Lwakatare atakiwa kuachia ngazi kukinusuru chama na kuchafuka | Page 6 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lwakatare atakiwa kuachia ngazi kukinusuru chama na kuchafuka

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Taswira, Mar 23, 2013.

 1. Taswira

  Taswira JF-Expert Member

  #1
  Mar 23, 2013
  Joined: Sep 23, 2012
  Messages: 1,198
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Na Albinei Marcossy Wa Taasisi ya Raia na Haki za kisiasa na mwenendo wa Bunge( CPRW) amemtaka Mkuu wa usalama wa CHADEM wilfred Lwakatare kujiuzulu mara moja ili kupisha uchunguzi huru kwa jeshi la polisi.Pia kujiuzulu kwake kutasaidia kukiepusha chama na kuchafuka machoni kwa waanchi.
  Kupitia Vyombo vya habari amesisitiza kuwa,Kitendo cha Lwakatare kuendelea kuwa mkuu wa usalama wa chadema na huku anamashitaka ya Ugaidi ni doa kwa chama na hakuleti picha nzuri kwa kuzingatia misingi ya utumishi.
   
 2. Mr Dhaifu

  Mr Dhaifu JF-Expert Member

  #101
  Mar 24, 2013
  Joined: Jul 14, 2012
  Messages: 775
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 45
  We gamba ugaidi upi hapo?
   
 3. J

  JERUSALEMU JF-Expert Member

  #102
  Mar 24, 2013
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 2,757
  Likes Received: 1,828
  Trophy Points: 280
  umejiunga kwa kubadili ID tarehe 22.3.2013 kufikia tarehe 24.3. 2013 ulikuwa na posts 63 zote against CHADEMA. masalia at work. hongera watakulipa vijisenti
   
 4. Mkullya Damu

  Mkullya Damu Member

  #103
  Mar 24, 2013
  Joined: Jul 18, 2012
  Messages: 81
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  He! Kumbe upo?
   
 5. M

  Maubero JF-Expert Member

  #104
  Mar 24, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 1,532
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Albinei Marcossy ameshatoka mafichoni?
   
 6. M

  Maubero JF-Expert Member

  #105
  Mar 24, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 1,532
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Albanie anaipenda chadema ndiyo maana katoa maoni haya.
   
 7. M

  Maubero JF-Expert Member

  #106
  Mar 24, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 1,532
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Atabadili ID tena
   
 8. MwanaDiwani

  MwanaDiwani JF-Expert Member

  #107
  Mar 24, 2013
  Joined: Mar 22, 2013
  Messages: 5,536
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  MASALIA ndiyo nini?.

  Kama wewe unalipwa vijisenti kutoka Mtaa wa Ufipa, usifikirie kila mmoja kama wewe.

  Jibu hoja, kama huna hoja usiumize videlo vyako kwenye keyboard/keypad. Press NEXT.
   
 9. M

  Maubero JF-Expert Member

  #108
  Mar 24, 2013
  Joined: Feb 21, 2013
  Messages: 1,532
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Pole sana.Naona TISS wamekuteka na wewe kisaikologia
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #109
  Mar 24, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,620
  Likes Received: 23,752
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mwanadiwani, kwanza sijawahi kujifanya msomi zaidi ya kesema nilipitia UDSM kitivo cha sheria, kwa muda wa miaka 4 ili tuu kutoa tongotongo za sheria, wala hata sikuwahi kusema nilipata nini!, wala sijawahi kueleza humu nimewahi kusoma nini tena, vyuo vipi na nilipata nini!.

  JF ni social forum, unazungumza the most comfortable language you feel bila kujali structure wala syntax, hapa ni informal communications kama tuu tunavyozungumza vijiweni!. Hapa hatufanyi formal communications wala presentation, hapa tunamwaga tuu nondo, ila nakupongeza, wewe ni mwalimu wa wito, born teacher, hivyo unaumia sana ukiona watu wa nakosea/kuchanganya lugha, sio vibaya ukifungua darasa hata humu jf, wanafunzi utatupata na tutajisajili tuingie class!
  Karibu!.
  Pasco.
   
