LWAITAMA aunguruma juu ya WARAKA wa LEMA kwa Rais Jk! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

LWAITAMA aunguruma juu ya WARAKA wa LEMA kwa Rais Jk!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Yericko Nyerere, Jun 5, 2012.

 1. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #1
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,204
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Nampa pole za dhati Ndugu Godbless Lema. Nilikuwa pale Viwanja vya Jangwani Dar es salaam siku ya Uzinduzi wa Vuguvugu la Mabadiriko (Movement For Change). Maelfu na maelfu ya vijana walionyesha mapenzi makubwa na huruma nyingi kwake.

  Walionyesha kukubaliana na dhana iliyonyuma ya Waraka wa Lema kuwa Mh Lema alidhulumiwa kwa kunyang'anywa Ubunge. Ushauri wangu kwake Mh Lema ni kuwa aandike Waraka wa Pili wa Lema na katika waraka huu wa pili aeleze kwa kirefu na kwa uwazi juu ya mkutano wake na Rais anaosema ulifanyika Osterbay 2010: nani aliomba uwepo mkutano, ulifanyika wapi, na yepi yaliyozungumzwa.

  Namuomba aweke wazi mazungumzo yao na mazingira ya kufanyika kwake. Katika mahakama hii ya nguvu ya umma ni vizuri umma ujue kwa kina kwa nini Mh Lema anadhani anaweza akadhurika ikiwa mkuu amekasirishwa na yeye Lema kutotekeleza waliyokubaliana Osterbay 2010.

  Ndugu yangu Nico Eatlawe nakuomba uusome Waraka wa Lema kama unavyosoma Waraka wa Mitume wa Yesu, "between the lines," na pole vile ukuwepo pale Jangwani Dar es Salaam maana vijana kwa maelfu na maelfu wamemkubali Mh. Lema na Waraka wake ni njia nzuri ya kujiami dhidi ya madhara yanayoweza kumpata kutokana na kukubalika huko.

  Kukubalika kwa Mh. Lema Arusha Mjini sasa kumesambaa nchi nzima baada ya kunyanganywa Ubunge na ili si jambo dogo. Kumbuka Mh Zitto Kabwe umaarufu wake uliubuka kutokana na kusimamishwa Ubunge tu kwa muda lakini Mh. Lema amepigwa na kudhalilishwa na polisi , amewekwa rumande na Mh. Livingstone Lusinde alikejeli kuwekwa kwake rumande.

  Na mwisho wa siku akanyanyanganywa Ubunge mara tu baada ya kuonyesha anapendwa pia hata Arumeru Mashariki. Huyu wako wapambe wa wakubwa wa nchi bila shaka wanaweza wakajituma kumwenyesha hata sumu. Tusipuze uwezekano huu. Tumpe moyo Mh Lema.

  Kumbuka mambao mbali mbali yaliyowahi kuwasibu msusuru wa watu mbali mbali toka Gavana Balali, Harrison Makyembe, Rostam Aziz hadi Edward Lowasa...Mh. Lema anapendwa sana na vijana wa kijiweni na wanamwamini...Tumpe Mh Lema moyo aendelee kuwaelimisha hawa vijana wa kijiweni...

  Tusimzidishie uchungu wake wa haki kwa kudhulumiwa na uonevu wote ambao amepata hadi sasa kwa kumuhukumu hata kabla hajatusimulia kisa kizima tangu Osterbay Oktoba 2010 hadi Arusha tarehe 5 Januari 2011 hadi juzi kuvuliwa ubunge katika mazingira ya kisheria tatanishi.

  Mungu si Athumnai bwana, ipo siku ukweli utashinda uzandiki!!! Ishara kuu yenye kuashiria nyota njema ni kukubalika kwa Mh. Lema kwa maelfu na maelfu ya vijana wa nchi hii.


  Mwl. Lwaitama
   
 2. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Sijaona mngurumo hapo, ni maoni tu.
   
 3. Mzizi wa Mbuyu

  Mzizi wa Mbuyu JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2012
  Joined: May 15, 2009
  Messages: 5,493
  Likes Received: 1,050
  Trophy Points: 280
  Tumemsoma mwanachama wa CCM mfu, kamanda mpiganaji, mzee mwerevu kama tai.
   
 4. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Yericko,

  Nilidhani na wewe ni great thinker kumbe hamna kitu unapoteza muda wako kusikiliza ujinga wa Lema kweli Tanzania ni masikini si kwa bahati mbaya bali ni matokeo ya wananchi wake kuwaamini wanasiasa wa hovyo.
   
 5. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,252
  Likes Received: 19,383
  Trophy Points: 280
  lwaitama ni nani?
   
 6. Graph Theory

  Graph Theory JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2012
  Joined: Jul 2, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 1,112
  Trophy Points: 280
  Kama unamwamini mwanasiasa yeyote, nawe pia ni mjinga maana hakuna mwanasiasa asiye wa ovyo.
  The unseen is illustrated by the seen.
   
 7. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #7
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Yericko kwenye mada yake amejikita kujua nini Lema na Jk walizungumza pale Osterbay
   
 8. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Naanza kupata hofu na UCCM Mfu wa huyu Mzee... Anachojaribu kusema hapa nini????? Kuna wadau wanasema huyu Mzee ni miongoni mwa waoiweka CCM Madarakani... Inasemekana ni miongoni mwa inteligent secrets wa CCM just imagine kwenye makala mmoja ya ZITO alimtaja kuwa tangu akiwa 1st year UDSM walishakuwa wana debate na aina ya Muungano ambao unatakiwa kuwepo......

  Of course huyu mzee kwa Jinsi anavyocritisize CCM asingeendelea kuwa pale UDSM na kuishi kwenye zile Quarters za Chuo....

  Wadau tusaidieni kumchunguza huyu mzee maana ni kama ni wa vuguvugu....
   
 9. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  ninamuombea ulinzi wa mungu kiongozi wangu mwana wa lema! ya mubarak yanamnyemelea jk. vuteni subira.
   
 10. w

  wade kibadu Senior Member

  #10
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  U have provided a very beatiful speech i join with u bro.
  The speech that u have provided to thinkable people he or she will accept ua speech bt to unthinkable people never accept the ua speech.
   
 11. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #11
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,204
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Sawa ndugu, lakini mimi kila ujinga huupitia, kwakuwa naamini hakuna ujinga ulio ujinga mtupu!
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Mkuu Mungi,

  JK na Lema wakizungumza unategemea watazungumza masula ya maana !.


   
 13. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #13
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,204
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Kwa mfumo wa intelijensia ya nchi yetu ni kuwa kila walipo watu kumi mmoja ni nyoka!
   
 14. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #14
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Samahani nimetumia lugha kali sikuwa nia mbaya.

   
 15. H

  Hansen Nasli JF-Expert Member

  #15
  Jun 5, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 881
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 45
  Lwaitama umeanza firisika kimawazo me nilijua utatumia elimu yako uzuri kuchambua mambo kwa kina lakin nawe unaendeshwa kwa ushabiki,punguza mapenz halafu tambua ukweli
   
 16. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #16
  Jun 5, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Jk hana la maana atakalozungumza na Lema. Lema ni mkubwa sana Ngongo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 17. Yericko Nyerere

  Yericko Nyerere Verified User

  #17
  Jun 5, 2012
  Joined: Dec 22, 2010
  Messages: 16,204
  Likes Received: 3,765
  Trophy Points: 280
  Pamoja kamanda ondoa hofu mkuu!
   
 18. m

  mashimbamang'oma Member

  #18
  Jun 5, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 53
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Lema ni special One katika siasa za bongo... Wakitokea watu kumi kama hawa hapa Tanzania... Hii nchi ingeiva... Ila naamin akitumika vizuri huyu mmoja tuliyenaye lazima ipo siku tutamkumbuka kwa jitihada zake... Ndio maana Arusha huwezi kusema lolote juu ya Lema.. Anapendwa na anaishi maisha ya kupendwa...
   
 19. mtotowamjini

  mtotowamjini JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 23, 2012
  Messages: 4,540
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  kama walikutana o'bay itakua kwa waziri mkuu nini? maana wengi wao wanaishi masaki
   
 20. F

  FJM JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Waraka wa Lema unaibua hisia mbaya sana kuhusu viongozi wote wa CCM na serikali yake. Unajenga hisia kwamba labda viongizi wengi (kama sio wote) wamepata vyeo kwa mtindo huu wa ki-oysterbay. Na watu wanaweza ku-test hiyo theory kwa kuangalia kigugumizi kinachowapata CCM kwenye suala la kuwajibika (accountability).

  Bado naamini lilikuwa kosa kwa rais kutaja 'miaka miwili isingewezekana kufanya mkutano mkubwa wa kimataifa Arusha'. Haikuwa lazima sana sana ni kuleta mgogoro.
   
Loading...