Luteni Jenerali Madeline Swegle: Mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,278
Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani.

Ameandika historia kwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na wanamaji na atatunukiwa cheo cha ”Wings of Gold” au ”mbawa za dhahabu”, baadae mwezi huu wa Julai, kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa Alhamisi wiki hii na Mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi..

Mkuu wa mafunzo ya kijeshi alimsifu Bi Swegle akitumia herufi “BZ,” au “Bravo Zulu,”neno linalotumiwa na wanajeshi – wanamaji , linalomaanisha “umefanya vyema.”

“BZ kwa Lt. j.g. Madeline Swegle kwa kumaliza mtaala wa mafunzo ya kimkakati ya kijeshi (ya mashambulio) ya anga,”aliandika Mkuu wa mafunzo ya kijeshi ya ndege za kivita za majini. “Swegle ni mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke anayetambuliwa kuwa rubani wa TACAIR na atapokea Mbawa za dhahabu baadae mwezi huu .

HOOYAH!”, uliandikwa ujumbe wa mkuu huyo wa mafunzo.

Kwa mujibu wa jeshi la majini la Marekani, ambalo limetoa taarifa chache sana kumhusu rubani huyu mpya, Swegle kwa sasa yuko katika kituo cha mafunzi cha Redhawks Squadron (VT) 21 katika kituo cha ndege za vita za wanamaji – Naval Air Station cha Kingsville kilichopo Texas.

Picha ambazo ziliambatana na twitter ya kikosi cha wanamaji ya kusherehekea mafanikio ya kihistoria ya Bi Swegle zilichukuliwa baada ya safari yake ya mwisho ya ndege ya Mkakati wa mashambulizi ya kivita.

Haifahamiki wazi ni wapi Swegle atakwenda baada ya mafanikio hayo, lakini kama mhitimu wa mpango wa mafunzo ataweza kuendesha ndege za mapigano ya kimkakati ya ndege zinazotumiwa na wanamaji wa kijeshi, kama vile the F/A-18E/F Super Hornet na F-35C Lighting II Joint Strike Fighter.

Swegle, ambaye alihitimu katika Shule ya mafunzo ya jeshi la wanamaji nchini Marekani – US Naval Academy , 2017, anafuata nyayo za wanawake wengine mashuhuri wanajeshi kama vile Kapteni Rosemary Mariner, mmoja wa waanzilishi wa jeshi la anga ambaye alikuwa mmoja wa wanawake marubani walioendesha ndege ya mkakati wa kijeshi mwaka 1974.

Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani

Wengine waliomtangulia na kufanya vyema ni pamoja na Sajenti Martha McSally, Luteni Kanali mstaafu wa Air Force ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza katika jeshi la Marekani kuendesha ndege ya kijeshi katika vita, na Luteni Komandoo Brenda Robinson, ambaye alikuwa rubani wa kwanza mwanamke mweusi kuendesha ndege ya majini, mwaka 1980.

Mafanikio ya kihistoria ya Swegle yanakuja wakati kikosi cha majini cha Marekani kikichukua hatua ngumu ya kushughuliakia ubaguzi wa rangi ndani ya kikosi hicho, huku kukiwa na hofu nchini kote Marekani juu ya ukosefu wa haki dhidi ya watu weusi na pia katika utoaji wa ajira.

Mwezi uliopita wakuu wa kikosi cha wanamaji nchini humo walisema: “tulibaini na kuondoa vikwazo vya rangi na kuboresha ujumuishwaji wa watu wa rangi tofauti katika kikosi cha majini .”

Chanzo: BBC Swahili
 
Ubaguzi Marekani kwisha mgumu sana yaani hadi jeshi bado wanatambuana kwa weusi na weupe very sad

Sisi tunao wanawake weusi kibao wanaendesha ndege za kivita.Marekani waje wajifunze kwetu
 
Kwa sababu ni mweusi basi na iwe ajabu kwenye ulimwengu.
ila usisahau kuleta ya mwanamke wa kwanza mweupe kuendesha ndege ya kivita japo haitokuwa habari ya kushangaza kwa kuwa ni mweupe.
 
Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani.

Ameandika historia kwa kupaa angani kama rubani wa ndege ya kivita ya Marekani inayotumiwa na wanamaji na atatunukiwa cheo cha ”Wings of Gold” au ”mbawa za dhahabu”, baadae mwezi huu wa Julai, kwa mujibu wa ujumbe wa twitter uliotumwa Alhamisi wiki hii na Mkuu wa mafunzo ya ndege za kijeshi..

Mkuu wa mafunzo ya kijeshi alimsifu Bi Swegle akitumia herufi “BZ,” au “Bravo Zulu,”neno linalotumiwa na wanajeshi – wanamaji , linalomaanisha “umefanya vyema.”

