Lwakatare, Silinde wapigwa ‘stop’ na polisi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lwakatare, Silinde wapigwa ‘stop’ na polisi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 6, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,123
  Likes Received: 36,329
  Trophy Points: 280
  Lwakatare, Silinde wapigwa ‘stop’ na polisi


  na Moses Ng'wat, Mbeya


  [​IMG] MBUNGE wa jimbo la Mbozi Magharibi, David Silinde, (CHADEMA), amezuiliwa na jeshi la polisi wilayani humo kufanya mkutano wa hadhara katika kata ya Tunduma uliokuwa na lengo la kuwashukuru wapiga kura wa jimbo hilo kwa kumchagua.
  Silinde aliyekuwa asindikizwe na Willfred Lwakatare ambaye yuko mkoani hapa kwa kazi maalumu ya ukaguzi wa uongozi na urekebishaji wake katika wilaya za mkoa wa Mbeya.
  Kwa mujibu wa mbunge huyo, polisi walimtaka asiitishe mkutano huo kwa kuelezwa kuwa hakutimiza vigezo vya kisheria vinavyoruhusu kufanyika mkutano wa hadhara.
  Akizungumza na waandishi wa habari, mbunge huyo alisema alipanga kufanya mkutano wa hadhara eneo la Mwaka katika mji mdogo wa wa Tunduma, lakini mkuu wa polisi wa wilaya amemkataza kufanya jambo hilo.
  Akizungumzia hilo kamanda wa polisi Mkoa wa Mbeya, Advocate Nyombi, alisema sababu kuu iliyosababisha jeshi hilo kushindwa kuruhusu mkutano huo wa hadhara ufanyike ni muombaji kutokidhi vigezo vya kisheria.
  Alitaja kigezo hicho kuwa mbunge huyo alichelewa kuomba kibali kwani maombi ya kibali yalifika ofisi za polisi wilaya jana, na kwamba sheria inataka kibali kiombwe si chini ya saa 48.
  “Hatuna ubaya na waheshimiwa tatizo ni watu kushindwa kuzingatia sheria, lazima kibali kisiwe chini ya saa 48 lakini wao waliomba jana yaani juzi Januari 5 na leo yaani Januari 6, hebu angalia wana saangapi tangu waombe na sheria inasemaje,” alisema Nyombi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 6, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 80,123
  Likes Received: 36,329
  Trophy Points: 280
  Hili vuguvugu la watanzania kutaka uhuru zaidi JK anafikiri ataweza kulizuia nchi nzima tutakapoanza kuandamana? Polisi watatosha.....Hivi sasa polisi wa Dar na Moshi wapo Arusha...............................maandamano yatakapohamia huko Dar na Moshi.........watafanyaje?
   
 3. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #3
  Jan 6, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,573
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  sasa ndiyo demokrasia gani hii? yaani watu wasiwe na mikutano? hofu ya uvunjifu wa amani kila siku inatoka wapi? si tunaambiwa tz ni nchi ya amani na utulivu? we need to redefine these words!
   
 4. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #4
  Jan 6, 2011
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,305
  Likes Received: 121
  Trophy Points: 160
  Si waombe tena
   
Loading...