoni na hasa kulishwa maneno. Nina uzoefu wa kesi ya kwanza ya ugaidi nchi hii na
kilichofanyika kupitia mitandao.
Wanaoweka maneno mitandaoni wanashindwa nini kuweka clip ya video ikionyesha hotuba yangu ya dk 5 niliyoyaongea kwenye Mkutano Bukoba? Mimi ni nyani mzee, nimeshakwepa misha
le mingi. Huo haunipati ng'o".

3.1.2017.

WILFRED LWAKATARE MBUNGE WA BUKOBA MJINI (CHADEMA).

Nina mashaka na aliye andika huu Ujumbe kama ni Wilfred Lwakatare.
 
Kuna kitu inaonekana wana chadema wengi hatujakielewa kutoka kwenye kauli aliyoitoa lwakatare na Joshua nassary kule Arusha nakauli zao zimepelekea wana chadema wengi kuwamlaumu na kumpiga vijembe haswa pasi na kujua au kuwaza kwanini amefanya hivyo.

Nilazima tujufunze mbinu za kuishi na hasimu wako haswa pale unapogungua kuwa hasimu wako anapenda sana vitu flani ,so ili atekeleze hitaji lako ni lazima uende nae sawa.

Mfano
Unapo gundua hasimu wako anapenda umbea, inakubidi umtafutie umbea ili akiusikia afurahi na kutekeleza unachokitaka kwa urahisi.

ndiyo sababu utagundua kuwa umbea na unafiki umetamalaki sana kwa sasa kwasababu walio karibu wanajia umbea unalipa sana haswa kwa nyakati hizi.

Ukila na kipofu ...............................
 
HARI SI SHWARI CDM ITENI ZIMAMOTO
Kuwa smart hata kidogo wewe!! UKAWA wameamua kuto kumkosoa Mtakatifu John huku waki mpigia makofi wakati anajikaanga na mafuta yake mwenyewe kama Kitimoto. Inshort wame mtupia kamba ili ajinyonge mwenyewe.
 
Kuna kitu inaonekana wana chadema wengi hatujakielewa kutoka kwenye kauli aliyoitoa lwakatare na Joshua nassary kule Arusha nakauli zao zimepelekea wana chadema wengi kuwamlaumu na kumpiga vijembe haswa pasi na kujua au kuwaza kwanini amefanya hivyo.

Nilazima tujufunze mbinu za kuishi na hasimu wako haswa pale unapogungua kuwa hasimu wako anapenda sana vitu flani ,so ili atekeleze hitaji lako ni lazima uende nae sawa.

Mfano
Unapo gundua hasimu wako anapenda umbea, inakubidi umtafutie umbea ili akiusikia afurahi na kutekeleza unachokitaka kwa urahisi.

ndiyo sababu utagundua kuwa umbea na unafiki umetamalaki sana kwa sasa kwasababu walio karibu wanajia umbea unalipa sana haswa kwa nyakati hizi.

Ukila na kipofu ...............................
Huu ndio Ukweli, kwakua mtukufu John hapendi kukosolewa basi klicho bakia nikumpigia makofi wakati akielekea kutumbukia shimoni.
 
No offense

Huyu sizonje ni kumsifia tu kinafiki ili walau wananchi wasife njaa

manake anaweza kuamua kuwakomoa tu wananchi kisa wamechagua opposition

Anajijua mwenyewe

hahahahahah

Mniombeee
 
Kuna taarifa inasambaa mitandaoni ikidai nilisema hivi:

Nakanusha maneno yanayosambazwa mitandaoni na kundi la watu nisiojua lengo lao.

Huwa sijibizani na hasa ninapolishwa maneno. Nina uzoefu wa kesi ya kwanza ya ugaidi nchi hii na kilichofanyika kupitia mitandao.

Wanaoweka maneno mitandaoni wanashindwa nini kuweka clip ya video ikionyesha hotuba yangu ya dk 5 niliyoyaongea kwenye Mkutano Bukoba?

Mimi ni nyani mzee, nimeshakwepa mishale mingi. Huo haunipati ng'o".

3.1.2017.

WILFRED LWAKATARE MBUNGE WA BUKOBA MJINI (CHADEMA).
 
Attachments

  • lwaka.jpg
    lwaka.jpg
    133.1 KB · Views: 42
Back
Top Bottom