“BZ kwa Lt. j.g. Madeline Swegle kwa kumaliza mtaala wa mafunzo ya kimkakati ya kijeshi (ya mashambulio) ya anga,”aliandika Mkuu wa mafunzo ya kijeshi ya ndege za kivita za majini. “Swegle ni mmarekani mweusi wa kwanza mwanamke anayetambuliwa kuwa rubani wa TACAIR na atapokea Mbawa za dhahabu baadae mwezi huu .

HOOYAH!”, uliandikwa ujumbe wa mkuu huyo wa mafunzo.

Kwa mujibu wa jeshi la majini la Marekani, ambalo limetoa taarifa chache sana kumhusu rubani huyu mpya, Swegle kwa sasa yuko katika kituo cha mafunzi cha Redhawks Squadron (VT) 21 katika kituo cha ndege za vita za wanamaji – Naval Air Station cha Kingsville kilichopo Texas.

Picha ambazo ziliambatana na twitter ya kikosi cha wanamaji ya kusherehekea mafanikio ya kihistoria ya Bi Swegle zilichukuliwa baada ya safari yake ya mwisho ya ndege ya Mkakati wa mashambulizi ya kivita.

Haifahamiki wazi ni wapi Swegle atakwenda baada ya mafanikio hayo, lakini kama mhitimu wa mpango wa mafunzo ataweza kuendesha ndege za mapigano ya kimkakati ya ndege zinazotumiwa na wanamaji wa kijeshi, kama vile the F/A-18E/F Super Hornet na F-35C Lighting II Joint Strike Fighter.

Swegle, ambaye alihitimu katika Shule ya mafunzo ya jeshi la wanamaji nchini Marekani – US Naval Academy , 2017, anafuata nyayo za wanawake wengine mashuhuri wanajeshi kama vile Kapteni Rosemary Mariner, mmoja wa waanzilishi wa jeshi la anga ambaye alikuwa mmoja wa wanawake marubani walioendesha ndege ya mkakati wa kijeshi mwaka 1974.

Luteni Jenerali Madeline Swegle amekuwa mwanamke wa kwanza Mmarekani mweusi kuendesha ndege ya kivita inayotumiwa na kikosi cha wanamaji cha Marekani

Wengine waliomtangulia na kufanya vyema ni pamoja na Sajenti Martha McSally, Luteni Kanali mstaafu wa Air Force ambaye alikuwa mwanamke wa kwanza katika jeshi la Marekani kuendesha ndege ya kijeshi katika vita, na Luteni Komandoo Brenda Robinson, ambaye alikuwa rubani wa kwanza mwanamke mweusi kuendesha ndege ya majini, mwaka 1980.

Mafanikio ya kihistoria ya Swegle yanakuja wakati kikosi cha majini cha Marekani kikichukua hatua ngumu ya kushughuliakia ubaguzi wa rangi ndani ya kikosi hicho, huku kukiwa na hofu nchini kote Marekani juu ya ukosefu wa haki dhidi ya watu weusi na pia katika utoaji wa ajira.

Mwezi uliopita wakuu wa kikosi cha wanamaji nchini humo walisema: “tulibaini na kuondoa vikwazo vya rangi na kuboresha ujumuishwaji wa watu wa rangi tofauti katika kikosi cha majini .”

Chanzo: BBC Swahili

Hawezi kumaliza shule mwaka 2017 halafu leo akawa Luteni Generali; bado ni mdogo sana

1594733302915.png

Huyo anaitwa Lieutenant Junior Grade (Lt.J.G) ambayo ni kama Second Liutenant hapa kwetu, yaani ndiyo anaaza kuwa afisa wa jeshi.
 
Luteni Generali anafanya missions bado??

Ndo kwanza katoka kujifunza Type Rating??? angalia vizur taarifa yako
 
Hawezi kumaliza shule mwaka 2017 halafu leo akawa Luteni Generali; bado ni mdogo sana

View attachment 1506576

Huyo anaitwa Lieutenant Junior Grade (Lt.J.G) ambayo ni kama Second Liutenant hapa kwetu, yaani ndiyo anaaza kuwa afisa wa jeshi.
... hata mimi nilishangaa ; Luteni Generali (3-start general) kuwa rubani wa ndege vita? Maajabu kweli kweli. Yaani kabisa wamjazie jenerali mabomu kwenye ndege halafu aelekezwe kwenda kupiga S-400? Hizo ni kazi za "nyoka" sio za majenerali jamaa umemstukia na matango pori yake.
 
Huyo ni Luteni, Luteni Jenerali ni kitu kingine kabisa.
... sure; Lt. Generals are high rank; very senior officers; 3-star generals just below 4-star or full generals and 5-star or marshals of the army.
 
Kwani wakenya Wanasemaje.
Sio m-luya au mkikuyu huyu Dada.
 
Back
Top Bottom