Lwakatare atakiwa kuachia ngazi kukinusuru chama na kuchafuka

Taswira

JF-Expert Member
Sep 23, 2012
1,198
447
Na Albinei Marcossy Wa Taasisi ya Raia na Haki za kisiasa na mwenendo wa Bunge( CPRW) amemtaka Mkuu wa usalama wa CHADEM wilfred Lwakatare kujiuzulu mara moja ili kupisha uchunguzi huru kwa jeshi la polisi.Pia kujiuzulu kwake kutasaidia kukiepusha chama na kuchafuka machoni kwa waanchi.
Kupitia Vyombo vya habari amesisitiza kuwa,Kitendo cha Lwakatare kuendelea kuwa mkuu wa usalama wa chadema na huku anamashitaka ya Ugaidi ni doa kwa chama na hakuleti picha nzuri kwa kuzingatia misingi ya utumishi.
 
Huyu si ndie tuliambiwa ametekwa na yeye?

je hili la Rwakatare kujiuzulu ndo msimamo wa CHADEMA au?
 
Hana lolote huyu jamaa,katumwa huyu na magamba!CPRW mnatafuta umaarufu kwa mgongo wa chadema
 
Kama tuhuma zinzomkabiri zingekuwa japo na 2% ya ukweli angekuwa sahihi!!!

Kama ndo mission yao hiyo imekula kwao!! "Lwakatare ndie Afsa usalama CDM Taifa!!!" Otherwise mjinyonge!!!
 
Where is Pasco?

last time Tundu Lissu alisema hii kesi ni ya masaa matatu kwisha kazi
sasa naona imeanza new spin ya kum isolate Rwakatare na chama
halafu huyo anaeanzisha hii new spin ndo huyo tulieambiwa nae ni mwanaharakati ambae 'ametekwa'..
hajulikani alipo..
kuna dots hapa Pasco anaweza help connects....
 
Last edited by a moderator:
Hii ni siasa nyingine inafanywa na magamba dhidi ya CDM, welevu tunaelewa na kujua kila kitu, kwanza atuambie maana ya kufutwa kwa kesi hii wakati ishu ya dhamana ilikuwa itolewe uamuzi na kuifungua upya ikiwa na mashtaka yale yale??
HAWA JAMAA SKUWAHI KUWASKIA KABLA CJUI WANADEAL NA VITU GANI?
 
Kwa hiyo yeyote akitungiwa tu tuhuma na wapinzani wake basi aachie tu ngazi kienyeji?

This is nonsense!

Wapo wanaotakiwa kuachia ngazi Tanzania ambao uzembe, ufisadi, kutokuwajibika kwao kumekuwa dhahiri, siyo huyu ambae bado uchunguzi unaendelea kujua kulikoni
 
Kama anataka Lwakatare ajiuzuru basi pia uongozi wote wa juu wa CHADEMA ujiuzuru pending court case kwa sababu Lwakatare alikuwa anafanya kile ambacho kimekuwa sactioned by CHADEMA machinery.

Huwezi ukawa na kiongozi wa juu mwenye fikra za KISHETANI na systematically anafanya mambo ya KISHETANI bila party high office kufahamu otherwise hiyo ofisi itakuwa haina kiongozi makini.

Alichokuwa anakifanya Lwakatare ni methodical organised.
 
Na Albinei Marcossy Wa Taasisi ya Raia na Haki za kisiasa na mwenendo wa Bunge( ) amemtaka Mkuu wa usalama wa CHADEM wilfred Lwakatare kujiuzulu mara moja ili kupisha uchunguzi huru kwa jeshi la polisi.Pia kujiuzulu kwake kutasaidia kukiepusha chama na kuchafuka machoni kwa waanchi.
Kupitia Vyombo vya habari amesisitiza kuwa,Kitendo cha Lwakatare kuendelea kuwa mkuu wa usalama wa chadema na huku anamashitaka ya Ugaidi ni doa kwa chama na hakuleti picha nzuri kwa kuzingatia misingi ya utumishi.

Kama tuhuma zinazo mkabili zinge tolewa na chama chake (CHADEMA), nadhani ingekuwa sahihi Lwakatare kujiuzulu. Vinginevyo ni kuto shirikisha ubongo kwa tuhuma ambazo zimetolewa na taasisi pinzani kwa CHADEMA.

Hiyo KIHIYO ameshindwa kumwambia Kawambwa ajiuzulu kwa kuwa na shutuma za kweli na za wazi za watoto wetu kufanya vibaya kwenye mitihani ya kidacho cha nne, anakuja na hoja zisizo na mashiko kisa anaongoza Taasisi ya CPRW.

Maneno hayo akamwambie mkewe na sio wanaume wa shoka wanao pigania haki za waTanganyika.
 
Halafu huyu Albanie Marcossy ameibukia wapi wakati kuna watu walidai ametoweka.

Tanzania kila siku ina vituko, ambavyo vingi vingine ni vya kupikwa bila hata kuiva.
 
huyu ndo alikua anasisitiza watu waandamane kisa viongozi wa nchi wanakashifiwa. huyo ni ccm, kinacho muuma ni chadema na siyo lwakatare. Ajihuzulu kwanza hoseah kwa sababu ya richmond, hussein mwinyi kwa mabomu yaliyo lipuka, shukuru kawambwa kwa watoto wetu kufail halafu dhaifu ndo tuongee mengine. mia
 
Na Albinei Marcossy Wa Taasisi ya Raia na Haki za kisiasa na mwenendo wa Bunge( CPRW) amemtaka Mkuu wa usalama wa CHADEM wilfred Lwakatare kujiuzulu mara moja ili kupisha uchunguzi huru kwa jeshi la polisi.Pia kujiuzulu kwake kutasaidia kukiepusha chama na kuchafuka machoni kwa waanchi.
Kupitia Vyombo vya habari amesisitiza kuwa,Kitendo cha Lwakatare kuendelea kuwa mkuu wa usalama wa chadema na huku anamashitaka ya Ugaidi ni doa kwa chama na hakuleti picha nzuri kwa kuzingatia misingi ya utumishi.

Mbona akina Ingh'ondu, Kawambwa, Mulugho na wengineo wengi ndani ya CCM na Serikali yake wana tuhuma lukuki lakini hawajiuzulu. Wengine wana tuhuma mpaka za kuua wanyama pori kama tembo na faru na kusafirisha wanyama hai, na wengine wametishia kuwatwanga wenzao kweupe na kuwahamishia nchi jirani lakini wote hao bado wameng'ang'ania madaraka na hakuna wa kuwahoji ama kuwaambia waachie ngazi, ama kwao na kwa CCM hayo siyo mambo ya kumfanya awe na tuhuma?
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom