Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 2,205
- 4,695
Ni habari ya kushtua sana ya kifo cha Jasusi mbobezi.
Taarifa kutoka vyanzo vya kuaminika zinathibitisha kuwa Jaques Musemakweli Lt Jenerali wa Jeshi la Ulinzi Rwanda amefariki huku sumu ikihusishwa na kifo chake.
Mwendazake aliwahi kuongoza Idara nyeti ya ujasusi almaarufu Directorate of Military Intelligence (DMI), Mkuu wa Kikosi cha Ulinzi wa Rais na Mkuu wa Utawala Jeshini.
Kabla ya kifo chake alihudumu katika nafasi ya Inspector General wa Jeshi la Rwanda
Taarifa za uhakika zinaeleza Mwendazake alikuwa mtu wa karibu sana na Rais Kagame hadi umauti unamkuta.
Kifo chake kimemshtua sana Rais Kagame aliyeagiza uchunguzi (Autopsy) ufanywe mara moja
Serikali ya Rwanda imetoa taarifa kuthibitisha kifo chake.
Luteni Generali huyo alifariki Februari 12, 2021 majira ya saa 1:30 AM kwa saa za Rwanda.
Ukaribu wa mwendazake na Rais Kagame inadaiwa ulileta chuki dhidi yake kutoka kwa baadhi ya Majenerali wa nchi.
Source: Vyanzo mbalimbali kutoka Rwanda + Jeshi la Rwanda