Lundenga: Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu ni miss halali mwenye vigezo vyote | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Lundenga: Miss Tanzania 2014 Sitti Mtemvu ni miss halali mwenye vigezo vyote

Discussion in 'Entertainment' started by GIBA KB, Oct 21, 2014.

 1. GIBA KB

  GIBA KB JF-Expert Member

  #1
  Oct 21, 2014
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 369
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  [​IMG]

  Muda mfupi uliopita,Lundenga akiongea na waandishi wa habari amesema Miss TZ 2014-2015 ana miaka 23 na hana masters ana degree.Kwa maelezo hayo anafaa kuwa miss Tz na hatavuliwa taji.

  Mwaka 2005 kulikua na ushindani kidogo, mwaka 2006 kulikua na ushindani wa Wema na Jokate na upinzani huu umeendelea kuwepo kwenye mashindano yetu lakini ya mwaka huu imezidi mno, kumekua na matusi.kashfa na hata naona wamevuka mpaka na kuingiza mambo ya kisiasa ambayo sisi hatuyapendi, huu ni mchezo kama mchezo mwingine wowote… yani taji la mwaka mmoja limefunika mpaka katiba na Simba na Yanga?

  Hayo ni maelezo aliyoyatoa Mr. Hasheem Lundenga mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam October 21 2014 kuhusu ishu ya Miss Tanzania ambae aliandikwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo mrembo huyu kudanganya umri, elimu na mambo mengine.

  Yafuatayo ni mambo waliyoyasema Hasheem Lundenga na Miss Tanzania Sitti.

  ‘Walidai kwamba Miss Tanzania ana mtoto baada ya kutoka picha moja akiwa na mtoto, nasema katika utafiti wetu sisi Miss Tanzania hana mtoto na mwenye vithibitisho halali kwamba ana mtoto atuletee, kama kuna uthibitisho wa cheti cha kuzaliwa cha mtoto….. leta hicho cheti'– Lundenga

  ‘Hili la sisi kuchukua rushwa kutoka kwa baba wa Sitti, Abbas Mtemv.jamani hii ni stori ya kijingajinga, ni mambo ya kipumbavu sana kuandika haya mambo, hamjui taratibu zetu tunavyowapata majaji na wanavyofanya kazi…Majaji huwa wanatafutwa siku nne za mwisho na huwa hakuna mtu anajua atakua Jaji na huwa tupeleka majina 15 BASATA na wao ndio wanaturudishia majina tisa ya Majaji waliopitishwa' – Lundenga

  Magazeti mbalimbali yameripoti kwamba Sitti alikua na Masters, ukweli ni kwamba katika fomu tulizonazo sisi Sitti hajaandika hata sehemu moja kwamba amesoma mpaka Masters, swala la Masters limetoka wapi? ni uongo huo' - Lundenga

  ‘Kuhusu swala la yeye kuzungumza kifaransa, mtu anajua lugha ya kimataifa mbona kwenye mashindano ya dunia wanazungumza Kifaransa na lugha nyingine? lakini mbona hata kwenye fainali alijibu kwa Kiingereza pia? Kifaransa zilikua ni mbwembwe kuwashawishi Majaji, na kweli walishawishika na ndio maana akashinda' – Lundenga

  ‘Jingine ambalo ni kubwa zaidi ni swala la umri lililozungumzwa sana, katika mashindano yetu washiriki wote hujaza fomu na kuandika tarehe ya kuzaliwa, fomu ya Sitti hii hapa na inaonyesha amezaliwa May 31 1991 kwa hiyo alitimiza masharti ya kushiriki kwa kuwa ana umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 24′ – Lundenga

  ‘Wote walioshiriki Miss Tanzania 2014 akiwemo Sitti walituletea vyeti vyao Original vya kuzaliwa tarehe 13 na kisha tukatoa nakala kupitia hivyo vyeti vyao Original' – Lundenga

  ‘Sisi kazi yetu sio kupeleleza sana, tukipata information chache zinatutosha… kama mtu anatatizo na hiki cheti cha Sitti cha kuzaliwa akafanye utafiti, ukipata ukweli tuletee sisi lakini kazi ya uchunguzi sio ya kwetu' – Lundenga

