Kwa kuwa ushirikiano umeshindikana, wanasiasa mahiri lazima waamue uwanja wao kufanya siasa-ama CHADEMA au CUF. Kwa maoni yangu sioni kwa nini Lwakatare aendelee kubaki huko alipo. Kimsingi hana sababu!
Mbona unajichanganya, unasema wanasiasa mahiri lazima waamue kuwa CHADEMA ama CUF, halafu hapo hapo unaona Lwakatare hafai kubaki CUF.
Nikirudi kwa mada, kwa BK mjini hata uchaguzi wa 2005 huyu jamaa walimfanyizia CCM ili ashindwe. Mazingira ya siku ya kuhesabu na kutangaza kura yanaonesha hilo. CUF ina nguvu sana BK mjini.