Lwakatare: Sina tatizo na Rais Magufuli, mimi ni nyani mzee

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,980
2,000
Kuna taarifa inasambaa mitandaoni ikidai nilisema hivi:
"Mimi sina tatizo na Mh Rais Magufuli, anaendesha nchi vizuri. Kilio cha siku nyingi chetu sisi wapinzani ni kumpata Rais anayepinga rushwa na ufisadi kimesikika. Magufuli anaifanya kazi hiyo vizuri. Tumuungeni mkono."
Nakanusha maneno yanayosambazwa mitandaoni na kundi la watu nisiojua lengo lao.

Huwa sijibizani na hasa ninapolishwa maneno. Nina uzoefu wa kesi ya kwanza ya ugaidi nchi hii na kilichofanyika kupitia mitandao.

Wanaoweka maneno mitandaoni wanashindwa nini kuweka clip ya video ikionyesha hotuba yangu ya dk 5 niliyoyaongea kwenye Mkutano Bukoba?

Mimi ni nyani mzee, nimeshakwepa mishale mingi. Huo haunipati ng'o".

3.1.2017.

WILFRED LWAKATARE MBUNGE WA BUKOBA MJINI (CHADEMA).
 

cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
24,811
2,000
Itakuwa vizuri wajipange siku ingine wajirekodi na sio kusubiri mapaparazi.

Nashangaa wapinzani wa nchi walipewa nafasi ya Mbunge kuongea, na hakuna aliyerekodi kusambaza alichosema.

Iwe funzo na sio kulalamika kwa maandishi tu.

Mwanya mmepewa hamjauchukulia kujipaisha, shame. Rais asingewapa nafasi mngekuwa wa kwanza kulalamika.
 

bily

JF-Expert Member
Apr 5, 2012
8,040
2,000
Sijajua tatizo lipo wapi ? Ni maoni yake kama mtanzania wa kawaida.
 

nyabhingi

JF-Expert Member
Oct 12, 2010
14,374
2,000
Hayo ni maoni yake,ila kuna ufisadi mwingi bwana yule anaogopa kuugusa,.e.g escrow
 

Frey Cosseny

JF-Expert Member
Feb 4, 2015
1,987
2,000
"Mimi sina tatizo na Mh Rais Magufuli, anaendesha nchi vizuri.Kilio cha siku nyingi chetu sisi wapinzani ni kumpata Rais anayepinga rushwa na ufisadi kimesikika. Magufuli anaifanya kazi hiyo vizuri .Tumuungeni mkono."

Nakanusha maneno yanayosambazwa mitandanoni na kundi la watu nisiojua lengo lao.
Huwa sijibizani na ujinga mitandaoni na hasa kulishwa maneno. Nina uzoefu wa kesi ya kwanza ya ugaidi nchi hii na kilichofanyika kupitia mitandao. Wanaoweka maneno mitandaoni wanashindwa nini kuweka clip ya video ikionyesha hotuba yangu ya dk 5 niliyoyaongea kwenye Mkutano Bukoba?
Mimi ni nyani mzee,nimeshakwepa mishale mingi. Huo haunipati n'go

3.1.2017.
WILFRED LWAKATARE MBUNGE WA BUKOBA MJINI (CHADEMA).
Shukrani Nyani mzee
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom