Lusinde adai Spika anaelekezwa na chama kuwatoa wabunge wa upinzani Bungeni

MWITONGO MAARIFA

JF-Expert Member
Aug 11, 2018
276
1,428
Kijana Lusinde ameeleza kuwa chama Cha Mapinduzi kimekuwa kikizuia wananchi wa maeneo yaliyowachagua wapinzani kupelekewa miradi ya maendeleo kwa lengo la kuwafanya wananchi wakasirike na kuacha kuwachagua viongozi wa upinzani. Ameyasema hayo kwenye kampeni za Ubunge ukonga na kuongeza kuwa katika majimbo ya wapinzani wapo Watanzania lakini wanapaswa kujutia maamuzi na ya kuchagua upinzani na uchaguzi mwingine wachague CCM.

Ameendelea kusema kuwa wao ndani ya chama ukaa kwenye vikao na kusikiliza hoja za mawaziri na pale inapoletwa hoja ya kuwapelekea maendeleo wananchi waliokatika majimbo ya upinzani waziri husika uelekezwa kuhamishia miradi hiyo kwa majimbo ya chama tawala.

Kuhusu wabunge wa upinzania kuchachama Bungeni, amesema kuwa chama utoa maelekezo kwa Spika kwamba Mbunge yeyote wa upinzani anayebainika kujenga hoja na kupingana na matakwa ya chama tawala lazima atolewe ndani ya Bunge.

Swali langu kwa uongozi wa Bunge, kauli hizi kwao hawaoni Kama zinaondoa kabisa tafsiri ya Bunge na kubakia kuwa chombo au taasisi ya chama Tawala?Ni wakati gani muhimili huu unakuwa independent kama umekuwa ukiingiliwa na kufanya maamuzi kwa matakwa ya watu wachache ambao kwao chama ndio kipaombele na siyo Watanzania?

Haya yanatamkwa hadharani kwa sababu viongozi wa muhimili huu wameshindwa kabisa kutenganisha Bunge na itikadi zao za vyama na nilitegemea suala kama la Lusinde likemewe na watu wote wakiwemo viongozi wa Bunge lakini Hadi Sasa kimya.

Ngoma ikivuma Sana inakaribia kupasuka, CCM inaona ufahari kwa haya yanayotokea lakini kisiasa wanajichimbia kaburi maana haki ikipokonywa kwa wananchi itapokonywa pia kwa viongozi wa siasa na hivyo wanaoishi Kama malaika leo kesho wataishi kwa kusaga meno. It's just a matter of time and if you don't believe ask Sumaye, Lowasa, Mwigulu, Nape, Mrema, Marando, Mwandosya, Mwapachu, Msalimie seif etc, Waliamini kuhusu CCM lakini baadaye CCM iliwakataa na waliporudi kwa wananchi wanaumizwa na mfumo walioutengeza wao.
 
Hivi TRA hawana namna ya kudhibiti hawa wanasiasa uchwara? Au hawaoni Kama hawa wanasiasa uchwara wanafifisha juhudi zao za kuwataka watanzania walio wengi wajisajiri na kuendelea kulipa kodi
 
Hivi TRA hawana namna ya kudhibiti hawa wanasiasa uchwara? Au hawaoni Kama hawa wanasiasa uchwara wanafifisha juhudi zao za kuwataka watanzania walio wengi wajisajiri na kuendelea kulipa kodi
Nadhani umefika wakati muafaka sasa kuishitaki sisiyemu kwenye mahakama za haki za binadamu watufafanulie juu ya hii habari
 
Unadhani mtu kama Lusinde akipewa kipaza sauti ataongea nini zaidi ya hayo aliyoyaongea? Na huo ndio msimamo wa awamu ya tano, ubaguzi ni ajenda kuu. Utadhani kodi zinalipwa na wanaCCM peke yao.
Lkn naamini kuwa mwisho wake utakuja kuwa ni majuto na kusaga meno na kilio kukubwa sana
 
Kweli Watanzania tutakuwa tumerogwa.Hii ni dharau sana kwa wananchi wenye vyama na wasio na vyama.Anachoongea ni kweli kabisa.Huku Mbeya sijaona mradi mpya wowote wa maana toka Jk ametoka madarakani.Hivi maprofesa na maPhD ya ccm kweli wanakubaliana na uhuni kama huu.Kweli ndo imekuwa hoja ya kupigia kampeni hii.Kweli Watanzania hatuna haya.Tunajiamiani kupitiliza aisee.
 
Tatzo tulilo nalo Watz ni unafiki,uoga, ujinga, umbumbumbu na uzezeta wa kiwango cha Lami...!!.
Ndugu zetu wa Uganda au Kenya huwa wako tofauti sana na Wanajitambua. Pale inapotokea Serikali kuwafanyia au kumfanyia mmojawao mambo ya kihuni huwa wanachukua maamuzi ya kupinga ujinga na upuuzi!!

Ukija Tanzania ni vichekesho. Tundu Lissu alifanyiwa unyama na udikteta uliopotiliza lakini cha ajabu mpaka leo Watz wamekaa kimya kama makondoo na leo hii ni mwaka 1 huku TL anaendelea kuuguza majeraha nchini Ubelgiji kwa gharama zake na misaada binafsi na Watz kimyaaaaa!!!Hii ni aibu.
.
Uganda Bobi Wine na Wabunge wengine wa Upinzani walifanyiwa unyama kama unaofanyika hapa Tanzania. Lakini RECTION yake. misimamo na kupaaza sauti kwa Waganda kuiambia Dunia kilichotokea na leo hii Bobi Wine yuko USA kwa matibabu kwa gharama za Serikali. Tayari Bobi Wine ameshaongea na media za Ughaibuni na dunia yote imejua kile M-7 anawafanyia Waganda na hatua zimeanza kuchukua na Bunge la EU.
 
Kweli Watanzania tutakuwa tumerogwa.Hii ni dharau sana kwa wananchi wenye vyama na wasio na vyama.Anachoongea ni kweli kabisa.Huku Mbeya sijaona mradi mpya wowote wa maana toka Jk ametoka madarakani.Hivi maprofesa na maPhD ya ccm kweli wanakubaliana na uhuni kama huu.Kweli ndo imekuwa hoja ya kupigia kampeni hii.Kweli Watanzania hatuna haya.Tunajiamiani kupitiliza aisee.
kodi. zenu. twachukua. maendeleo twapeleka kwingine. hiki chama. ni zaidi. ya genge la uporaji.
 
Kweli Watanzania tutakuwa tumerogwa.Hii ni dharau sana kwa wananchi wenye vyama na wasio na vyama.Anachoongea ni kweli kabisa.Huku Mbeya sijaona mradi mpya wowote wa maana toka Jk ametoka madarakani.Hivi maprofesa na maPhD ya ccm kweli wanakubaliana na uhuni kama huu.Kweli ndo imekuwa hoja ya kupigia kampeni hii.Kweli Watanzania hatuna haya.Tunajiamiani kupitiliza aisee.
Mkuu sema lusinde na kundi lake ndio wanastahili kuitwa hayo majina maana ukisema watanzania unatuonea sisi wengine tusiyo na vyama wala hatujihusishi na siasa za maji taka
 
Back
Top Bottom