Lwakatare aufunika mji wa Bukoba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lwakatare aufunika mji wa Bukoba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kaa la Moto, Apr 4, 2009.

 1. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #1
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Wakuu nimepokea picha hizi toka Bukoba na kuambiwa kwamba Lwakatare amefika Bukoba na kulakiwa na umati mkubwa wa wafuasi wake pale uwanja wa ndege na kufanya maandamano makubwa ya kumpongeza na kisha kuhutubia mkutano mkubwa sana tangu 2005.

  Nasikia kwa hili wafuasi wa Lwakatare walikuwa wanawa beep SISI M waliokuwa wanadhani huyu bwana kaisha kisiasa kwa sababu mshindani wake kwanza ni waziri mtoto au niseme mtoto wa waziri na isitoshe alishawapotosha wana SISI M kwamba alimshinda kaatika kesi ya uchaguzi iliyo mahakamani na anamdai pesa nyingi.

  Habari zaidi zinasema pamoja na vitimbwi vingi vinavyofanywa kumaliza umaarufu wake katika jimbo la Bukoba mjini, lakini ni ajabu bado Lwakatale kaonekana ana wafuasi kibao. Wengi ni walala hoi na inasemekana huyu mpinzani wake mkuu wafuasi wake wengi ni wafanyabiashara au kwa jina lingine matajiri.

  Ukweli ni kwamba SISI M bado wana shughuli 2010. Wasidhani jimbo la Bukoba mjini ni rahisi tena. Inaelekea jimbo hili ni Pemba ya bara. Lazima waje na mbinu kali ambazo alitumia Hon. Obama.

  Haya nawashushia mambo.


  View attachment 4133
  Hii ni sehemu ya maandamano ya wafuasi wa Lwakatare mjini Bukoba

  View attachment 4134
  Wafuasi wakiwa wamebeba majani ya miti kama moja ya upambaji wa maandano yao.

  View attachment 4135
  Hii ni sehemu ya maandamano ya wafuasi wa Lwakatare mjini Bukoba

  View attachment 4136
  Hii ni sehemu ya maandamano ya wafuasi wa Lwakatare mjini Bukoba

  View attachment 4137
  Hii ni sehemu ya maandamano ya wafuasi wa Lwakatare mjini Bukoba

  View attachment 4138
  Mheshimiwa Lwakatare akiwa anapungia mkono wananchi kila alikopita katika mitaa ya Bukoba mjini.

  View attachment 4139
  Gari iliyobeba walinzi wa mh. Lwakatare katika msafara.

  View attachment 4140
  Hii ni sehemu ya maandamano ya wafuasi wa Lwakatare mjini Bukoba

  View attachment 4141
  Hivi ni baadhi ya vitimbwi vilivyopanba maandamano hayo ya mh. Lwakatare

  View attachment 4142
  Hapa ni katika viwanja vya uhuru ambako ulifanyika mkutano wa hadhara.

  View attachment 4143
  Mkutano wa hadhara katika uwanja wa uhuru.
   
 2. B

  Balingilaki Member

  #2
  Apr 4, 2009
  Joined: Aug 2, 2008
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  lwakatare ndo tegemeo lililobaki bk na pia katka jimbo la muleba kusini tunataka mtu kama huyu si yule anayesimama bungeni huku wapiga kula wanaadhilika na kusema ''unataka wabunge wasinunue magari mtu akikuita fisadi we kashitaki''ila pamoja na watu kukosa shule na waliojitolea kujenga akawazuia kwa kuwa alihisi watamnyanganya ubunge yeye amejenga orofa na kushindwa hata kujenga zahanati nzuri mpaka mtu aende kwny hospitali za misheni, lakini huyu bwana wananchi wangote ambao katika wilaya wanaongoza kwa kuwa na wasomi weng katika shahada na shahada za juu wamekuwa wakiongwa chumvi na vipande vya sabuni na kuuza kula zao na haki yao ya kikatiba.

  Bukoba na kagera kwa ujumla wake ambapo elimu ndo ilipoanzia wamegeuka wajinga kimya kimya....................................
   
 3. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #3
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Pamoja na kuwa mkusanyiko huo mkubwa wa wafuasi waliojitokeza kumpokea inaweza kuwa dalili ya kuungwa mkono, lakini uzoefu unaonyesha kuwa makundi ya watu katika mikutano si kigezo sahihi cha ushindi. Lwakatare anatakwia kufanya mikakati ya kujihakikishia kuwa kundi linalomuunga mkono lina wapiga kura wa kutosha, na si watu wa kumshangilia tu ambao hawana shahada za kupigia kura
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Apr 4, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Tanzania bwana! Laiti hizo nguvu tunazotumia kuwatukuza wanasiasa kwenye majukwaa, tungezielekeza kwenye ku mobilize watu wetu ili wajiletee maendeleo yao wenyewe ingekuwa poa sana.

