Lwakatare: Nilimwona Mungu nikiwa mahabusu

Jackal

JF-Expert Member
Apr 10, 2012
9,686
12,981
MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare amesema siku 92 alizokaa gerezani, alimwona Mungu, ndiyo maana yupo nje kwa dhamana. Pamoja na kumwona Mungu, mkurugenzi huyo ameahidi kuandika kitabu kinachoelezea maisha yake hatua kwa hatua jinsi alivyoishi mahabusu kwa siku hizo.

"Nimeamua kutengeneza kitabu kitakachoelezea maisha yangu hatua kwa hatua siku zote 92 nilizokaa mahabusu," alisema Lwakatare wakati wa ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa King'ong'o, Kimara jijini Dar es Salaam.

Lwakatare alikamatwa Machi 11 mwaka huu na kuachiwa kwa dhamana Juni 11 kwa tuhuma za ugaidi kabla ya kufutwa na kubaki na shitaka la kupanga njama za kutaka kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.

Alisema Mungu amejibu maombi yake bila kuangalia dini, dhehebu wala itikadi. "Washarika wenzangu Mungu anajibu maombi kama utamwomba kwa nafsi moja… nikiwa gerezani nimejifunza kitu kimoja, Mungu hakujibu kwa sababu wewe ni dini fulani, dhehebu fulani au chama fuani, anajibu kama utanyenyekea na kupeleka hitaji lako."

Alisema akiwa gerezani na mahabusu mwenzake Sheikh Ponda Issa Ponda, kila mtu alikuwa akitumia muda wake mwingi kumwomba Mungu kwa imani anayoamini

SOURCE:TANZANIA DAIMA
 
Mathayo 7:21-23
Si kila mtu aniambiaye, Bwana, Bwana, atakayeingia katika ufalme wa mbinguni; bali ni yeye afanyaye mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni.
Wengi wataniambia siku ile, Bwana, Bwana, hatukufanya unabii kwa jina lako, na kwa jina lako kutoa pepo, na kwa jina lako kufanya miujiza mingi?
Ndipo nitawaambia dhahiri, Sikuwajua ninyi kamwe; ondokeni kwangu, ninyi mtendao maovu.

Matthew 7:21-23
"Not everyone who says to me, 'Lord, Lord,' will enter into the kingdom of heaven - only the one who does the will of my Father in heaven.
On that day, many will say to me, 'Lord, Lord, didn't we prophesy in your name, and in your name cast out demons and do many powerful deeds?'
Then I will declare to them, 'I never knew you. Go away from me, you lawbreakers!'

Sheria zinatungwa na binadamu na binadamu wanaweza kucheza na sheria. Sio wote walioko mitaani ni wasafi, wengine wako mitaani kwa sababu sheria hazina macho.
 
Biblia ,Kutoka 33:20 "Kisha (Mungu) akasema, Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaisha(akaendelea kuishi)".
 
Wewe stroke peleka uchafu wako kwa baba yako na sio kutuletea humu.
Umezidi sana kudhihaki watu, unashindwa hata kuheshimu imani za watu wengine.

inategemea wewe unaichukulia vp, hilo ni wazo tu mkuu, kashfa imetoka wapi hapo
 
Anayemtumaini Mungu, siku zote kwa moyo mkuu. Ataona mastaajabu, zikija shida na msiba. Anayemngojea Mungu, amejenga juu ya mwamba. Katika shida usidhani Mungu kaniacha sasa lakini matajiri wote anawapenda vizuri. Mungu aweza upesi kugeuza hali yo yote. Anayemtumaini Mungu ni kama mlima Sayuni, hatatingishika milele yote..

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Alimwona Mungu kwa njia ya yeye kuweza kuishi mahabusu na sio kumwona live maana imeandikwa kuwa hakuna ataemwona Mungu akapona
 
Aine ...FP?
Na tumtafute Mungu wakati wowote maadam anapatikana
siyo tungojee kwenda lupango ndo tujue kuwa Mungu yupo
hii labda ni kwa wale wa mataifa.

FP, Mungu huonekana wakati wote, ila sisi wanadamu mara nyingi tunamtafuta Mungu tukiwa na shida tu!
 
Last edited by a moderator:
samahani lakini, kwani huyo Denis Msaky na yule jamaa anayetaka kumkatia rufaa (ndio mara yangu ya kwanza kusikia rufaa kama hiyo) wanasali sehemu gani!?
 
MKURUGENZI wa Ulinzi na Usalama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Wilfred Lwakatare amesema siku 92 alizokaa gerezani, alimwona Mungu, ndiyo maana yupo nje kwa dhamana.
Pamoja na kumwona Mungu, mkurugenzi huyo ameahidi kuandika kitabu kinachoelezea maisha yake hatua kwa hatua jinsi alivyoishi mahabusu kwa siku hizo.
“Nimeamua kutengeneza kitabu kitakachoelezea maisha yangu hatua kwa hatua siku zote 92 nilizokaa mahabusu,” alisema Lwakatare wakati wa ibada ya shukrani kwa Mungu iliyofanyika kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT) Usharika wa King’ong’o, Kimara jijini Dar es Salaam.
Lwakatare alikamatwa Machi 11 mwaka huu na kuachiwa kwa dhamana Juni 11 kwa tuhuma za ugaidi kabla ya kufutwa na kubaki na shitaka la kupanga njama za kutaka kumdhuru Mhariri Mtendaji wa gazeti la Mwananchi, Denis Msacky.
Alisema Mungu amejibu maombi yake bila kuangalia dini, dhehebu wala itikadi. “Washarika wenzangu Mungu anajibu maombi kama utamwomba kwa nafsi moja… nikiwa gerezani nimejifunza kitu kimoja, Mungu hakujibu kwa sababu wewe ni dini fulani, dhehebu fulani au chama fuani, anajibu kama utanyenyekea na kupeleka hitaji lako.”
Alisema akiwa gerezani na mahabusu mwenzake Sheikh Ponda Issa Ponda, kila mtu alikuwa akitumia muda wake mwingi kumwomba Mungu kwa imani anayoamini

SOURCE:TANZANIA DAIMA

Kumbe source Tanzania Daima? Ok najua sasa nilitaka kushangaa
 
Aache kulisha watu sumu huo usanii wa roho mtakatifu tumeusikia kwa wasanii wenzake wengi tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom