Nilipata bahati ya kutembelea Lushoto mwaka jana mwanzoni na kunahitaji msaada wa serikali. Ukitokea mombo mpaka Lushoto mjini ni kuzuri na kuna barabara lakini ukienda vijijini maisha ni magumu, hakuna maji, barabara wala umeme kwa ufupi ni porini!. Ni vigumu sana kwa wananchi kwani huwezi kuchumba visima kwenye milima mikubwa, na hata barabara ni mbovu sana. Serikali ningeshauri waweke barabara mpaka kule juu mlimani kuimarisha utalii na kusaidia wananchi va vilevile wasaidie kwenye kuleta maji na umeme.