Lusinde kushangiliwa na Wabunge wa CCM ni mkakati wa chama chao au ni upofu wa mawazo?

Chakaza

JF-Expert Member
Mar 10, 2007
39,758
71,139
Tumeshuhudia leo hii yule Mbunge mashuhuri kwa kusema bila kufikiri bw Lusinde akibwabwaja maneno ya hovyo hovyo huku akishangiliwa kwa nguvu na wabunge wengi wa CCM pamoja na mawaziri.
Hili limenishangaza sana kuona pamoja na kuelewa jinsi Lusinde anavyo kiharibia chama chao katika jamii ya watanzania bado wanadirika kumshangilia bila aibu wala woga.
Jee hii inaweza kuwa mikakati iliyowekwa na Chama kumtumia Lushinde kwa vile anaweza kuzungumza lolote bila aibu kuutukana upinzani na wabunge hata wale makini kulazimishwa kumpa support?
 
kwani wana kipi cha kushangilia tena wanachokijua zaidi ya matusi. Hata huku nje mbona wanashabikia matusi tu. We huoni Nape kuwaita wanachama wao Oil chafu ni lugha ya staha hiyo kumuita mtu alikupigia kura juzi mwaka 2010 Oil Chafu
 
Kwa hiyo Wabunge wa CCM wanamshangilia kwa shangwe kwa viele zile kauli ni za chama?
 
yule ndo piere issa wao,mzee wa og ila kwa vile ccm wanataka nyavu zitingishike hata kama ni zao hawajali.
 
That's the best they have! Si unaona nchi iliko?
Serikali gani uliona inaomba misaada karibu nusu ya bajeti yake lakini wakati huo huo wanatoa msamaha wa kodi kuzidi kile wanachoomba?
 
lusinde anatuhumiwa na kuhisiwa kujihusisha na wizi wa mamilion BOT.. Kimsingi sioni haja ya wana ccm kumsifia watakuwa wanashabikia ujinga na si kitu chema.. Kamwe..
 
Wanaoshangilia na anayeshangiliwa, wote uwezo wao wa kufikiri uko sawa na umefikia kikomo!!!!
 
ciciem woote ni hovyo tuu ndio maana tunasema 2015 tutapiga chini woote.. na kuna baaadhi ya majina hii nchi ndio yatafutika hivyo kwenye siasa kama hawa kina lusinde
 
Back
Top Bottom