 11. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #110
  Mar 24, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,620
  Likes Received: 23,752
  Trophy Points: 280
  Mkuu Azipa,
  Nakubaliana na wewe, kwa asilimia 100% kuwa kama raia mwema, unapojua jinai inataka kutendeka/imetendeka, unapaswa kutoa ripoti kwenye vyombo husika!. Kitendo cha kutoripoti ni kosa kisheria na unapaswa sio kuunganishwa "accesory" bali kwa kosa jingine dogo zaidi!. Hata hivyo, kuna watu wenye kinga ambao hata ukijua, na hujaripoti, hupaswi kushitakiwa, wala kutumiwa kama shahidi. Watu hawa ni Mke na mume na mzazi na mtoto, mwalimu na mwanafunzi, daktari na mgonjwa, padri na muumini wake na mwanasheria na mteja wake!, hii inaitwa "fidutiary relationship".

  Yaani mke hata akijua mumewe ni jambazi, hatarajiwi kushitakiwa na hata mumewe akishikwa, mke anapewa kinga ya kutolazimika kuja kutoa ushahidi, unless mke akiamua mwenyewe kumripoti mumewe kwa usalama wake, maana anaweza kuogapa kuwa siku moja anaweza kushikwa na kuuwawa!.

  Padri na muumini, mfano unaweza kukuta watesaji wa Dr. Ulimboka, Kibanda na wauawaji wa Prof. Jwani Mwaikusa, au wauaji wengine wowote, usikute walishaenda kanisani na kutubu madhambi yao kwa padri, hivyo anawajua, japo serikali inasisitiza mwenye taarifa alete, huyo padri licha ya kujua kwa kutopeleka taarifa yoyote, anakinga ya kutoshitakiwa, na hata zawadi ikitangazwa, akijitolea kuripoti, hatapaswa kuitwa kama shahidi!. Vivyo hivyo kwa daktari na mteja wake, mwalimu na mwanafunzi na mwanasheria na mteja wake.

  By now, Rwakatare, ameisha waambia kila kitu mawakili wake, A-Z, mawakili wake japo wanaujua ukweli halisi, bali ndio hao humshawishi mteja wao kukana kila kitu kwa sababu mfumo wetu wa sheria ni wa Mwuingereza, "innocent until proven guilt" na "the burden of proof lies with the prosecution" hivyo waipe serikali task ya "to prove beyond reasonable doubt" ile "astus reus" na "mens rea" ya jinai ya njama za utekaji nyara, imefanyika!. Ndio maana kuna wahalifu wengi tuu wanaachiwa kwa kukosekana ushahidi wa kutosha huku kiukweli wameitenda wao ile jinai husika!.

  Mara tuu baada ya tukio la kibanda, nilipandisha uzi kuhusu TISS yetu ilvyo hovyo hovyo modes wakaibania!, nilisema kitendo cha Mwingulu kutangaza anayo video ya mikakati ya chadema kupanga mauaji, alipaswa kutiwa ndani kuisaidia polisi kwa kitendo tuu cha kuutangazia umma, bila kwanza kulishirikisha jeshi la polisi!.

  Nilisema kitendo cha Membe, kutangaza maadui 11 na kuwa "ole wao", tiss walipaswa kuwajia ni kina nani, na chochote kibaya kikiwatokea, the first suspect shuld have been Membe!. Kwa vile alisema kuna waandishi wawili, in case Kibanda was one off, Membe alipaswa awe ndani kuisaidia polisi!.

  Nliwahi kusema humu jinsi jeshi letu la polisi lilivyo ovyo ovyo, hii kesi ya Rwakatare ni ushahidi wa wazi wa double standards, niliuliza kama kwa Ulimboka hadi majina walipewa, and they did nothing!, what chances kwamba kwa Kibanda they'll do something?!. Hivyo walipoimata tuu hiyo video, (japo naendelea kuisisitiza ni "bonafide genuine"), sasa ndio wamepatia "scape goat" wa maroroso yao, tena msishangae mashitaka yakibadilishwa na kumuunganisha ya Kibanda, kwa the principle ya "aliyekutwa na ngozi, ndiye aliyekula nyama!".

  Dr. Mwakyembe alitumiwa assassins na waliconfess under video recorded kwa kuficha sura zao!, Dr. akaupeleka huo mkanda (DVD) kwa Mkuu wa TISS, IGP na kusambaza copy kwa baadhi ya balozi ili just incase anything happens to him, wabaya wake wachukuliwe hatua!. Huyo porpotes assassin aliwataja waliomtuma na kutoa all details!. Hiyo confession ilipatikana kwa ahadi kuwa Dr. hatamchoma kwa polisi. Polisi wameipokea na hawakumhoji yoyote kati ya hao wabaya waliotajwa, wala hawakufanya uchunguzi wowote eti mpaka kwanza Dr amtaje huyo assassin, Dr. aligoma and nothing was done!, likaja tishio la ajali, Dr akapiga kelele polisi did nothing!, likaja tishio la sumu!, they did nothing!, ila hili la video tuu ya Rwakatare!, they are now doing everything!.

  How long sisi wananchi tutaendelea kutolerate this double standard ya jeshi letu la polisi?.

  God Knows!.

  Mungu Ibariki Tanzania!.

  Pasco.
   
 12. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #111
  Mar 24, 2013
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,488
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Huyo Marcosy ni MSENGEnyaji sana, watoto wetu walivyofelishwa na akina kawambwa mbona hakuonekana...!?
   
 13. T

  Thesi JF-Expert Member

  #112
  Mar 24, 2013
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  We umeshamhukumu Lwakatare kwamba anahusika na katumwa na viongozi wake. Kesi iko mahakamani subiri mtakavyoumbuka. Kumbuka Mungu naye yupo kuwaumbua waovu wanaowasingizia watu wema uovu.
   
 14. Nyakageni

  Nyakageni JF-Expert Member

  #113
  Mar 24, 2013
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 14,080
  Likes Received: 1,404
  Trophy Points: 280
  unauma na kupuliza mkuu Pasco
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. T

  Thesi JF-Expert Member

  #114
  Mar 24, 2013
  Joined: Aug 8, 2010
  Messages: 998
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kwa kuwa hii kesi inaonekana ni kesi ya kutungwa hakuna haja Lwakatare kujiuzulu. Akijiuzulu waliowatuma kina Ludovick, Mwampamba na wengine watakuwa wamefanikiwa katika propaganda yao. Najua mtu akifanya kosa kuna haja ya kujiuzulu lakini ukweli hii ni kesi ya kisiasa zaidi. Ukiona mtu mwenye makosa ya kawaida kabisa anafunguliwa mashitaka ya ugaidi ujue kuna bundi yuko nyuma ya kesi hii.
  Kwa kuwa lengo lao ni kuichafua CDM akijiuzulu pamoja na kwamba ni njia nzuri ya kuonyesha uwajibikaji lakini kwa hapa itakuwa ni kuwaachia waovu wenye malengo mabaya na taifa letu kuendeleza propaganda za kutugawa na kutukatisha tamaa kudai Tanzania iliyoendelea kiuchumi na kidemokrasi.
  Kwa kuwa mwelekeo wa kesi hii imeshaanza kuwageuka ccm na mawakala wake kinachotakiwa ni kukomaa na kuondoa giza la uongo walilotaka kutuletea juu ya uaminifu wa chama kinachoonekana kuonyesha mwanga katika kuleta mabadiliko katika nchi yetu CDM. Ni wazi ccm hapa walicheza propaganda mbaya mno kwa CDM kuliko zote walizowahi kuzitunga. Wengi walianza kuonyesha mashaka kwa CDM na ndio lilikuwa lengo la walioweka ile picha kwenye youtube. Ni wazi ukweli utakapojulikana kwenye hii kesi itaiimarisha CDM kuliko walivyodhani ccm. Kwa hiyo hakuna haja kurudi kule tulikoanza kutoka baada ya mwanga mdogo kuanza kuonekana kuwa ni picha ya kutungwa na mhusika mkuu ni Mwigulu Nchemba.
   
 16. Tukundane

  Tukundane JF-Expert Member

  #115
  Mar 24, 2013
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 8,625
  Likes Received: 2,955
  Trophy Points: 280
  Hakuna sababu yoyote ya msingi itakayo mfanya Lwakatale ajiuzulu.kwa sababu Lwakatele hajaifanyia kosa lolote CHADEMA wala CHADEMA haiamini kama Lwakatale amefanya kosa kama hilo ndiyo maana hakuna hata mwana CHADEMA yeyote awe kiongozi au mwanachama yeyote aliyekiri kuwa Lwakatare amefanya kosa hilo.CHADEMA inacho kiamini ni kwamba hiyo video na makosa yote anayoshitakiwa ni mchongo wa CCM na vyombo vyake vya usalama ndiyo maana mtuhumiwa kashitakiwa kwa kosa la ugaidi.Ugaindi ambao haujatokea mahali popote Tz yaani hata ule wakutafutiza ili wambandike nao imeshindikana ni sawa na jambazi ukamshitaki kwa kosa la ujambazi kosa ambalo hakulifanya wala halikufanyika mahali popote.CHADEMA hawamupelelezi Lwakatale wanao mupeleleza Lwakatale ni serekali ya CCM kwa kutumia vyombo vyake vya dole. CHADEMA nao wanafanya kazi ya kuipeleleza serekali ya ccm na vyombo vyake vya dola ili kubaini kuwa ni mbinu gani waliyoitumia ili kufanikisha kuchonga mchongo huo na ninani aliyeagiza ili kumunufaisha nani na kwa lengo lipi.swala la kujiuzulu lwakatare ili kupisha upelelezi huru wa polisi kama ndiyo itakuwa tiba ya kupatikana ukweli ambaye anapaswa kujiuzulu si lwakatare tu ni pamoja na ccm na viongozi wake kwa sababu wote wanapelelezana na kila mtu anayo haki ya kufanya upelelezi huru bila kuingiliwa na mtu yeyote.
   
 17. M

  MgonjwaUkimwi JF-Expert Member

  #116
  Mar 24, 2013
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 1,299
  Likes Received: 547
  Trophy Points: 280
  Samahani, statistical significance level a.k.a p-value inatakiwa iwe chini ya 0.5% ku prove hypothesis yako. Kwa mantiki hii utakuwa unatumbia kwamba statistically it is insignificant kusema kwamba jamaa ni magamba kwasababu p-value yake ni way above 0.5%.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #117
  Mar 24, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,620
  Likes Received: 23,752
  Trophy Points: 280
  Mkuu Nyakageni, siumi wala kupuliza bali nasimama kwenye kweli. Najua kila nikigusia tuu kuhusu "bonafide genuine" mlioaminishwa "its fake" na kuamini hivyo, lazima mtaniona mimi ndiye muongo!. Uzuri wa ukweli ndio huwa unasimama mpaka mwisho!.

  Pia nilisha watotoa wasiwasi siku nyingi kuwa "bonafide genuine" sio tiketi ya kukubaliwa ushahidi mahakamani, kuna mlolongo mrefu wa kupokea ushahidi, kanisome hapa Rwakatare Hawezi Kushitakiwa Kwa Ushahidi wa "You Tube ..., na hadi kufanyika "trial within trial" ili ku determine ushahidi fulani upokelewe au laa!.

  Pasco.
   
 19. Communist

  Communist JF-Expert Member

  #118
  Mar 24, 2013
  Joined: Jun 1, 2012
  Messages: 5,382
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Tuana kazi kweli na masalia. Lakini huu ni upepo tu.
   
 20. Baba V

  Baba V JF-Expert Member

  #119
  Mar 24, 2013
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 19,488
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  videlo...!?? salia hilo
   
 21. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #120
  Mar 24, 2013
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,620
  Likes Received: 23,752
  Trophy Points: 280
  Na utapita tuu!, tatizo ni ukiwa upepo mkali, unaweza kuvuruga vuruga tuu, ukiwa kimbuka, unaweza kuezua hata paa!, lakini ukiwa tsunami, unasomba kila kitu!.
  Pasco.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...