Lwakatare aachiwa huru kisha kukamatwa hapo hapo kwa kosa lingine

Kumbe JF imejaa mambumbumbu wa sheria kiasi hiki? Lwakatare anaweza akaachiwa hata kwa mara ya pili na polisi wakamkamata tena na hili si Lwakatare kama ndio mtu wa kwanza kufanyiwa hivi.

Hata katika kesi nyingine ushahidi unatakiwa uwe umekamilika baada ya kipindi fulani na usipokamilika Mahakama inamuachia huru mtuhumiwa na Polisi inamkamata tena na zile siku za kukamilisha ushahidi zinaanza kuhesabiwa upya, hii inategemea nature ya kesi inakuwa ina interest zipi na waendesha mashtaka.
Mkuu naomba siginecha yako niibandike ofisin!!!!!!
 
Ameachiwa na youtube criminal court,akakamatwa tena na ccmpolice force,kwa kosa la kukusanyika youtube kinyume cha matakwa ya ccm. Hivi kama mahakama zetu zimefikia kutumia vikatuni kama ushahidi wa ugaidi mbona kazi tunayo?ndio maana wamarekani wa FBI kwa kuelewa uozo wa bongo zetu walituchorea kikatuni kisicho na tangible reflection,na kutuacha tuhangaike nacho!!!!kwekwe kwe kwe kwe kweee,ile hadithi ya vichaa waliochorewa picha ya mlango ukutani na wakaigombea kupita hapo iliihusu tanzania na vyombo vyetu vya dola,mvuta bange mmoja tu katengeneza upuzi wake huko kaubandika youtube,kina madelu wameugombea na kuuona lulu yao kisiasa!! Kweli safari bado ndefu ssssana.
...Hii burudani jamani!
 
Kwa stage hapo ilipo, mahakama haina uwezo wa kumuachia kutokana na kutokuona hatia yoyote, kwa sababu mpaka sasa kesi hiyo bado haijasikilizwa ili kuestablish hatia au la!. Hata hivyo uwezo wa mahakama kuifuta kesi kabla haijasikilizwa ni endapo ikitokea mmoja wa washtakiwa kutokuwepo duniani kwa sababu yoyote ile, ndipo mahakama hapo hapo huifuta kesi.

Ikumbukwe, amefikishwa mahakani ili tuu kukidhi matakwa ya kisheria ya mtu kutokushikiliwa zaidi ya saa 24 bila kufikishwa mahakamani, ila kwa nature ya mashitaka anayotuhumiwa nayo ya ugaidi, then mahakama ya Kisutu, sio mahakama yenye "competent jurisdiction" kusikiliza shauri hilo, hivyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo, hivyo hapo Kisutu, kesi inatajwa tuu, upelelezi ukikamilika, inahamishiwa Mahakama Kuu, ambayo kisheria inaelezwa kuwa na "pecuniary jurisdiction" kusikiliza shauri lolote!.

Kwa stage hii ilipo, mwenye uwezo wa kuifuta kesi ni DPP tuu. Katika mfumo wetu wa utawala, mtu mwenye mamlaka makubwa kabisa ya kisheria kuliko hata mkuu wa nchi ni DPP, anamamlaka ya kuamua kupeleka mashitaka mahakamani au laa bila kuingiliwa na chombo chochote, na pia ana mamlaka ya kuingilia kesi yoyote ya jinai, ikiwa mahakama yoyote, au hatua yoyote kabla ya hukumu na kuifuta kwa kutuma hati inaitwa "nolle proseque!' na haruhusiwa kuhojiwa na yoyote, popote.

Spika wa bunge ana mamlaka tuu ya uendeshaji bunge, na bunge linamamlaka ya kutunga tuu sheria, mwenye mamlaka ya kuipitisha sheria yoyote ni rais "accent" hivyo bunge likipitisha sheria, rais ana mamlaka ya kuikataa na hapo hapo kulivunjilia mbali bunge!.

Jaji Mkuu ana mamlaka ya kutoa "capital punishment" lakini hukumu hiyo haiwezi kutekelezwa mpaka rais asaini!. Pia ni rais ndie anayemteua Jaji Mkuu wa Tanzania japo hawezi kufuta kazi!. Hivyo "the doctrine of checks and balances kati ya mihimili mikuu ya dola ni kiini macho tuu!".
Pasco.

Hayo ya Dpp kuwa the only person anayeweza futa kesi bongo hii yapo vitabuni tu km angekuwa ana uwezo huo mafisadi wote wangekuwa behind bars kitambo tu. Halafu kumbuka huyo Dpp ni mteule wa rais sasa utaona uwajibikaji wake unabanwa kiasi gani. Uwezo wake unaonekana pale wapinzani, wanyonge na maskini wanapotengenezewa kesi na kubambikiwa mashtaka ya uongo lkn ile layer ya mafisadi papa aka wanamtandao hawezi kuwagusa.
 
Kwa niaba ya wapenzi wa JF nakuomba uombe radhi kwa lugha uliyotumia hapo juu as bolded, elewa kuwa JF Members siyo wote wanasheria kama wewe, Ukienda Muhimbili National Hospital Usidhani wote walioenda kama wewe wanaugonjwa kama wako, kwa hili unakitu kinaitwa Parochial Mind, and that is very bad you are an egoistic person.
yuko right

tupo mambumbumbu wengi wa kisheria

tunachohitaji ni yeye kutoa shule sio kusema something we do know

wengine humu ni wanamuziki, wanasiasa, wachawi, wanga, wakulima, wanafizikia, madaktari nk.... si lazima tujue sheria ili tuishi

matola anachohitaji kujua ni kwamba hata yeye ni mbumbumbu wa eneo fulani na asimind wakimtwanga notice ya umbumbumbu
 
Kwa niaba ya wapenzi wa JF nakuomba uombe radhi kwa lugha uliyotumia hapo juu as bolded, elewa kuwa JF Members siyo wote wanasheria kama wewe, Ukienda Muhimbili National Hospital Usidhani wote walioenda kama wewe wanaugonjwa kama wako, kwa hili unakitu kinaitwa Parochial Mind, and that is very bad you are an egoistic person.
dada upo sahihi kabisa, mie sijui kutukana nami ningemtusi, nisaidien jaman!!
 
Nimesoma michango ya watu wote humu ndani sikuwa nimepata ninachotaka,ila nilipofika kwako nimepata
nilichotaka kijibiwe.Asante mkuu hapa umemaliza ni kusubiri tu way forward' Naongeza LIKE'
..pamoja kamanda...
 
Basi mwombeeni kama ameanza kupangua kesi moja. Mi nafikiri serikali ichunguze mambo haya vizuri maana yanatia hofu.


Serikali unayotaka ichunguze tatizo ni hii hapa:

RAIS MWISLAM, MAKAMU WA RAIS MWISLAMU, JAJI MKUU MWISLAMU, MKUU WA USALAMA WA TAIFA MWISLAM,
IGP MWISILAM WAZIRI WA ULINZI MWISLAM, WAKUU WA MIKOA 19 KATI YA 28 NI WAISLAM,
MATAJIRI 9 KATI YA 10 NI WAISLAM, 78% YA WAJUMBE WA KAMATI KUU YA CCM NI WAISLAM,
81% YA WAJUMBE WA TUME YA KATIBA MPYA NI WAISLAM. 66% YA WAKUU WA WILAYA NI WAISLAM

Ukitaka wachunguze kitu ni lazima kiwe asilimia 70, 80 au 90 hivi cha kiislamu.
 
polisi wanatakiwa kujua kuwa kikojozi hapati usingizi ugenini. huko wanakotaka kuingizwa na kina Mwigulu ni ugenini wakati wenyewe wanajijua ni vikojozi tangu zamani. watang'aa macho mpaka asubuhi maana wakisinzia tu washalimwaga. Wakumbuke pia kuwa kuna wakati wakuubali ukweli kuwa hata bibi alikuwa binti CCM ashakuwa mzee ule uzuri wake wa kuimbwa mashuleni ushaisha waachane nae wajitegemee. Nawakilisha tu.
 
Hakika wataangamia mkuu, shetani hana nguvu kamwe..
Naapa chini ya Mbingu na Ardhi kamwe Shetani hatamshinda Mungu.

Kama Daudi alimuua Goliathi kwa jiwe katu Mashetani hawa wanaotaka kuichafua Chadema hawatafanikiwa na wataangamia.

Naapa kwa Mungu aliye hai yeyote aliyeshiriki kutunga mpango huu mchafu hatabaki salama.

Naapa kwa Mungu Mkuu muumba kila kitu kwamba kila aliyeshiriki kutunga uchafu huu lazima ataumbuka siku si nyingi na ataomba radhi hadharani.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Anania akapasuka matumbo mbele ya madhabahu kwamba wahalifu hawa watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Herode akadondoka juu ya kiti cha kifalme na mwili wake kuliwa na siafu kwamba waovu waliotunga mbinu hii watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu wa Abraham,Isaka na Yakobo kwamba watu hawa hawataweza kuendelea kuharibu Taifa letu kwa uchochezi wao bali watakipata sawasawa kile kiwapatacho watu wasiomjua Mungu.

Naapa kwa Mungu ambaye jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO kwamba Shetani kamwe hatajitwalia utukufu.

Wao wana Baali na Chadema wana Mungu kamwe Baali hawezi kumshinda Mungu.
 
Lwakatare hana kesi, hata ukipitia makosa manne ambayo wamembabikizia, hayawezi kuthibitishwa kwenye mahakama yoyote ile. Kadiri siku zinavyokwenda waache hawa watawala ghadhabu ya mwenye haki izidi kuwaadhibu na wataaibika sana katika uso wa ulimwengu huu!
 
Kwa tukio hill la Lwakatare sasa waTZ ndiyo tunapata ushahidi usio na shaka yoyote kuwa Jeshi hilo linafanya kazi zake kwa maagizo ya Ikulu.

Iweje issue ya Ulimboka wameshindwa kumkamata Ramadhan Ighondu, ambapo ushshidi wa kutosha wa kumhusisha na tukio la Ulimboka upo na badala yake wamedhupalia issue ya Lwakatare, kisa ndivyo mkulu anavyotaka kwa kuwa alishawahakikishia wana CCM wenzie kule Kigoma kuwa ni lazima nchi hii ataikabidhi kwa kiongozi wa CCM mwaka 2015!!!!!
 
Back
Top Bottom