LWAITAMA aunguruma juu ya WARAKA wa LEMA kwa Rais Jk!

Nampa pole za dhati Ndugu Godbless Lema. Nilikuwa pale Viwanja vya Jangwani Dar es salaam siku ya Uzinduzi wa Vuguvugu la Mabadiriko (Movement For Change). Maelfu na maelfu ya vijana walionyesha mapenzi makubwa na huruma nyingi kwake.

Walionyesha kukubaliana na dhana iliyonyuma ya Waraka wa Lema kuwa Mh Lema alidhulumiwa kwa kunyang'anywa Ubunge. Ushauri wangu kwake Mh Lema ni kuwa aandike Waraka wa Pili wa Lema na katika waraka huu wa pili aeleze kwa kirefu na kwa uwazi juu ya mkutano wake na Rais anaosema ulifanyika Osterbay 2010: nani aliomba uwepo mkutano, ulifanyika wapi, na yepi yaliyozungumzwa.

Namuomba aweke wazi mazungumzo yao na mazingira ya kufanyika kwake. Katika mahakama hii ya nguvu ya umma ni vizuri umma ujue kwa kina kwa nini Mh Lema anadhani anaweza akadhurika ikiwa mkuu amekasirishwa na yeye Lema kutotekeleza waliyokubaliana Osterbay 2010.

Ndugu yangu Nico Eatlawe nakuomba uusome Waraka wa Lema kama unavyosoma Waraka wa Mitume wa Yesu, "between the lines," na pole vile ukuwepo pale Jangwani Dar es Salaam maana vijana kwa maelfu na maelfu wamemkubali Mh. Lema na Waraka wake ni njia nzuri ya kujiami dhidi ya madhara yanayoweza kumpata kutokana na kukubalika huko.

Kukubalika kwa Mh. Lema Arusha Mjini sasa kumesambaa nchi nzima baada ya kunyanganywa Ubunge na ili si jambo dogo. Kumbuka Mh Zitto Kabwe umaarufu wake uliubuka kutokana na kusimamishwa Ubunge tu kwa muda lakini Mh. Lema amepigwa na kudhalilishwa na polisi , amewekwa rumande na Mh. Livingstone Lusinde alikejeli kuwekwa kwake rumande.

Na mwisho wa siku akanyanyanganywa Ubunge mara tu baada ya kuonyesha anapendwa pia hata Arumeru Mashariki. Huyu wako wapambe wa wakubwa wa nchi bila shaka wanaweza wakajituma kumwenyesha hata sumu. Tusipuze uwezekano huu. Tumpe moyo Mh Lema.

Kumbuka mambao mbali mbali yaliyowahi kuwasibu msusuru wa watu mbali mbali toka Gavana Balali, Harrison Makyembe, Rostam Aziz hadi Edward Lowasa...Mh. Lema anapendwa sana na vijana wa kijiweni na wanamwamini...Tumpe Mh Lema moyo aendelee kuwaelimisha hawa vijana wa kijiweni...

Tusimzidishie uchungu wake wa haki kwa kudhulumiwa na uonevu wote ambao amepata hadi sasa kwa kumuhukumu hata kabla hajatusimulia kisa kizima tangu Osterbay Oktoba 2010 hadi Arusha tarehe 5 Januari 2011 hadi juzi kuvuliwa ubunge katika mazingira ya kisheria tatanishi.

Mungu si Athumnai bwana, ipo siku ukweli utashinda uzandiki!!! Ishara kuu yenye kuashiria nyota njema ni kukubalika kwa Mh. Lema kwa maelfu na maelfu ya vijana wa nchi hii.


Mwl. Lwaitama

Hivi haujagundua Lwaitama anamtusi Lema? na anawatusi vijana wanaoshabikia pasi kujua ukweli?

unamjua Lwaitama?
 
Mkuu Yericko,

Nilidhani na wewe ni great thinker kumbe hamna kitu unapoteza muda wako kusikiliza ujinga wa Lema kweli Tanzania ni masikini si kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya wananchi wake kuwaamini wanasiasa wa hovyo.



Ngongo!

Hv wewe unakuwaga na akili timamu kweli?
Ama mawazo ya kutafakari kwako na kujua kinachozungumziwa ndiyo tabu?
Msome tena Y. Nyerere anazungumzia nini hasa!

Member mingine mizigo kweli kweli!
 
Mkuu Yericko, Nilidhani na wewe ni great thinker kumbe hamna kitu unapoteza muda wako kusikiliza ujinga wa Lema kweli Tanzania ni masikini si kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya wananchi wake kuwaamini wanasiasa wa hovyo.
Watu waliolambishwa tamu na CCM wapepoteza uwezo wa sense organ zote kufanya kazi, hawasikii, hawaoni, hawanusi, wakilamba hawahisi radha yoyote, ngozi ndo imekufa kabisaa! Ningekuwa natazamana uso kwa uso na wewe uvumulivu ungenishinda, nahisi ningetapika kwa hasira.
 
Hapa naomba niwe msemaji wa lema! Alishawahi sema walidiscuss ugombea wake via ccm na kupewa cheo akapuuzia!
 
Waraka wa Lema unaibua hisia mbaya sana kuhusu viongozi wote wa CCM na serikali yake. Unajenga hisia kwamba labda viongizi wengi (kama sio wote) wamepata vyeo kwa mtindo huu wa ki-oysterbay. Na watu wanaweza ku-test hiyo theory kwa kuangalia kigugumizi kinachowapata CCM kwenye suala la kuwajibika (accountability).

Bado naamini lilikuwa kosa kwa rais kutaja 'miaka miwili isingewezekana kufanya mkutano mkubwa wa kimataifa Arusha'. Haikuwa lazima sana sana ni kuleta mgogoro.

Nashangaa mkutano wa Bank ya Africa ni mkubwa kuliko mkutano wa Wakuu wa EAC? Mbona in the last 2 years mikutano hiyo imefanyika bila tabu? JK hapimi maneno yake kwenye hotuba kabla hajasema lolote. Alivyosema " miaka" miwili iliyopita alimaanisha nini haswa. Mkutano huo kufanyika Arusha haukupangwa two weeks before. Ni maandalizi ya muda mrefu labda miaka miwili au zaidi. Ni kwa misingi hiyo ili kuhakikisha kuwa venue haibadiliki ilibidi "Lema" "aka" mzee wa maandamano apigwe benchi. Ninakubaliana na Lema kuwa hukumu yake was pre-judged. Hiyo ni hatari kwa ustawi wa utawala bora na utoaji haki wa mahakama zetu. Ninaomba Mungu sana miaka iliyobaki ya JK ipite haraka ili watu wanaoonewa kwa kutofautiana na utawala wake wapate faraja, mzee Mahalu na wengine, nilisoma hata kina babu seya wako kwrnye kundi hilo
 
Watu waliolambishwa tamu na CCM wapepoteza uwezo wa sense organ zote kufanya kazi, hawasikii, hawaoni, hawanusi, wakilamba hawahisi radha yoyote, ngozi ndo imekufa kabisaa! Ningekuwa natazamana uso kwa uso na wewe uvumulivu ungenishinda, nahisi ningetapika kwa hasira.

Hahaahaaa ebwanaeeee! Nashukuru kwa kumjibu maana kanitusi kwelikweli!
 
Mkuu Yericko,

Nilidhani na wewe ni great thinker kumbe hamna kitu unapoteza muda wako kusikiliza ujinga wa Lema kweli Tanzania ni masikini si kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya wananchi wake kuwaamini wanasiasa wa hovyo.
gamba upo kazini,umekunywa maji ya bendera ndo maana huelewi.pole boya mkubwa.
 
Ngongo acha chuki binafsi na Lema, Level aliyonayo Lema kwa sasa may be mpaka unaingia kaburini huwezi ifikia.
Acha kuwa na chuki za wakati uliopita ndugu.
Mungu akuangazie uweze ona nyota ya alfajiri

kweli kaka. Shida ya ngongo ni wivu, roho yake imekaa kama ndoano, hapendi kuona maendeleo ya watu, labda ni mch...i nini maana wao tumba tu
 
nafikiri lema bado ana deni katika hili kupitia waraka wake na ningempa credit za kutosha na kumuona ni shujaa asie na mfano kama tu ange expose kile waliochoongea na mkulu huko o.bey ili kujiridhisha hasa kwa kile alichosema kwamba hukumu ya kesi yake ilikuwa na mkono wa ikulu anyway labda tuendelee kusubiri siku atakapoona itakuwa ni wakati muafaka wa kuweka wazi yaliyotukia kwenye kikao chao..God bless lema

mnapoenda vitani hupeleki vifaa vyote, anasubiri majibu toka kwa mzee wa mipasho, kama sio mzee wa vidole juu kuanza maneno kamanda asingefunguka leo, hizo zilikuwa zana za maangamizi kipindi kijacho
 
Mkuu Yericko,

Nilidhani na wewe ni great thinker kumbe hamna kitu unapoteza muda wako kusikiliza ujinga wa Lema kweli Tanzania ni masikini si kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya wananchi wake kuwaamini wanasiasa wa hovyo.

WE NDO SIYO GREAT THINKER KABISA WE UNATAKA KUWADANGANYA NA WATU WA ARUSHA AMBAO TUNAJUA MBINU ILIYOTUMIKA KUWANUNUA MADIWANI WA ARUSHA NDO ILITUMIKA KWA LEMA IKASHINDIKANA SII HIVYO TU VIONGOZI KADHAA WA CDM ARUSHA WAMEONGWA WAMEKATAA............ kwa hiyo wewe unawaamini ccm ndo maana unamshambulia mtu aliyetoa maoni tofauti na fikra za wana magamba
 
Kama unamwamini mwanasiasa yeyote, nawe pia ni mjinga maana hakuna mwanasiasa asiye wa ovyo.
The unseen is illustrated by the seen.
siyo kweli acha kupotosha kuna wanasiasa ambao ni very smart na kuna wanasiasa wa ovyo na Lema siyo miongoni mwao kwani angekuwa waovyo asingeweza kuwateka watu wote wanaomkubali pia watu wa jiji la Arusha siyo watu wa ovyo useme walichagua mtu wa ovyo ..................... kama huna cha kusema please tulia kijana.
 
Hivi haujagundua Lwaitama anamtusi Lema? na anawatusi vijana wanaoshabikia pasi kujua ukweli?

unamjua Lwaitama?

Ndugu Waberoya ,nimepitia kwa makini waraka wa Dokta.Hakuna mahali amemtusi kamanda Lema.Labda kuna waraka unazungumzia tofauti na huu tunaoufuatilia!
Kilicho dhahiri kwa yeyote kuelewa ni kuwa anahuzunika pamoja nasi kufuatia sakata la kamanda wetu.
Kadiri ninavyoelewa, Dokta atakuwa mtu wa mwisho kumponda Lema na /au mashabiki wake vijana.
Tofauti kabisa na baadhi ya watu ambao wamechagua kuwa neutral Dokta alikwishachagua upande wa mabadiliko kitambo sana.
 
huyo ni mtaalam aliyebobea wa siasa na falsafa.....za afrika na kimataifa...
wengine sisi huku maranyingi ni wafata upepo tuu....
 
huyo ni mtaalam aliyebobea wa siasa na falsafa.....za afrika na kimataifa...
wengine sisi huku maranyingi ni wafata upepo tuu....
 
Ndugu Waberoya ,nimepitia kwa makini waraka wa Dokta.Hakuna mahali amemtusi kamanda Lema.Labda kuna waraka unazungumzia tofauti na huu tunaoufuatilia!
Kilicho dhahiri kwa yeyote kuelewa ni kuwa anahuzunika pamoja nasi kufuatia sakata la kamanda wetu.
Kadiri ninavyoelewa, Dokta atakuwa mtu wa mwisho kumponda Lema na /au mashabiki wake vijana.
Tofauti kabisa na baadhi ya watu ambao wamechagua kuwa neutral Dokta alikwishachagua upande wa mabadiliko kitambo sana.


Lema the former MP,

Umenena maneno mazuri sana ila yale tu ambayo wajinga kama wewe wanawezakuyakubali na wajinga wa kwanza ni wafusi wa chadema wenyewe ambao kwaokukosoana sio desturi

umesema kuhusu mahama umezungumza aibu yako, kesi nyingi zimetokea hivikaribuni ambazo wabunge wa CDM wameshinda kwa hizo hizo mahakama!


Hivi Lema, kusema mimba ya yule dada ilikuwa ya Lowassa ndizo sera za chadema??

you are potential, una attributes zote za uongozi na unatakiwa sana kipindi hikikizuri sana cha kuliokoa taifa letu! Lakini bangi na ujinga wako wa kitoto ndiouliopelekea kusema lolote jukwaani!

why give your enemy a chance? yes you gave him a chance

ni wewe ulikuja humu na kusema Kikwete alitaka ugombee ubunge kwa tiketi ya CCMulikataa , na ukijua kuwa ulivyokuwa TLP ulikuwa mshindi wa pili hilo jimbohaukugundua kwa nafasi kubwa uchaguzi ule ungeshinda wewe??
Ukijua Kikwete ana uadui na wewe na bado uliona dalili za ushindi kwa niniulitumia maneno ya kashfa, matusi au vyovyote usemamvyo wewe

The truth now you are not MP , kikubwa rudi kwenye game na tafuta fomu, kusemamahakama basi CDM wote wangeshindwa why you? kuna jimbo lilokuwa hot kamaubungo?

Mwenzio Mdee tulimuonya mapema sana kuhusu matusi na kama si juhudi za Slaakawe Mdee angepokonywa!!! ilikuwa aibu

CDM wale wafuata mkumbo kutokumkosoa mtu potential kama Lema ni sawa nakuwambia aliyepata 1.3 A-level ya PCB akasome sociology!!

mna watu wazuri ila ujinga kama huu MUONYANE MAPEMA, adui akipata nafasiinakuwa too late

au

Nini faida hii ya Lema kulia ni ikulu wakati si mbunge tena??? anawaumiza naniwananchi wanaompenda kwa ujinga wake mwenyewe....

Uliharibu unachofanya sasa ni sawa kabisa na Maige!! hizo habari za ikulu ni zakufikirika majaji wote walimpania Lema!! kaa chini jifunze

kuwa kiongozi ni pamoja na kubashiri yajayo....kama haukuliona kuwa Kikweteataweka bifu na ngali uliendelea kuongea pumba jukwaani..what are you?

sisi wengine tutasema kweli japo tunawapenda, kamwe sitajivua mimi kuogopakusema ukweli..CCM imefika hapa kwa kutokukosoana!!! watch!

aweke wazi mkutano wao wote kati ya yy na jk, ndicho anachosemalwaitama.....hajaanza kuambiwa leo afanye hivyo....


 
siyo kweli acha kupotosha kuna wanasiasa ambao ni very smart na kuna wanasiasa wa ovyo na Lema siyo miongoni mwao kwani angekuwa waovyo asingeweza kuwateka watu wote wanaomkubali pia watu wa jiji la Arusha siyo watu wa ovyo useme walichagua mtu wa ovyo ..................... kama huna cha kusema please tulia kijana.

Tanzania unaweza ukawa na mashabiki hata kama ww ni mjinga au hamnazo

mifano mingi tusijaze server, kwa tanzania unaweza ukawa 'msanii' na bado ukashabikiwa na uka-wainfluence wanafunzi kuandika mashairi yako kwenye NECTA!!

I will choose all MPs in CDM but not Lema, is just another bogus!! huwezi kusimama jukwaani badala ya kutangaza sera za chama chako au utawafanyia nini, wewe unasema mwanamke yule kapewa mimba na mwanaume yule...yet he is hero??...common guys!!

Thank us by at least restoring your lost senses
 
Hapa naomba niwe msemaji wa lema! Alishawahi sema walidiscuss ugombea wake via ccm na kupewa cheo akapuuzia!

Hamna binadamu wasahaulifu kama wabongo....

Halafu vijanjaaa kumbe hamna kitu.......

Nitaendelea kumuamini Lema mpaka hapo ntakapojiridhisha vinginevyo......

Taifa hili katika hatua ambayo lipo kihistoria ukilinganisha na mataifa mengi makubwa ambayo kwa bahati mbaya sana wasomi wengi sana wanataka kulinganisha kila harakati za nchi hii na hizo nchi zingine ambazo ni kubwa (kiuchumi), hivyo basi ukombozi wetu unategemea sana muamko wa watu katika kusimama na kupinga kwa kiburi kikubwa kukandamizwa na serikali hizi zetu za vibaraka ( kwa IMF na WB)........

Hatua za kujenga msimamo wa namna hiyo kwa watu (UMMA) sio suala la kutumia "usomi" na mbwembwe zingine ambazo wengi wetu mnazitegemea, inahitaji uongozi wa mfano ie hapo ndio Lema anapoingia!


Namuunga mkono Lema!
 
Mwl. Lwaitama na watu wote,

Ni vema ifahamike kuwa Mh. Godless Lema aliupata ubunge katika mazingira magumu sana. Lakini muda mfupi baadaye tulishuhudia vurugu zisizokuwa na sababu na kusababisha fifo vya watu wasikuwa na hatia. Vilevile, mambo yalizidi kuwa magumu kwani watu wachache walitengeneza kesi ya ajabu ambayo wananchi bado tuna mashaka na hukumu ya kumvua ubunge Mh. Lema. Nataka kushawishika kwamba Arusha huenda iliandaliwa kuwa chini ya uongozi wa mbunge wa kiislamu. Pia naona mvutano juu ya Lema ni dalili kwamba maandiko matakatifu katika kitabu ninachokiamini na kukitumia mimi na wengine kina unabii wa kweli juu ya chuki za watu kwa mtu apendaye haki. "Hata wakawashawishi watu waliosema, Tumemsikia mtu huyu akinena maneno ya kumtukana Musa na Mungu.Wakawahatarakisha watu na wazee na waandishi, wakamwendea, wakamkamata, wakampeleka mbele ya baraza. Wakamsimamishia mashahidi wa uongo waliosema, Mtu huyu haachi kusema maneno ya kukufuru juu ya mahali hapa patakatifu na juu ya torati." (Bible=> Matendo ya Mitume 6:11-14). Watu wote mjue hukumu ya kumvua Lema ubunge jimboni Arusha ni sawa na hili la watu na tukio alilofanyiwa mtumishi huyu katika Neno la Mungu. Hata vitendo vya kupigwa bakora au mabomu kwa wakati huu ni mambo yaliyokuwepo tangu zamani.
Kuhusu kumtaka G. Lema aweke wazi mazungumzo ya kule Oysterbay mwaka 2010, ni jambo zuri lakini tusubiri Wakuu wa nchi watasema nini! Hakuna sababu ya kuandika waraka mwingine. Inatosha. Mwisho, Lema hapendwi na vijana wa vijiweni bali anapendwa na wananchi wote wapenda haki hapa Arusha na kwingeneko.Uandikapo kuwa anapendwa na vijana wa vijiweni zaidi ni kumdhalilisha Mtumishi wa Mungu na Mbunge huyu wa kabla ya Aprili, 2012. Je! Unakubaliana na hayo?
 
Wakuu kuhusu lema kukutana na jk ostabey sina mashaka nalo, wengi wenu humu mnamfahamu elisha mkuu wa wilaya ya kishapu jinsi alivyo kisaliti CDM Katika uchaguzi mkuu ulio pita .zikiwa zimebaki wiki mbili kabla ya uchaguzi alijitoa kugombea ubunge kwa tkt ya CDM na kurud ccm baada ya kufanya mazungumzo na jk.
 
Mkuu Mungi,

Mkuu wangu Tanzania ni nchi masikini sana ingawa ina rasilimali kibao.Umasikini wa wananchi wa Tanzania umesababishwa na uongozi mbovu,sera mbovu na wananchi [wapiga kura wengi]wasiojua wajibu wao [inawezekana na wewe umo ndani ya hilo kundi.

Lema amewahi kumshawishi diwani wa upinzani hadi akajiunga na CCM na akashiriki kumpigia debe hadi akashinda.Kama unashangaa Kikwete kuteta na Lema Oysterbay mimi sishangai hata kidogo.

Huwezi kumweka Lema kundi moja na John Mnyika au Tindu Lissu hawa ni mashujaa wangu Lema ni kikaragosi kilichovamia upinzani waTanaganyika kama wewe wakaadaika na usanii wake.Ukitaka kumchambua Lema huwezi kummaliza leo kifupi huyu Bwana hana sifa za kuivusha Tanzania tulipo sasa sana sana atatukwamisha zaidi na zaidi.Lema hana jipya zaidi ya maandamano yasikuwa na tija.


Hakuna mtu mwenye dhambi ambaye atabaki kuwa mwenye dhambi milele, Sauli alikua muuwaji mkubwa wa wakristo lakini baadaye alikua mtume wa Kristo, sasa iweje Lema? Hata yeye sasa ni mwanachadema mzalendo punguza fitina ndugu na chuki binafsi.
 
Back
Top Bottom