  Baada ya Lundenga kuongea, Miss Tanzania 2014 Sitti nae aliongea machache kwamba ni kweli ana umri wa miaka 23 vilevile cheti chake cha kuzaliwa kilipotea sababu amekua akisafiri mara kwa mara' -Sitti

  Waandishi wa habari walipotaka awaambie na uthibitisho kama aliripoti Polisi kuhusu kupotea kwa cheti chake, Sitti alisema ‘sikutegemea haya maswali leo kwahiyo sikuja nimejiandaa kihivyo, kama mtakua mnahitaji kunihoji mnaweza kupanga siku yenu na mkanihoji' – Sitti

  Kuhusu yeye kuwa na mtoto Sitti amejibu kwa ufupi kwa kusema >>> ‘Nadhani inajieleza kama Muheshimiwa alivyosema kwamba sina mtoto na mkitaka tunaweza kwenda Hospitali kwa sababu naona kama mnaniandama kwa vitu ambavyo sio vya kweli'

  Kuhusu ukweli kama hati ya kusafiria pamoja na leseni ya gari vilivyosambazwa mitandaoni ni kweli vikionyesha kwamba amezaliwa mwaka 1989, Sitti amesema ‘Sitogusia hilo swala sababu nilivyokua nakuja kuomba Miss Tanzania niliomba cheti cha kuzaliwa, hivyo vitu vingine ni maisha binafsi…. kwahiyo sidhani kama na nyie mngependa kuona mtu anachukua leseni ya gari au Passport iwe ya kweli ama feki na kuiweka kwenye mtandao'


  Chanzo: millardayo.com


  Post update : Video

   
 2. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #2
  Oct 21, 2014
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,355
  Likes Received: 703
  Trophy Points: 280
  je, ameleta vielelezo gani katika kuthibitisha hayo aliyoyasema!?
   
 3. mwanaapolo

  mwanaapolo JF-Expert Member

  #3
  Oct 21, 2014
  Joined: Mar 14, 2014
  Messages: 256
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 35
  Ushahidi je?
   
 4. Mzito Kabwela

  Mzito Kabwela JF-Expert Member

  #4
  Oct 21, 2014
  Joined: Nov 28, 2009
  Messages: 17,455
  Likes Received: 1,618
  Trophy Points: 280
  Lundenga kuna siku atampandisha mkewe agombee umis
   
 5. GIBA KB

  GIBA KB JF-Expert Member

  #5
  Oct 21, 2014
  Joined: Jul 3, 2012
  Messages: 369
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Amesema ushahidi huo ulitolewa mtandaoni sio sahihi
   
 6. cute datty

  cute datty JF-Expert Member

  #6
  Oct 21, 2014
  Joined: Jul 11, 2014
  Messages: 581
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Mbona hajatoa hoja za kutu convince kuwa hajamuuzia taji kama inavyosemekana.Au wewe mleta mada ndo hujatuainishia vizuri.Ushahidi tafadhali.
   
 7. Ngirimaji

  Ngirimaji Senior Member

  #7
  Oct 21, 2014
  Joined: Oct 5, 2014
  Messages: 187
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 45
  He he he raha jamani' watu wameweka Document kama vithibitisho yeye analeta maneno' Doc speak for itself' miss alikua anaona rahaaa kujaza jaza pasport' leseni ya mbele na kujiweka weka mtandaoni pasipo kuwa na malengo. Brother Hashimu amebugi thic tym
   
 8. hyusuph

  hyusuph JF-Expert Member

  #8
  Oct 21, 2014
  Joined: Dec 5, 2013
  Messages: 1,490
  Likes Received: 271
  Trophy Points: 180
  Nasikia mkewe ni miss mbona alioaga miss tanga wa enzi zilee
   
 9. Mr.Junior

  Mr.Junior JF-Expert Member

  #9
  Oct 21, 2014
  Joined: Sep 8, 2013
  Messages: 7,626
  Likes Received: 3,332
  Trophy Points: 280
  Tushawazoea kila kitu ubabaishaji.

  Lakini ukweli utabaki palepale.
   
 10. komunte

  komunte Member

  #10
  Oct 21, 2014
  Joined: Aug 24, 2012
  Messages: 48
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 13
  Lundenga si astaafu tu..!!
  Tumeshamchoka..!! Kama Vip chadema watangaze maandamano nchii nzima kumpinga Lundenga..!!
   
 11. Paula kilaki

  Paula kilaki JF-Expert Member

  #11
  Oct 21, 2014
  Joined: Jun 26, 2014
  Messages: 1,916
  Likes Received: 225
  Trophy Points: 160
  heee kwa hiyo ametoa maneno matupu bila evidence yoyote na wanahabari wakakubali??? so ile paspot na lesen imefojiwa??? sasa hapo si alipaswa kuonesha original jamani??? mmmmmh!!! makubwa haya
   
 12. Mawenzi

  Mawenzi JF-Expert Member

  #12
  Oct 21, 2014
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,268
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huyu msichana lazima ana birth certificate. Iko wapi? Ina maana mamaake mzazi ni mwongo?
   
 13. kimugina

  kimugina JF-Expert Member

  #13
  Oct 21, 2014
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 1,097
  Likes Received: 88
  Trophy Points: 145
  ha ha ha Asante Lundenga tuna shukuru sana,,

  Apo ndio kamiliza tayari???
   
 14. Kibo10

  Kibo10 JF-Expert Member

  #14
  Oct 21, 2014
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 11,191
  Likes Received: 3,010
  Trophy Points: 280
  Lundenga amesema hakuna suala la yeye kupewa rushwa, ila Sitti Mtemvu ameshinda kihalali kwa kupitishwa na Majaji.
  Juu ya tuhuma za unene amesema wao huwa hawaangalii wembamba wala ufupi, muhimu ni awe na vigezo vinavyotakiwa.
  Kuhusu suala la passport na leseni zikionesha Sitti amezaliwa 1989, Lundenga amesema wao huwa hawangaali vitu hivyo.
  Lundenga amesema kuwa cheti halali walichonacho wao ni kile kinachoonesha Sitti Mtemvu kazaliwa 24 mei 1991.
  Nafungua mjadala miss TZ 2014.
   
 15. MasterP.

  MasterP. JF-Expert Member

  #15
  Oct 21, 2014
  Joined: Jun 5, 2013
  Messages: 4,001
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  Angeleta wa kwake ambao ni sahihi tungemwelewa na si kuja na maneno matupu....
  Kimeshanuka tuu huyo miss ni ajuza
   
 16. Amalinze

  Amalinze JF-Expert Member

  #16
  Oct 21, 2014
  Joined: May 6, 2012
  Messages: 5,918
  Likes Received: 2,480
  Trophy Points: 280
  Imekaa safi sana hii.
   
 17. Going Concern

  Going Concern JF-Expert Member

  #17
  Oct 21, 2014
  Joined: Jul 25, 2011
  Messages: 931
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 60
  kitendo tu chakusema alikua na miaka 18 then tukaja kujua ana 23 tayari alikua keshapoteza sifa. kama miaka 23 anasifa yakugombea why alisema ana 18? poor us...
   
 18. Kibo10

  Kibo10 JF-Expert Member

  #18
  Oct 21, 2014
  Joined: Aug 20, 2013
  Messages: 11,191
  Likes Received: 3,010
  Trophy Points: 280
  Binafsi naona siasa zimeingia kwenye mashindano ya urembo.
   
 19. MasterP.

  MasterP. JF-Expert Member

  #19
  Oct 21, 2014
  Joined: Jun 5, 2013
  Messages: 4,001
  Likes Received: 1,631
  Trophy Points: 280
  Another drama....
  So ile passport yake na Leseni vyote ni feki ama?
   
 20. MANI

  MANI Platinum Member

  #20
  Oct 21, 2014
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,310
  Likes Received: 1,708
  Trophy Points: 280
  Duuh au anaona aibu kujirudi. Sasa kwenye miss world ataenda na passport nyingine.
   
Loading...