Lwakatare aitisha press conference makao makuu CHADEMA

Status
Not open for further replies.

HAMY-D

JF-Expert Member
Sep 18, 2011
7,149
3,817
Habari wana-JF?

Leo majira saa 4 asubuhi bwana Lwakatare ambae ni mkurugenzi wa ulinzi na usalama CHADEMA atakuwa na mazungumzo na waandishi wa habari, ajenda ikiwa kuhusiana na sakata zima la kesi yake.

My take;

Huyu bwana Lwakatare akumbuke hayuko huru, ametoka kwa dhamana tu, pia najua kwa sasa huko CHADEMA kuna shehena ya watu walio bobea kwa siasa za majitaka na siasa uchwara.

Aidha, kwa siasa zao hizo 'reja reja' watamshinikiza huyu bwana Lwakatare aichafue CCM kwa makusudi kabisa kwamba imehusika na kuunda tuhuma hizo.

Rai yangu kwa bwana Lwakatare, asikubali kwa namna yeyote kushinikizwa kuwa suala la kesi yake ni la kichama, kama minong'ono mingi ilivyo.

Hili lilitokea hata mahakamani alivyo achiwa kwa dhamana, kwani kuna vijana wa CHADEMA walisikika wakisema mipango ya CCM imeshindwa.

Lwakatare, be smart.
 
Relax, pressure ya nini, ina maana umesahau kuwa kale kamovie mlichomtengenezea cha ugaidi kilitupiliwa mbali? Hivyo hapo ana haki ya kuuelezea ulimwengu huo uhuni nani aliufanya na kujisafisha.
 
We muuaji, mzushi, gaidi muongo na mnafiki mkubwa Mwigulu Nchemba ni bora tu unyamaze baada ya kufanya uharamia wako. Unyama wako wa kupandikiza haukutosha kumtia hatiani Lwakatare kajaribu kutengeneza sinema nyingine pumbavu mkubwa wee.
 
Habari wana-JF?

Leo majira saa 4 asubuhi bwana Lwakatare ambae ni mkurugenzi wa ulinzi na usalama CHADEMA atakuwa na mazungumzo na waandishi wa habari, ajenda ikiwa kuhusiana na sakata zima la kesi yake.

My take;

Huyu bwana Lwakatare akumbuke hayuko huru, ametoka kwa dhamana tu, pia najua kwa sasa huko CHADEMA kuna shehena ya watu walio bobea kwa siasa za majitaka na siasa uchwara.

Aidha, kwa siasa zao hizo 'reja reja' watamshinikiza huyu bwana Lwakatare aichafue CCM kwa makusudi kabisa kwamba imehusika na kuunda tuhuma hizo.

Rai yangu kwa bwana Lwakatare, asikubali kwa namna yeyote kushinikizwa kuwa suala la kesi yake ni la kichama, kama minong'ono mingi ilivyo.

Hili lilitokea hata mahakamani alivyo achiwa kwa dhamana, kwani kuna vijana wa CHADEMA walisikika wakisema mipango ya CCM imeshindwa.

Lwakatare, be smart.
...He! hivi CCM bado ni safi? kuna mtu anaweza kuichafua zaidi ya ilivyochafuka?
 
Vipi Gamba leo linakuwasha?-fear of uncertainity,unaliogopa jiwe ambalo atalitoa leo lwakatare....!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Unajihami bro! Ngoja tuwake.k.e.t.e leo. Kila kitu kitawekwa wazi. Pole yenu magamba.

Cc: mwigulu, mwampamba, shonza, chama, ritz, bungeni, utaifa kwanza, chris lukosi na le mutuz.
 
Unataka kusema kuwa yeye Lwakatare ni bogozo kiasi kwamba hajui lipi la kuongea na lipi la kuacha, hadi awe spoon-fed?
Acha kuwanga bana!

Mkuu, ukiwekwa kati na mtu kama Marando akakushinikiza kusema uongo ni rahisi sana kushawishika, nilikuwa nampa tu angalizo.
 
mkuu mbona unawashwa sana? Heading unasema aitisha, then kwenye content unatuambia ataitisha....

Si usubiri hiyo saa nne, kuliko kujifanya Shekh Yahaya?

Soma kati ya mistari wewe acha kukurupuka, heading nimesema 'aitisha', ila content nimesema 'atakuwa'. Nadhani unajua kama kuna tofauti kubwa kati ya kuitisha na kufanikiwa kupata ulicho ita.
 
Yule kijana msaidizi wa Lwakatare aliyekuwa anaonyesha alama ya Chadema mahakamani naye atakuwepo?
 
Muache aongee anavyojua kabisa ila tumshukuru Mungu taifa limeshamfahamu ni matumaini yangu kila mtanzania atachukua tahadhari na mtu huyu muovu.
 
Relax, pressure ya nini, ina maana umesahau kuwa kale kamovie mlichomtengenezea cha ugaidi kilitupiliwa mbali? Hivyo hapo ana haki ya kuuelezea ulimwengu huo uhuni nani aliufanya na kujisafisha.

Lakini nimetoa tahadhali kwake asije akahusisha suala la kesi yake na kulifanya kichama (kitaasisi), nadhani umenielewa?
 
Umekosa story? sijaelewa huu uzi unamaanisha nini? think great coz this is the home of great thinker.
 
Kuchafua ccm? Ccm tayari ni kokoro mfu..inakuuma nini wewe Lwakatare kuweka kila kitu bayana? MWIGULU SAVIMBI mwaka huu utakimbilia UHAMISHONI
 
...He! hivi CCM bado ni safi? kuna mtu anaweza kuichafua zaidi ya ilivyochafuka?

Watanzania bado wana matumaini nayo na wako tayari kukifia chama chao, kwani chama hiki kimetoa taifa hili mbali.

Wewe na wenzako wachache ndio wenye mawazo kuwa CCM ni chafu.

Jamani, kama mbinguni tu palipatikana na usaliti (bwana Ibilisi), sembuse CCM?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom