Lusekeko: Kikwete avutia pumzi suala la Dowans | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lusekeko: Kikwete avutia pumzi suala la Dowans

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Jan 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Lusekeko: Kikwete avutia pumzi suala la Dowans


  na Betty Kangonga


  [​IMG] MCHUNGAJI wa Kanisa la GRC Ubungo Kibangu, Dar es Salaam, Anthony Lusekelo, amesema anaamini Rais Jakaya Kikwete bado ana nafasi ya kuzungumzia suala la ulipaji wa fidia wa sh bilioni 185 kwa Kampuni ya Dowans.
  Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu, Lusekelo alisema suala hilo ni zito na linahitaji kutafakari zaidi hasa ukizingatia kauli ya Rais Kikwete ndiyo ya mwisho.
  Alisema jambo hilo halikwepeki, Rais Kikwete ni lazima alifafanue suala hilo kwa wananchi, kwa kuwa limesababishwa na uzembe wa baadhi ya viongozi wa serikali.
  “Rais Kikwete atakapozungumza ndiyo inakuwa kauli ya mwisho labda inawezekana hakutaka kukurupuka au anasubiri wananchi wote wazungumze, lakini kulifafanua hili ni lazima kwani wananchi wanahitaji kauli yake,” alisema.
  Alisema hatua ya kulipa mamilioni ya fedha kwa Dowans linahitaji tafakari zaidi maana suala hilo linahusu ufisadi na linagharimu ulipaji wa fedha nyingi kwa wamiliki wa kampuni hiyo ambao hawajafahamika.
  Aliongeza kuwa Rais Kikwete atakapotoa kauli yake katika hilo inawezekana wale waliohusika na uzembe wa kimkataba wakachukuliwa hatua kutokana na kusababisha hasara kwa taifa.
  Juzi katika hotuba yake ya salamu za mwaka mpya, Rais Kikwete ameshindwa kugua suala hilo ambalo limetikisa nchi miaka miwili iliyopita na hivi karibuni Mahakama ya Migogoro ya usuluhiishi imeamuru TANESCO kuilipa Kampuni ya Dowans sh bilioni 185.
  Ulipaji wa fidia hiyo unafuatia uamuzi uliotolewa na mahakama hiyo Novemba 15 mwaka jana, chini ya Mwenyekiti Gerald Aksen na wasuluhishi Swithin Munyantwali na Jonathan Parker.
  “Jopo la wasuluhishi limeamuru zaidi ya sh bilioni 36 (dola za Marekani 24,168,343) na riba ya asilimia 7.5 kwa mwaka inayofikia kiasi cha zaidi ya sh bilioni 26 (dola za Marekani 19,995,626) tangu Juni 15, 2010 hadi fidia hiyo itakapolipwa,” ilieleza sehemu ya uamuzi huo.
  Pia jopo hilo la wasuluhishi wa migogoro ya kibiashara liliamuru sh bilioni 60 (sawa na dola za Marekani 39,935,765) na riba ya kiasi cha asilimia 7.5 ambayo ni sawa na sh bilioni 55 (dola za Marekani 36,705,013.94) zilipwe kuanzia Juni 15, 2010 hadi wakati wa malipo.
  Jopo hilo lilisisitiza kuwa ada na gharama za wasuluhishi na za utawala sh bilioni moja (dola za Marekani 750,000) kwa wasuluhishi wa ICC zinatakiwa zilipwe na pande zote husika, yaani TANESCO na Dowans.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,806
  Likes Received: 420,364
  Trophy Points: 280
  Kuzungumza tu hakutoshi.........................Tunataka wote ambao walihusika katika kulitia taifa hasara hii wafikishwe mahakamani kwa makosa ya "criminal negligence" na walipe gharama zote hizi kutoka mifukoni mwao.....
   
 3. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Hiki kitendawili sijui kitateguliwa lini
   
 4. m

  mzambia JF-Expert Member

  #4
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Siyi hivyo kwa nini isipitishwe sheria wote waliohusike wanyongwe hadharani mpaka wafe hapo ufisadi unaweza ukakoma.
   
 5. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #5
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Mh!si suala gumu kulishughulikia kama yeye ni msafi na hakuhusika kwenye sakata hilo,lakini ni vigumu kushughulikia kama na yeye alikuwa sehemu ya tatizo lenyewe!!
   
 6. m

  mbezibeach Senior Member

  #6
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 4, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukiona kikwete kitu anakivutia pumzi ujue ndio imetoka hiyo...Huyo Lusekelo nadhani hamfahamu vizuri Rais wake.. Kwani ni mambo mangapi na yenye maslahi makubwa kwa Taifa ambayo mpaka leo bado Mkwere amekaa kimya na kuacha taifa likiingia katika malumbano yasiyo na msingi...RADAR anavuta Pumzi....KAGODA anavuta pumzi...MEREMETA anavuta pumzi...DOWANS nayo azima avute pumzi....

  UKIPANDA MIHOGO USITARAJIE KUVUNA MAHIDI - Muumin Mwinjuma.
   
 7. Shapu

  Shapu JF-Expert Member

  #7
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 17, 2008
  Messages: 1,922
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Huyu mchungaji sioni ni nini kaongea... kwanza wala haelewi what the issue is on DOWANs. Eti kauli ya raisi kikwete ndo ya mwisho! ya mwisho wa nini?? anataka kuwa kama AG Warema eti kafunga mjadala wa Dowans? Mwisho upi? Hebu mchungaji acha kujipendekeza, kafanye homework yako ndo uonge. Njoo hapa JF kuna nondo za kutosha ili uweze toa hizo sentensi zako si kuongea tu kwa kujipendekeza.

  By the way ule mpango wako wa kutaka kutambulika kama maaskofu na serikali wa pamoja na kupewa pass za kidiplomat umeishia wapi? nilikusikia ukilalamika sana serikali inaubaguzi kwamba wewe hutambuliki, umetambulika sasa??
   
 8. Lekanjobe Kubinika

  Lekanjobe Kubinika JF-Expert Member

  #8
  Jan 3, 2011
  Joined: Dec 6, 2006
  Messages: 3,067
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  JK hawezi kuongelea hilo ikiwa naye ni mdau katika malipo hayo kwa namna moja au nyingine. Mbona swala la TANESCO na bei juu alilisemea, kwani hakuna uhusiano kati ya DOWANS na bei za umeme za TANESCO kuwa juu kwa sasa? Unao ujasiri gani kuukata mkono unaokusababisha uende chooni kila siku?
   
 9. Rugaijamu

  Rugaijamu JF-Expert Member

  #9
  Jan 3, 2011
  Joined: Jul 10, 2010
  Messages: 2,833
  Likes Received: 556
  Trophy Points: 280
  Naamini jk hawezi kulizungumzia tena suala hili,kipi kilimzuia asiliunganishe na suala la kupanda kwa bei ya umeme?Kikwete mwenyewe sio msafi so hawezi kuanzisha 'ugomvi wa mawe' ilhali anaishi nyumba ya vioo.Pia huu ni mpango wa ccm kurudisha mabilioni waliyotumia kwenye uchaguzi uliopita.
   
 10. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #10
  Jan 3, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kama alikumbuka bei ya umeme atasahau dowanz?c vyote vnaihusu tanesko,ala
   
Loading...