Lwakatare atakiwa kuachia ngazi kukinusuru chama na kuchafuka

Ujinga hauna shule, ukiwa mpumbavu hata kama utasoma hadi upate zile shahada za uzamivu kama ni mpumbavu utaendelea tu kuitwa Dr. Mpumbavu au Prof. Mpumbavu. Mbona swala la lwakatare mnalivalia sana njuga?? ajiuzulu kwa faida ya nani?? yaani maccm baada ya kuona kile kikosi cha mawakili nguli watano kimesimamia show sasa mnatapatapa na kuhangaika ili mpate kuhalalisha uhuni wenu. Subirini kwanza shauri liishe kisheria, si mmelipeleka wenyewe mahakamani, sasa kinachowawasha ni nini??. Subirini sheria ichukue mkondo wake, nyie maji mshayavulia nguo subirini kuyakoga msiweweseke, tulieni msubiri anguko lenu la kihistoria.
 
Ha ha ha haaaaaa issue ya Lwakatare imewabana masaburi cdm ile mbaya. Mzee wa domo lenye square za mraba 1,2000,000,000,0000 kimyaaa!. Oh tuiachie mahakama mara maandamano!. This time mading'a yanagonga bikini tu. Hakuna cha kamanda wala mgambo!. Na bado jamaa mahabusu hawajafunguka!
 
Ha ha ha haaaaaa issue ya Lwakatare imewabana masaburi cdm ile mbaya. Mzee wa domo lenye square za mraba 1,2000,000,000,0000 kimyaaa!. Oh tuiachie mahakama mara maandamano!. This time mading'a yanagonga bikini tu. Hakuna cha kamanda wala mgambo!. Na bado jamaa mahabusu hawajafunguka!

kweli KITAMBI HESHIMA, na KICHWA KIKUBWA NDO KUWA NA ALIKI NYINGI. naona haya uliyoyaandika umeshirikisha Tumbo badala ya kichwa pole sana.
 
Wanajuana hao.gaidi huyo hawezi kufanya kazi pekee yake.akina slaa na mbowe wanahusika.

Slaa amechanganyikiwa hajui afanye nini.lwakatare wakimtimua anachoma moto kibanda
anafichua siri zote.
 
Kama tuhuma zinzomkabiri zingekuwa japo na 2% ya ukweli angekuwa sahihi!!!

Kama ndo mission yao hiyo imekula kwao!! "Lwakatare ndie Afsa usalama CDM Taifa!!!" Otherwise mjinyonge!!!

Shame on you! Kama unaona tuhuma alizonazo sio za ukweli si uende mahakamani ukatoe ushahidi wa kumuokoa!! Unapiga kelele tu hapa JF na kufata mkumbo badala ya kufikiri kwa kichwa chako mwenyewe; sio kuacha watu wengine wafikiri kwa niaba yako. Eti "Afisa Usalama CDM Taifa".... hahahahahah. nadhani unafikiri kwa tumbo wewe. shame on you...
 
NADHANI MSOME KWANZA TAMKO LENYEWE:

