Lwakatare aachiwa huru kisha kukamatwa hapo hapo kwa kosa lingine

Naapa chini ya Mbingu na Ardhi kamwe Shetani hatamshinda Mungu.

Kama Daudi alimuua Goliathi kwa jiwe katu Mashetani hawa wanaotaka kuichafua Chadema hawatafanikiwa na wataangamia.

Naapa kwa Mungu aliye hai yeyote aliyeshiriki kutunga mpango huu mchafu hatabaki salama.

Naapa kwa Mungu Mkuu muumba kila kitu kwamba kila aliyeshiriki kutunga uchafu huu lazima ataumbuka siku si nyingi na ataomba radhi hadharani.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Anania akapasuka matumbo mbele ya madhabahu kwamba wahalifu hawa watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu aliyemwangamiza Herode akadondoka juu ya kiti cha kifalme na mwili wake kuliwa na siafu kwamba waovu waliotunga mbinu hii watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa Mungu wa Abraham,Isaka na Yakobo kwamba watu hawa hawataweza kuendelea kuharibu Taifa letu kwa uchochezi wao bali watakipata sawasawa kile kiwapatacho watu wasiomjua Mungu.

Naapa kwa Mungu ambaye jina lake ni NIKO AMBAYE NIKO kwamba Shetani kamwe hatajitwalia utukufu.

Wao wana Baali na Chadema wana Mungu kamwe Baali hawezi kumshinda Mungu.
 
kuachiwa na kukamatwa maana yake ni kwamba kuna makosa yaliyokuwa yanampa dhamana lakini amekamatwa tena kwa yale yasiyompa dhamana sio kwamba hana hatia
 
..kiongozi hii inawezekana, kama polisi hawakujipanga kuandaa kesi vizuri ukifika mahakamani unaachiwa huru ila kwakuwa polisi wanatambua kosa lao wanakukamata palepale unapotoka nje ya mahakama ili wakaandae kesi upya na wanapunguza usumbufu wa kukutafuta tena. ukibaki ndani hawakukamati maana ni eneo la muhimili mwingine wa dola

Nimesoma michango ya watu wote humu ndani sikuwa nimepata ninachotaka,ila nilipofika kwako nimepata
nilichotaka kijibiwe.Asante mkuu hapa umemaliza ni kusubiri tu way forward' Naongeza LIKE'
 
Lwakatale amefutiwa mashtaka yanayomkabili na kukamatwa tena,kisha akafungulia mashtaka upya.
Kufutwa kwa mashtaka ya Lwakatale inatokana na makosa yaliyofanywa na upande wa serikali, na kumfanya DPP kufuta mashtaka hayo.

 
Hizi taarifa zenu wana_jf hasa wana_CDM mliopo hapo Kisutu hazikati kiu. Hebu mseme kinaga ubaga. Mungu yu upande wetu cdm tutashinda.
 
Kumbe JF imejaa mambumbumbu wa sheria kiasi hiki? Lwakatare anaweza akaachiwa hata kwa mara ya pili na polisi wakamkamata tena na hili si Lwakatare kama ndio mtu wa kwanza kufanyiwa hivi.

Hata katika kesi nyingine ushahidi unatakiwa uwe umekamilika baada ya kipindi fulani na usipokamilika Mahakama inamuachia huru mtuhumiwa na Polisi inamkamata tena na zile siku za kukamilisha ushahidi zinaanza kuhesabiwa upya, hii inategemea nature ya kesi inakuwa ina interest zipi na waendesha mashtaka.

Umeisoma comment ya kwanza ya michael p aweda ?
 
Kama ameachiwa huru, mana yake yale makosa manne yote aliyoshtakiwa nayo mwanzo hayajaweza kuthibitishwa,
Sasa kakamatwa tena kwa kosa gani?, Jamaa wameweka clip nyingine mpya you tube?

...No ipo kwa Zoka wanamalizia editing.
 
Hasidi hana sababu na mwisho wa fedheha ni aibu maana Lwakatareameshikiwa na polisi wakaanza kutafuta waaamshtaki vipi maana hawana facts ilawanatii amri za TISS sasa wanataabika na Lwakatare. Time will tell as time goeson. Ndiyo maana suluhisho la uonevu uliojaa ulimwengu mzima kuanzi Middle Eastna kwingineko ni Armageddon tu basi kwa Tarumbeta kupulizwa na Kiti cha Hukumukuchukua Mahala Pake. Someni Zaburi ya 37:7;9;11 & 29 na Revelation 21:1-5Amina
 
naapa chini ya mbingu na ardhi kamwe shetani hatamshinda mungu.

Kama daudi alimuua goliathi kwa jiwe katu mashetani hawa wanaotaka kuichafua chadema hawatafanikiwa na wataangamia.

Naapa kwa mungu aliye hai yeyote aliyeshiriki kutunga mpango huu mchafu hatabaki salama.

Naapa kwa mungu mkuu muumba kila kitu kwamba kila aliyeshiriki kutunga uchafu huu lazima ataumbuka siku si nyingi na ataomba radhi hadharani.

Naapa kwa mungu aliyemwangamiza anania akapasuka matumbo mbele ya madhabahu kwamba wahalifu hawa watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa mungu aliyemwangamiza herode akadondoka juu ya kiti cha kifalme na mwili wake kuliwa na siafu kwamba waovu waliotunga mbinu hii watafuata njia hiyo hiyo.

Naapa kwa mungu wa abraham,isaka na yakobo kwamba watu hawa hawataweza kuendelea kuharibu taifa letu kwa uchochezi wao bali watakipata sawasawa kile kiwapatacho watu wasiomjua mungu.

Naapa kwa mungu ambaye jina lake ni niko ambaye niko kwamba shetani kamwe hatajitwalia utukufu.

Wao wana baali na chadema wana mungu kamwe baali hawezi kumshinda mungu.
inshaallah...
 
Lwakatale amefutiwa mashtaka yanayomkabili na kukamatwa tena,kisha akafungulia mashtaka upya.
Kufutwa kwa mashtaka ya Lwakatale inatokana na makosa yaliyofanywa na upande wa serikali, na kumfanya DPP kufuta mashtaka hayo.

...Naomba msaada jamani. Hivi mashitaka yakifutwa inaruhusiwa kurudia kushitaki kwa mashtaka hayohayo yaliyofutwa baadaye? au itabidi watunge mengine.
 
Kumbe JF imejaa mambumbumbu wa sheria kiasi hiki? Lwakatare anaweza akaachiwa hata kwa mara ya pili na polisi wakamkamata tena na hili si Lwakatare kama ndio mtu wa kwanza kufanyiwa hivi.

Hata katika kesi nyingine ushahidi unatakiwa uwe umekamilika baada ya kipindi fulani na usipokamilika Mahakama inamuachia huru mtuhumiwa na Polisi inamkamata tena na zile siku za kukamilisha ushahidi zinaanza kuhesabiwa upya, hii inategemea nature ya kesi inakuwa ina interest zipi na waendesha mashtaka.

Kwa niaba ya wapenzi wa JF nakuomba uombe radhi kwa lugha uliyotumia hapo juu as bolded, elewa kuwa JF Members siyo wote wanasheria kama wewe, Ukienda Muhimbili National Hospital Usidhani wote walioenda kama wewe wanaugonjwa kama wako, kwa hili unakitu kinaitwa Parochial Mind, and that is very bad you are an egoistic person.
 
waTZ kwanza tunapaswa kumshukuru sana Mungu hata kwa hiyo hali ya kuachiwa kwa muda kwa Lwakatare.

Tokea mwanzo ilipoibuka hii kesi ya kufikirika nilisema hiyo kesi imewezeksna tu kufunguliwa kutokana na hako kacoalition kalikoundwa baina ya Jeshi la Polisi, TISS na CCM.

Lakini waTZ tunalazimika kuushukuru sana mhimili wetu wa mahakama kwa kukataa kujiunga na hiyo coalition.

Kwa maana hiyo hata kama Jeshi la Polisi limeamua kumkamata tena Lwakatare hayo yatakuwa maagizo ya ofisi 2, moja ipo Magogoni na nyingine ipo Lumumba.

Lakini hao watu wakumbuke msemo mmoja wa kiswahili unsosema mwisho wa ubaya aibu!!

Wao wana madaraka na pesa na sisi tuna Mungu. Hakuna nguvu yoyote ya kidunia inayoweza kushinda uwezo wa Mungu!!!
 
Back
Top Bottom