  Kila siku ni wanasiasa majukwaani, tunafanya kazi saa ngapi? Uchaguzi mpaka 2010, si ingelikuwa bora kutumia huu muda ku mobilize resources ili wananchi wajiletee maendeleo yao?

  Mambo kila sehemu yameanza sasa, mwaka mzima kabla ya uchaguzi, kufika mwisho wa mwaka kesho si nchi nzima itakuwa hoi?

  Wasaidieni hao vijana waondoke kwenye vijiwe vya kupiga majungu ya kisiasa na waende kwenye uzalishaji wowote ule.

  Picha ambayo mimi naiona TZ ya sasa sio nzuri kabisa. Watu wenye elimu, kutumia ujinga wa wananchi ili kuwayumbisha. Ingependeza kuona picha za waheshimiwa wakiwaongoza wanachama wao kuchimba visima, kutengeneza barabara, kujenga shule, kuchimba mabwawa ya kuzuia mafuriko nk. badala ya mipicha ya propaganda tu.
   
 5. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #5
  Apr 4, 2009
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,635
  Trophy Points: 280
  Ni ishara nzuri sana kwa Bwana Lwakatare lakini sijui ile kesi yake ya uchaguzi na mheshimiwa Kagasheki inaweza kumyima nafasi ya kugombea ubunge mwaka 2010.
   
 6. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #6
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ikoje hiyo kesi? Ameshitakiwa kuwa ametoa rushwa?
   
 7. N

  Ng'wanamalundi Member

  #7
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 90
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 25
  sawa kabisa. Kumbuka yale maandamano aliyokuwa anapewa Mrema baada ya kujiengua CCM. Kura alizokuwa anapata zilikuwa hazilingani kabisa na ukubwa wa maandamano aliyokuwa anapewa.
   
 8. ThinkPad

  ThinkPad JF-Expert Member

  #8
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 1,851
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Kama mambo ndo hayo,2010 kazi ipo tena pevu
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kazi nzuri aliyoifanya wakati akiwa mbunge bado wananchi wake wanamkumbuka , hivyo kila mmoja wetu hana budi kufanya kazi na akiondoka atawafanya wananchi waweze kumkumbuka na kuendelea kumuunga mkono kama huyu .
   
 10. K

  Kadogoo JF-Expert Member

  #10
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 26, 2007
  Messages: 2,072
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hee!!!

  IMEKUWAJE TENA JAMANI! SI TULIAMBIWA HAPA KUWA LWAKATARE ANAHAMIA CHADEMA? LINI TENA KABADILI UAMUZI WA KUENDELEA KUWA CUF? PIA TUMEAMBIWA KUWA CUF NI CHAMA CHA WAPEMBA SASA HUKO BUKOBA PIA KUNA WAPEMBA!! JAMANI MAALIM SEIF WACHA KUSAFIRISHA MAMLUKI TOKA PEMBA HADI BUKOBA! SASA NA WEWE UMEANZA KUIGA TABIA ZA CCM ZA KULETA MAMLUKI WA KURA TOKA BARA HADI VISIWANI! AU HAYA YA SASA NDIO UTEKELEZAJI WA MAAZIMIO YENU YA CUF KUWA "NGOMA ITAKAVYO PIGWA NDIVYO MUTAKAVYO ICHEZA"?
   
 11. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #11
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mkuu MF, katika hizo picha ulizorushiwa hakuna hata moja inayomwonyesha lwakatare mwenyewe? maana tunaona mashabiki tu!
   
 12. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #12
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Mtanzania,
  Haya ulioandika para ya mwisho ni kweli na huwa inafanyika. Ni lazima uelewe kila kitu kina wakati wake. Kuna wakati wa kufanya uliyosema na kuna wakati wa kukaa pamoja kuzungumzia yaliyofanyika. Kama unataka tukae shambani kila siku, ina maana hakuna siku tutapika na hakuna siku tutakula. Unaposema kila siku watu wanaandamana barabarani si kweli maana hujasema ni mara ngapi umeona haya yakifanyika. Nadhani na wewe umesukumwa tu msimamo wa ki si hasa.
  Na pia ninakushauri uzungumze na raisi wetu MH. sana JMK na serikali yake ambao wao ziara zao haziishi mikoani na kimataifa. Tena hawa ufanya kwa gharama za kodi yetu wavuja jasho.
  Mwisho hawa vijana si wajinga. Siasa ni sehemu ya maisha yao ni lazima waijadili. Maana walipojaribu kunyamaza kuijadili tu hapo wajanja wakaona ndio nafasi ya kuliibia taifa na wamepora kweli kweli mpaka nchi imebaki hoi.
  viongozi wetu hawaoni haya kuita nchi yetu eti ni maskini. Wanashinda kuomba omba na wanaona fahari hata kututangazia kwa ufahari kwamba waliomba pesa na wamepewa au mara nyingine utasikia upuuzi kama niliosikia siku mbili zilizopita kwamba umaskini wa wazungu utatutia matatizoni! kwa nini? eti kwa sababu misaada itapungua. Huu ujinga ujinga tu. Vijana wasipojadili siasa hata kazi wanazofanya hazina maana. Ninachojua kuwa ni hakika maandamano hayo yalihusisha wote, vijana na watu wazima na ajabu wengi wanafanya kazi za vipato na kwa bidii kweli kweli.
  Ebu nikuulize Mtanzania hata ukifanya kazi masaa 18 katika nchi hii ya wadanganyika kuna lolote utavuna? Sana sana utaishia hali ile ile ya umaskini tu. Na unajua kwa nini? Kwa sababu sisi ni wadanganyika na tunadanganywa na chama hiki cha majambazi. Hakika kama nchi itaendelea kuwa chini ya SISI M hatutapata maendeleo kamwe. Maana jitihada zetu wanazimaliza wao.
   
 13. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #13
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Unamfahamu vizuri Lwakatare? angalia picha ya sita.
   
 14. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #14
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kama ni kweli, basi tumekubali kudanganywa (kwa sababu tumeshajua kuwa tunadanganywa). je, tatizo ni anayetudanganya au sisi wenyewe tuliokubali kudanganywa na tukadanganyika?
   
 15. Kitila Mkumbo

  Kitila Mkumbo Verified User

  #15
  Apr 4, 2009
  Joined: Feb 25, 2006
  Messages: 3,347
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145

  Yaani kama vile upo bongo! Huku kazi siku hizi ni siasa, na siasa ni kazi! Kila mahala ukipita mjadala ni siasa. Na inaonekana kama vile huwezi kuchangia maendeleo mpaka uwe mwanasiasa!

  Hata hivyo, haya maandamano ni changamoto kubwa kwa CUF. Maana walipomtema kwenye uongozi kiaina sidhani kama walijua nguvu yake huku Bukoba. Kimsingi Lwakatare ni nguzo nzito sana ya CUF huku bara, kiasi kwamba akinyanyua mguu akautua kwingine atakuwa ameisambaratisha kabisa nguvu ya CUF huku. If I were to be a devil's advocate, can we sustain two strong opposition political parties in TZ? Kwa kuwa ushirikiano umeshindikana, wanasiasa mahiri lazima waamue uwanja wao kufanya siasa-ama CHADEMA au CUF. Kwa maoni yangu sioni kwa nini Lwakatare aendelee kubaki huko alipo. Kimsingi hana sababu!
   
 16. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #16
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Nasikia alilizungumzia hata katika aliyosema kwenye mkutano huo kwamba kama umati wote huo unahitaji agombee 2010 basi ni vema wote watafute shahada. Hii nadhani hata yeye anajua. Ni mwanasiasa mkongwe hawezi kuwa hajui hili. Pia ni kweli si wote wanaokuwa katika pilika pilika upiga kura maana misafara ya Mamba na Kenge wamo lakini pia tusisahau kuwa mwanzo wa mvua ni mawingu na manapofuka moshi.........?
   
 17. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #17
  Apr 4, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Ooooh namfahamu sana! Sikumuona awali Mkuu, thanks kwa kunionyesha
   
 18. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #18
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Kesi ya uchaguzi alishindwa na akakata rufaa mahakama ya rufaa
   
 19. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #19
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Jibu nimeli highlight hapo juu
   
 20. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #20
  Apr 4, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,668
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  [
  Kitila,
  Hapa naomba nitofautiane nawe kama mwanasiasa mzoefu.
  Ninajua kuwa siasa ni sehemu muhimu ya kila mtu maana inagusa maisha yake moja kwa moja. Kwenye hali ngumu ya kisiasa kama ilivyo katika nchi yetu, the stuation we see cannot be avoided. Watu watazungumzia siasa mbele na nyuma maana hali yao ya maisha imeguswa na hii ni bahati maana ukiona hali kama hii ujue very soon yale ya Madagascar yanaweza kutokea.


  Hapa tuko wote. Nimekuelewa maana mimi nafagilia chama chako:). Hata hivyo ninapenda kila mwanamageuzi:D
   
Loading...