CIVIL AND POLITICAL RIGHTS WATCH
The Citizens' Parliament watch
Leo Machi 21, 2013 TAARIFA KWA UMMA JUU YA HALI YA KISIASA NA USALAMA NCHINI Taarifa hii ni matokeo ya ufuatiliaji shughuli za kisiasa na mwenendo wa haki za Raia unaoendelea hivi sasa nchini kwa kipindi cha Januari hadi Machi hii 2013. Tumeshuhudia mwenendo usioridhisha nchini juu ya shughuli za kisiasa na haki za raia katika utekelezaji shughuli za umma na huduma za kijamii katika kujenga mustakabali wa pamoja na ustawi wan chi katika kipindi ambacho nchi imekuwa ikikabiliwa na changamoto za umasikini, maradhi na ukosefu wa huduma bora za jamii. Hata hivyo tumeona kuzungumzia mambo machache kwa leo ili kuipa changamoto serikali, Bunge na jamii kuangalia mambo hayo kwa jicho la pekee kama ifuatavyo: 1. Uhuru wa Kupata Habari: Kumekuwa na malalamiko miongoni mwa watuaji wa Televisheni nchini juu ya upatikanaji habari na mawimbi ya televisheni kuwa wengi wao wamelazimika kutopata habari kwa njia hiyo baada ya serikali kuzima mitambo ya analojia. Aidha vyombo kadhaa vya televisheni vimelelemika kushindwa kuwafikia watuaji wa huduma hiyo kwa kuwa wameshindwa kupata ving'amuzi kuwawezesha kutumia huduma hiyo. Kuna taarifa kuwa kuna ving'amuzi 500,000 tu kwa Dar es salaam mkoa wenye wakaazi zaidi ya milioni nne na ambapo kunakadiriwa kuwa na vizio vya televisheni 1.5 milioni. Hii ni sawa na kusema katika kila watu watatu wenye vizio vya televisheni ni mtu mmoja tu ndiye mwenye kupata mawasiliano leo baada ya serikali kuzima mitambo ya analojia huku wananchi wengi wakiwa hawana uwezo wa kifedha kununua ving'amuzi na au kuvilipia kila mwezi! Hata hivyo, Kwa mujibu wa 1bara ya 18 (1) Uhuru wa kupata, kutafuta na kutoa habari ni HAKI isiyo na mipaka kwa wa Tanzania. Pia hakuna sheria yoyote iliyotungwa na Bunge inayoharamisha aina yeyote ya teknolojia ya mawasiliano nchini, na hivyo kuzuia watumiaji wa analojia kupata habari na mawasiliano ni kinyume cha Katiba! Niwakumbushe pia kuwa kwa mujibu wa Katiba 1b. 8(1)b : Lengo kuu la serikali litakuwa ni Ustawi wa wananchi; na hivyo hatua za kudhibiti matumizi ya analojia na kutatiza haki za wananchi kupata habari ni kinyume cha matakwa ya uwepo wa Serikali kwa mujibu wa Katiba. Izingatiwe pia kuwa, wanaotaka kuendelea kutumika kwa Analojia hatupingi ujio wa Digitali. 2. Mwenendo wa Shughuli za Bunge: Tuanfahamu kuwa Baada ya kuvunjwa isivyo halali Kamati za bunge zimeundwa upya na kupewa majukumu yake. Pamoja na hatua hii tumeshuhudia pia kuwa Bunge limeendelea kuunda Kamati zenye kuchanganya majukumu bila kuzingatia Katiba ya Nchi. Hii ni pamoja na kuchanganya mambo ya Muungano nay ale yasiyomo kwenye majukumu ya Kamati na kuteua wajumbe wa Kamati wasio na sifa. a. Kwa mfano, Kamati za Bunge za Mahesabu ya Serikali za Mitaa na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Kamati hizi zinashughulikia mambo yasiyo ya Muungano lakini wajumbe wake ni pamoja na Wazanzibari ambao sasa wanapewa majukumu ya kujadili na kujihusisha na mambo yasiyowahusu. Katika Kamati ya masuala ya UKIMWI ambapo pia si ya Muungano, zaidi ya 20% ya wajumbe wake ni Wazanzibari, huku Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ikiwa ni 27.8% na ile ya TAMISEMI ikiwa na wajumbe wanne kati ya 18 toka Zanzibar. b. Kamati ingine ni ile ya Ardhi, Maliasili na Mazingira ambayo inajumusiha mambo ya Muungano na yasiyo ya Muungano. Ikumbukwe kuwa kwa Mujibu wa Katiba mambo ya Muungano ni Maliasili ya mafuta na au bidhaa za mafuta na gesi asilia tu, huku mengineyo yakiwa si ya Muungano. Hata hivyo Kamati hii imepewa wajumbe toka nchi mbili za Muungano. 3. Hivi sasa kuna tafrani isiyoeleweka vema juu ya hali ya usalama wa raia na viongozi huku tukishuhudia hali hiyo ikihusishwa na shughuli za Kisiasa na au harakati za watetezi wa Haki za binadamu na waandishi habari. Tafrani hii imetokana na kile kinachoonekana kuwa ni juhudi za kudhibiti uhuru wa vyombo vya habari na upashanaji habari Tanzania. Tunaona kutekwa, kuteswa na hata kuuwawa kwa wanahabari na wanaharakati ni muendelezo ule ule wa kubinywa uhuru wa habari nchini. Na hivyo suala hili linahusiana na maamuzi ya kuzimwa mitambo ya mawasiliano ya analojia kwa utaratibu na uharaka usiozingatia mahitaji na hali halisi ya jamii. a. Kwa hili la usalama wa wanaharakati wa waandishi tunaitaka serikali kuchukua hatua za dhati kuimarisha usalama wetu sote: hii ni pamoja na yenyewe kujisafisha kuhusishwa na kadhia hii. Kwa haraka ile ile inayoonekana kuchukuliwa dhidi ya watuhumiwa wa ugaidi dhidi ya mwandishi habari anayetajwa serikali ichukue hatua dhidi ya matukio yaliyokwisha tokea yakiwemo mauaji ya Mwangosi, kutekwa na kuteswa Dr. Steven Ulimboka na Absalom Kibanda na matukio mengine yaliyokwisha tolewa taarifa Polisi. b. Serikali itatujengea imani kujitoa katika kadhia ya kudhibiti uhuru wa habari na waandishi iwapo pia itasikiliza kilio cha wadau wa habari na wananchi juu ya kufungiwa gazeti la MwanaHALISI na kuzimwa mitambo ya ANALOJIA. 4. Uwajibikaji wa Viongozi; a. Kumekuwa na maoni mbalimbali baada ya matokeo mabaya ya mitihani ya kidato cha Nne mwaka 2012 na hivyo wengi wetu kumtaka Waziri anayehusika ajiuzuru kuonesha kujali na kuwajibika kwa yale yaliyotokea chini ya wizara anayoiongoza. Sisi tunaungana na wadau wote wanaoona umuhimu wa Waziri Shukuru Kawambwa na Naibu wake kujiuzuru, tena bila kusubiri maandamano ya umma kushinikiza. b. Tunajua kuna tuhuma mahakamani zinazomhusu Bw. Wilfred Rwakatale, Mbunge wa Zamani wa Bukoba na Mkurugenzi wa Usalama wa CHADEMA. Kwa mujibu wa tuhuma hizo Bw. Rwakatare anatuhumiwa kujihusisha na mambo yanayoharibu au kuhatarisha usalama wa raia nah ii ni kinyume cha matarajio ya raia kwa nafasi aliyonayo kwenye chama kikuu cha upinzani nchini na ambacho kinaongoza kambi rasmi ya upinzani Bungeni. Kwa hiyo tunatoa wito kuwa Bw. Rwakatare ajiuzuru. Hii sit u itasaidia kupisha uchunguzi huru wa Polisi na vyombo vingine vya dola bali pia itatoa nafasi kwa CHADEMA na wanachama wake kumchunguza Rwakatare na au kujichunguza kama chama na kuhusishwa kwake. Hii ni changamoto pia kwa chama ambacho mara zote kimekuwa mstari wa mbele kutaka viongozi kuwajibika bila hata kuhukumiwa na mahakama. 5. Uchochezi na kuhamasisha migawanyika nchini: Hii ni kwa kuzingatia kuwa mara kadhaa viongozi wa serikali yetu pamoja na wale wa chama kilichoko madarakani wamekuwa wakikaririwa kulalamika kuwa kuna watu wanawachochea wananchi kuvuruga amani. Tuhuma hizi zimekuwa zikilengwa zaidi kwa wanaharakati, wanahabari na viongozi wa kidini. Uchunguzi wetu umebaini kuwa miongoni mwa wachochezi wakubwa wa migawanyiko na chuki za kidini na kikabila ni baadhi ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi na serikali yake. Mfano mzuri ni ule wa ziara ya Alhaji Bulembo, Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi wa CCM Taifa na mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM. Matamshi yaliyonukuliwa na vyombo vya habari na vyanzo vingine yanamkariri Bw. Bulemboo akiwahamasisha wakazi wa Kanda ya Magharibi kujiepusha na chama kimoja cha kisiasa kwa madai ya kuwa ni kutoka kanda moja ya nchi na kuwa wote ni wa dini moja na kwamba wanahamasiha watu wa kanda nyingine kuandamana na kuhatarisha usalama wao huku wao na familia zao wakiwa salama makwao. Tunaitaka serikali kuchukua hatua zinazostahili kwa wanansiasa wa aina hii na kukemea matamshi ya kuwagawa raia kwa vigezo vyovyote vya kibaguzi hivi. Pia tunaitaka CCM ijitenge na viongozi na wanachama wake wenye mitazamo ya aina hii na kuhubiri mgawanyiko. 6. Gesi ya Mtwara: Tunakumbusha kuwa tafrani iliyoibuka mwishoni mwa mwaka 2012 na mwanzoni mwa mwaka huu kule Mtwara inaonekana kutopatiwa ufumbuzi na baadala yake kuwekwa kwenye propaganda za kisiasa zaidi. Madai ya wanaMtwara yamepotoshwa na hatua zilizochukuliwa kutatua changamoto zilizotokana na wanaMtwara kudai haki yao ya kushirikishwa katika matumizi ya rasilimali za nchi hazijatatua kiini cha mgogoro huo. Tunaiomba serikali iache kutumia propaganda na vyombo vya habari kupotosha ukweli juu ya kile kinachoendelea Mtwara na mipango ya matumizi ya gesi iliyogundulika. Tunatahadharisha kuwa migogoro juu ya gesi na mafuta duniani kote imeonekana kuwa ni migogogoro hatari kama ilivyo ya kidini na ukabila. Serikali ichukue hatua madhubuti kwa kukaa na wanaMtwara na kusikiliza hoja zao huku ikisitisha mipango ya uchimbaji gesi asilia hadi pale tunapokuwa na sera na sheria mahsusi kwa ajili hiyo. Mapendekezo Tumekuwa tukiainisha mambo humu na mapendekezo ya nini kifanyike papo hapo. Ni jukumu sasa kwa kila anayehusika achukue hatua bila kuchelea juu ya changamoto hizi kuiepusha nchi yetu na matatizo yasiyo ya lazima na kuweka mazingira sawia kwa ajili ya raia kupata haki zao na kujiendeleza huku tukijenga nchi bora tuitakayo: TANZANIA NI NCHI YETU SOTE! Imetolewa na Taasisi ya Raia ya Haki za Kisiasa na Mwenendo wa Bunge, CIVIL AND POLITICAL RIGHTS WATCH
Marcossy Albanie Mkurugenzi Mtendaji
 
Na Albinei Marcossy Wa Taasisi ya Raia na Haki za kisiasa na mwenendo wa Bunge( CPRW) amemtaka Mkuu wa usalama wa CHADEM wilfred Lwakatare kujiuzulu mara moja ili kupisha uchunguzi huru kwa jeshi la polisi.Pia kujiuzulu kwake kutasaidia kukiepusha chama na kuchafuka machoni kwa waanchi.
Kupitia Vyombo vya habari amesisitiza kuwa,Kitendo cha Lwakatare kuendelea kuwa mkuu wa usalama wa chadema na huku anamashitaka ya Ugaidi ni doa kwa chama na hakuleti picha nzuri kwa kuzingatia misingi ya utumishi.
afu nataka msaada kuhusu hawa watu wa usalama,mbna wanaogopwa sana.
 
Back
Top Bottom